Asante kwa kufuatilia mjadala.
Mimi ninasoma Masters, hivyo nadhani kuna utofauti wa katika ada pamoja na mambo mengine, lakini bado nina nafasi ya kukuelezea yale ninayo yafahamu.
1. Ada - Chuo Kikuu Huria tunalipa ada kwa Unit, ninaposema unit maana yake ni Structure/Composition/Uzito wa course husika, Uzito wa course ndio huonyesha unit za ulipaji, mfano kama course ina unit moja na ada yake unit ni tsh 180,000 maana yake ni kuwa somo lenye unit 2 ada yake itakuwa 180,000x2 = 360,000.
Hivyo huku tunalipa ada kwa course unazochukua kwa kipindi husika cha masomo, na kwa uzoefu wangu mara nyingi course za undergraduate huwa zina mchanganyiko wa unit kuna ambazo zina units 1 na ambazo zina units 2, na mara nyingi course zenye unit 2 zinakuwaga ngumu na hubeba dhamana kubwa katika matokeo yako. hivyo ni vyema unaposoma uwe mwangalifu wa course zenye unit 2.
2. Kuhusu muda wa kumaliza degree - Mkuu nadhani hili nashindwa kulijibia kwakuwa mimi ninasoma Masters, lakini kwa ufahamu wangu ni kuwa kiwango cha chini kabisa kilichowekwa na mamlaka ya elimu tanzania kuhusu kupata degree ni miaka 3, hivyo sidhani kama kuna uwezekano wa kupata Degree chini ya miaka mitatu.
Nami pia nilikuwa ninadhani kama hii, ya kufanya Masters ndani ya mwaka mmoja, lakini imeshindikana sabab chuo kina sisitiza kila course lazima isomwe kwa miezi isiyopungua mitatu. so hata ufanyeje ni lazima uwe ndani ya kipindi kilichowekwa na chuo ili kukidhi ile dhana ya muda uliyowekwa kwa ajili ya Degree au Masters au Phd.
Lakini pia kumbuka huwezi kusoma tu kisha ugraduate, ndio mana kuna mitihani ambayo hupangwa kwa muda husika, hivyo sio speed yako ya usomaji itakufanya kuwa na nafasi ya komba mtihani muda wowote unapojiona uko tayari kwa ajili ya mtihani, waalimu wanahitaji kujipanga kisha kuandaa mitihani kwa muda/semista husika.
Pia hata kama umepata nafasi ya kumemaliza course work ndani ya miaka miwili, utalazimika kusubiri miaka miatatu ipite ndio ugraduate, maana yake utakaa pending mwaka mmoja kusubiri miaka mitatu itimie
3.Utaratibu wa Field - Kama nilivyosema,awali, mimi ninasoma masters, lakini bado ninatambua kuwa Chuo kina muhula kama ilivyo kwa vyuo vingine, hivyo utaratibu wa mafunzo kwa vitendo upo kama kawaida na wanafunzi huomba katika taasisi mbali mbali ili kufanya mazoezi kwa vitendo, hii pia inategemea na course unayosomea, kuna wengine hufanya mazoezi wakiwa mwaka wa kwanza, wengine mwaka wa pili na wengine hufanya mwaka wa tatu. na mazoezi haya ya vitendo unaweza fanya katika ofisi unayofanyia kazi au sehemu yoyote ambapo unaona itafaa kwa ajili ya kutimiza matakwa ya mazoezi ya vitendo na kupata recommendation toka kwa supervisor wako.
Mwisho. mfumo wanaotumia chuo kikuu huria ni mfumo unaotumika sana katika vyuo vingi vya nje, na jambo linalofurahisha zaidi ni aina ya delivery ya materials inayotumiwa na waalimu wa OUT, kwakweli ina motivate hata mtu kusoma kwa bidii, walimu wanasisitiza mwanafunzi kuelewa na sio kukariri, na ndio mana assignment pamoja na mazoezi mbalimbali huwekwa katika platform inayoitwa MOODLE
(Modular Object-Oriented Dynamic Learning Environment), yaani kwa namna yoyote mwalimu lazima atajua kama umecopy na kupaste sababu wana software ambazo zimeshakuwa attached to moodle ambazo zinadetect mambo hayo.