Wanazuoni na mimi nahitaji msaada wetu. Nina BAED (Shahada ya Ualimu) nimeomba Open Degree ya Law.
Kuna kosa nimelifanya kwenye system wakati wa kuomba. Nimeomba kwa Direct entry nimejaza kila kitu nikatuma, nkagundua kuna kitu nimekosea nikaedit nikatuma tena.
Mara nikasoma maelekezo tena nikaona wanasema lazima uwe na 4.0 cut points. Mimi nina 3.5, kuna jamaa akaniambia niapply kama Equivalent nikafanya hivyo nikatuma tena sasa hii inakuwa mara ya tatu.
Wasiwasi wangu je nitachaguliwa kweli, maana nimetuma mara 3 na ni moja tu ambayo inaonyesha vigezo hii ya Equivalent pekee. Na je ukikosa unatakiwa kufanya nini? Naombeni neno lenu ndugu zangu.