Kusoma Bachelor ya Sheria kutokea Diploma

Kusoma Bachelor ya Sheria kutokea Diploma

nsharighe

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
1,441
Reaction score
2,220
Wakuu nawasalimu .

Nina mdogo wangu ana ndoto ya kuwa mwanasheria/wakili. Baada ya kumaliza advance level mwaka jana akapata division 2 ya points 12'

Lengo afanye Diploma ya sheria kisha degree.

Naomba mnipe msaada wa mawazo, kwa ufaulu wake ni vyema afanye anavyotaka, na faida na hasara za kufanya diploma kisha degree.. pia chuo gani anaweza kuomba kutimiza ndoto yake.

Nawasilisha, pia mnisamehe kwa kuleta uzi huu jukwaa la sheria na sio Elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa mpe hongera kwa kuchagua moja ya fani chache ambazo utakachosoma ni kweli utakitumia katika maisha na kazi zako. Maana Tanzania kuna fani nyingi sana ambazo vitu unavyosomea chuoni wala hutavitumia kwenye kazi wala maisha yako.

Baada ya hilo nikuulize swali - kama amefaulu A-level kwanini anataka aende Diploma? Ukifaulu A-level unaingia Degree moja kwa moja.
 
Kajitahidi though sijajua alikua kombi gan. But kutokana na competition maybe ndo kakosa kuchaguliwa hiyo course

au pia hakujaza vyuo vyote alijaza vile maarufu tu anavovijua

Kwa degree LLB inatolewa na UDSM,Mzumbe,Tumaini,SAUT,MoCu, i think na iringa university.. hizo option zote alkua nazo

Kwa diploma anaweza kwenda IJA-lushoto, Mzumbe, au Tumaini
 
kwa nini anataka kuanzaia diploma kama amefaulu? Sheria wengi wanachukuliwa wenye C ya English form four na angalau division two advance.... Kama ana hizo sifa kuepusha kupoteza muda aanzie tu degree maana degree ya sheria n ndefu kidogo kwa baadhi ya vyuo mfano UDSM, UDOM, RUCU na SAUT n miaka minne

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umesikia pre - form one , diploma ni pre - degree

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga wewe. Pre-form one haimo kwenye National Qualification Framework (NQF). Ni kama kusoma tuition tu. Ya kuwasiaidia wale wazito kuelewa. Ndo maana ni kitu cha muda mfupi.

Diploma ni ngazi mojawapo ya NQF, na inachukua miaka miwili. Kama anapenda kupoteza huo muda sawa ni hiari yake. Lakini ana uwezo wa kwenda moja kwa moja LLB.
 
Mkuu Alijaribu Kuweka Uelewa Kdg
 
Moja Kati Ya Fani Bora Yenye Option Ya Kujiajiri Au Kuajiriwa, Ila Ni Kitu Ambacho Muda Mwingine Ni Kipaji Binafsi Kutoka Moyoni,
 
Kwanza kabisa mpe hongera kwa kuchagua moja ya fani chache ambazo utakachosoma ni kweli utakitumia katika maisha na kazi zako. Maana Tanzania kuna fani nyingi sana ambazo vitu unavyosomea chuoni wala hutavitumia kwenye kazi wala maisha yako.

Baada ya hilo nikuulize swali - kama amefaulu A-level kwanini anataka aende Diploma? Ukifaulu A-level unaingia Degree moja kwa moja.
Mkuu, Aliomba Udsm na mzumbe wakamtema... anadai anadhani ili mzuri zaidi aende IJA Tanga then atokee huko kwenda Degree

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Aliomba Udsm na mzumbe wakamtema... anadai anadhani ili mzuri zaidi aende IJA Tanga then atokee huko kwenda Degree

Sent using Jamii Forums mobile app

Vyuo vingine mbona vipo. Angeenda Tumaini. Uzuri wa siku hizi kokote unakotokea lazima upitie Law School ndo uwe wakili. Ila zamani ndo watu walikuwa wanahangaika kuona umesomea wapi.
 
Back
Top Bottom