Kusoma Masters Open University of Tanzania

Guys kwa anayehitaji msaada juu ya kusoma Open. Please weka tatizo hapa tutakusaidia tuliotangulia, uzoefu upo wa kutosha.

NB: Sihitaji inbox messages. Karibuni.
mimi nmechaguliwa open university bachelor degree chemistry with zoology (Bsc chemistry n zoology (minor)l.
Tatzo langu nimeshachagua courses na kuzilipia lakini hadi sasa moodle haifanyi kazi nimeshaenda DRC anadai niendelee kusubir wiki ya pili hii sina hata notice na masomo yangu ndo hayo daah.
 
Pole sana!
Mara nyingi kipindi hiki waalimu wengi bado wanaandaa ratiba za masomo pamoja na mpangilio wa mafunzo!
Hali itakuwa vizuri baada ya graduation tarehe 28/11/2019.

Hata ivyo, kwa kesi yako, DRC anaweza akawa anasubiri muongozo toka makao makuu. Cha kufanya wasiliana na IT wa makao makuu ili aweze ku activate account yako!!

Namba za IT unaweza fuatilia hapo hapo kwa DRC au ukamuomba drc akuunge katika group lolote ili uweze kubadilishana mawazo na wenzio wenye kesi kama yako.
Nimeshindwa kuweka namba yake hapa kwakuwa sio uungwana kuweka namba ya mtu bila idhini yake!!

DRC akishindwa piga, customer care out, huwa wanapokea simu na kusikiliza matatizo ya wateja wao( wanafunzi).
Usihofu, utasajiliwa!

Ahsante na Karibu.
 
Pole kwa changamoto iliyokupata. Je, umeweza kutengeneza Nywila (password) ya Moodle? Kama huna nywila ya Moodle hutaweza kuingia kwenye Moodle.
 
Pole kwa changamoto iliyokupata. Je, umeweza kutengeneza Nywila (password) ya Moodle? Kama huna nywila ya Moodle hutaweza kuingia kwenye Moodle.
Nywila inatengenezwa baada ya kuwa registered kwenye account ya moodle.
Nasisitiza wengi mlio wagen jiungen katika ma group ya WhatsApp, ya wanafunzi wa OUT, mtasaidiwa haraka, kwakuwa kule kuna baadhi pia walikuwa na matatizo kama hayo, wakapata miongozo toka kwa wenzao
 
Nywila ya Moodle hutengenezwa kwenye account ya SARIS (ambayo pia ndio account yako ya Moodle). Ni hii inawezekana tu pindi unapolipa angalau nusu ya malipo unayotakiwa kulipa. Kwenye SARIS account yako utatakiwa kuingiza PI code ya invoice yako. Then unatengeneza password hapo.
 
Guys kwa anayehitaji msaada juu ya kusoma Open. Please weka tatizo hapa tutakusaidia tuliotangulia, uzoefu upo wa kutosha.

NB: Sihitaji inbox messages. Karibuni.
Bado kuna uwezekanao wa kutuma maombi ya kusoma masters kwa mwezi disemba?ada zao ni shilingi ngapi?
 
Bado kuna uwezekanao wa kutuma maombi ya kusoma masters kwa mwezi disemba?ada zao ni shilingi ngapi?
Nenda kituo chako cha mkoa umuone Regional coordinator atakupa taarifa sahihi za usajili.
 
Ahsa
Ahsante nilifanikiwa kuingia moodle tatzo lilikuwa DRC hajapload malipo yangu
 
Tatzo ni kuzipata hzo groups mkuu
 
Tatzo ni kuzipata hzo groups mkuu
Coordinator anaweza kukusaidia, maana huwa wana groups za wanafunzi zinazowasaidia kutoa taarifa mbali mbali zinazohusu wanafunzi.
Usichoke wala kukata tamaa!!
 
Guys kwa anayehitaji msaada juu ya kusoma Open. Please weka tatizo hapa tutakusaidia tuliotangulia, uzoefu upo wa kutosha.

NB: Sihitaji inbox messages. Karibuni.
Naomba kujua kwa mfano nimechaguliwa kusoma MASTERS . alafu nimesoma unit chache na nikazilipia. Je nitarihusiwa kuendelea kusoma unit nyingine mpaka nagraduate bila kumalizia ada ya unit zinazobaki. Alafu wakabaki na cheti hadi nimalizie ada yao??? Au utaratibu ukoje?

Asante
 
Mkuu, ni vigumu kuendelea na unit nyingine bila kulipia! Na hivyo hutakuwa na access ya moodle ambapo assignment na discussion mbalimbali hifanyika! Kwa hiyo hutafanya assignment wala mijadala mbali mbali inayohusu course husika.

Kumbuka discussion na assignment vina marks katika matokeo yabmwisho.

Labda uombe msaada wa kuendelea na masomo kwa msaada wa coordinator wako na uongozi wa OUT kwa ujumla!
 
Habari!
kwa kutumia uzoefu wako na maelezo yako natumai utanipa majibu sahihi. Mimi nilifanya online application wiki mbili nyuma na leo nimetumiwa Email ya majibu na majibu yenyewe ni kama ifutavyo.

"This is to inform you that you have been admitted into Masters in .............. at the Open University of Tanzania (OUT), Once names are posted to OUT website kindly visit any nearby OUT centre for more information on orientation"

Hivyo kwa maelezo hayo nikusubiri mpaka pale majina yatakapotolewa kwenye tovuti ya chuo ndiyo natakiwa kulipoti kwenye kituo chochote cha Open University Tanzania kilichopo karibu na mimi.
 
Unaweza kufika kuanzia hapo ulipotumiwa huo ujumbe mkuu, kituo chochote cha OUT kilicho karibu nawe, njoo Pm mkuu nikupe namba za wahusika wa hili
 
Hiyo ni notification juu ya status ya maombi yako. wanakutaalifu kuwa tayari umekuwa admitted.

Hivyo, orodha ya majina yakiwekwa kwenye website yao, utapaswa kutembelea kituo chochote cha OUT kilichopo karibu na wewe ili upate taarifa zaidi juu ya usajili wako pamoja na orientation.

Pia nakushauri, utembelee OUT centr iliyoko karibu yako upate muongozo zaidi juu ya Email uliyo tumiwa.

Asante.
 
Unaweza kufika kuanzia hapo ulipotumiwa huo ujumbe mkuu, kituo chochote cha OUT kilicho karibu nawe, njoo Pm mkuu nikupe namba za wahusika wa hili
Wamenipa Numba kwenye Email yangu ila bado sijawapigia nilikuwa nasubiri majina yatoke kwenye website.
 
Hivyo kwa sasa nisubiri majina yawekwe kwenye Website ya chuo, baada ya hapo nireport kwenye kituo chochote cha OUT. Hivyo eveidence ya kuonyesha hapo kituoni ni majina yatakayowekwa kwenye website.
 
Hivyo kwa sasa nisubiri majina yawekwe kwenye Website ya chuo, baada ya hapo nireport kwenye kituo chochote cha OUT. Hivyo eveidence ya kuonyesha hapo kituoni ni majina yatakayowekwa kwenye website.
Nakushauri uende kituo chochote cha OUT kupata ushauri juu ya usajili wako
 
Guys kwa anayehitaji msaada juu ya kusoma Open. Please weka tatizo hapa tutakusaidia tuliotangulia, uzoefu upo wa kutosha.

NB: Sihitaji inbox messages. Karibuni.
Asant mkuuu nimetuma maombi ya kuomba bacharol chemistry B,biology C,Geography C kwa direct huku nikiwa na diploma tena yenye GPA nzuri na yenye kukizi vigezo ila vyeti hivi viko mbali nami nikaona naweza chelewa April intake je naweza pata kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…