Kusoma Kiingereza muda mrefu bila kukimudu sawa sawa tatizo ni nini?

Tatizo ni mfumo wa elimu na jamii inayotuzunguka.mfano Tanzania unafundishwa kiingereza na mwalimu ambaye hakijui vizuri na anakufundisha Kwa kiswahili halafu ukifika nyumbani unapiga kilugha na kiswahili mwanzo mwisho.Hapo lazima ze ze ze ziwe nyingi.
 
Mwalimu anayekufundisha sio fluent. Wewe mwenyewe ukitoka mazingira ya shule unakiweka kapuni. Ukiangalia movie basi mpaka iwe imetafasiriwa. Husomi (hasa novel). Nyimbo unazosikiliza sio za kiingereza hata ukisikiliza basi ni kwa ajili ya Melody na beat. Kinachoimbwa huzingatii. Mwisho kabisa, umeridhika.
 
Kitu chochote ukijifunza bila kupractice huwezi kukimudu. Ndio kingereza kinafundishwa ila kinaachwa darasani , wanafunzi wakiwa hata nje ya darasa hawakitumii.
Nafuu Iko kwa wale wa English Medium... Hao angalau Wana practice.....
 
1. Tatizo kinafundishwa kwa kiswahili.
2. Wengi wetu tunawaza kwa kiswahili na kuzungumza/andika kiingereza.
3. Kuna "common mistakes" za kutamka maneno, muundo wa sentensi kama hii "Juma he is at home", "Did you went to school yesterday" hazifanyiwi kazi na walimu wetu.
 
Kitu chochote ukijifunza bila kupractice huwezi kukimudu. Ndio kingereza kinafundishwa ila kinaachwa darasani , wanafunzu wakiwa hata nje ya darasa hawakitumii.
Nafuu Iko kwa wale wa English Medium... Hao angalau Wana practice.....
Mfano mzuri wazungu wakija Tanzania ukiwaongelesha kwa kimombo wao wanajibu kwa kiswahili ili wajifunze kiswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…