Kusoma atlas ilikuwa raha sana

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakati nipo mdogo mzee wangu aliniachia atlas. ilikuwa ya kiswahili na picha nzuri sana. Basi nikiisoma nilikuwa najenga picha hiyo sehemu ikoje napata raha sana.
Kuna haya majina yalikuwa yananifurahisha sana.
Kampuchea ni Laos au Cambodia.

Korongo kuu, nilikuwa nawaza likoje hilo korongo kumbe ndiyo grand canyon.
Kuna korongo la kifo/ndiyo death valley, hili lilikuwa linaniogopesha sana.

Kusoma atlas inafanya kufuatilia habari na movies iwe rahisi.
Jamaa mmoja aliniambia ndugu yake yuko ulaya, nikamuuliza nchi gani akasema sijui ila kuna nchi inaitwa ulaya?!

Mwingine ananiambia Marekani kubwa sana, mfano toka Calfornia hadi Los Angeles si mchezo!?

Umewahi penda kusoma atlas?
 

Mimi mpaka leo nastaajabu hii ramani ya kale sana iliyo accurate kama vile ilichorwa kwa technology ya GPS ikionyesha Antarctica kuwa haikuwa na barafu na binadamu waliishi huko.
Hii ni ramani ya mwaka 1513 na alikuwa anaimiliki General wa jeshi la Uturuki.
 
Nimesoma sana enzi hizo, na jamaa zangu tunashindana kutafuta sehemu.

Anakwambia nitafutie Laos, unatafuta wee ukikosa anakuonesha, hapo unakuwa umeshindwa.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ulikuwa usomaji wetu na rafiki zangu enzi hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…