Kusoma nje ya Nchi, Is it worth it?

Kusoma nje ya Nchi, Is it worth it?

Mkuu,

Tumeona kuwa hata hao wanaoitwa failures, wengine si failures kweli, ni mifumo tu inawafelisha.

Kuanzia ukosefu wa vifaa, walimu, nafasi, mpaka usahihishaji.

Kuna watu wamefeli kwa sababu hakukuwa na nafasi, si kwamba wamefeli kweli.

Tumeona kuna yule binti wa Kiislamu alifelishwa na baraza la mitihani, akakata rufaa, akapewa matokeo tofauti kabisa.

Sasa kuna watu wangapi wamekubali matokeo si hao na hata hawakukata rufaa?

Kuna binti wa kiongozi mkubwa alifeli sekondari, akasomeshwa private akaendelea mpaka Ph.D, akaja kuwa mtaalamu wa kutegemewa katika vyombo vya afya vya nchini mpaka United Nations!
Mm ninae ndugu wa kuitwa nelson Huyu ni mfano halisi wa anacho zungumza Kiranga .
 
Kuanzia mazingira ya vyuo tu,Internet ipo fasta,Library materials za kutosha,wanafunzi wa mataifa tofautitofauti na totozi,kwa wale wenyeji mikopo mizuri ya kulia bata siku ya freshers.
 
Elimu za mbele Zipo good ila za bongo ni mbovu maana zinafundishwa na walimu waliofeli
Kuna vitu vinashangaza sanaa.....katika hii nchi kungekua na tuzo au sanamu za WALIMU BORA...
ukoo wetu ungechongewa sanamu.....

Mm nili achanaga na izo mambo...

Mwalimu sio G.P.A ni content.....
 
Nitatoa mfano wa Marekani, kwa sababu ndipo niliposomea.

Nilipokuwa nasoma undergraduate, kulikuwa na somo moja elective la Philosophy. Halikuwa la lazima kwa course yangu. Nililichagua kwa sababu napenda Philosophy.

Sasa basi, kuanzia siku ya kwanza, kabla ya kujuana sana na Profesa, sikungojea sana kuanza ubishi wa kifalsafa.

Badala ya kubishia mada ya darasani, nikaanza kulibishia somo lenyewe, kwamba somo limeitwa Philosophy, lakini katika materials tunazungumzia Western Philosophy tu. Yani hakuna hata topic moja kuzungumzia falsafa za Asia au Africa, ilikuwa Wagiriki na kwenda mbele kwenye Western Philosophy.

Profesa akajitetea kwamba hivyo ndivyo somo lilivyo, na hata akitaka kufundisha nje ya hapo, hana ujuzi nako.

Profesa wa somo alikuwa mtu tofauti sana na mimi, alikuwa mzungu, mimi muafrika, alikuwa conservative, mimi nilikuwa liberal, alikuwa mzee, mimi nilikuwa kijana, alikuwa a relatively wealthy published judge, mimi nilikuwa mwanafunzi kutoka Afrika.

Basi kutoka hapo, kila siku darasani ubishi kwenda mbele. Yani huyu Kiranga unayemuona hapa ana afadhali, darasani ilikuwa Kiranga++. Mpaka siku nyingine nikaona nina dominate sana darasa. Nabishana na Profesa, namtajia vitabu, falsafa, nazama ndani sana.

Kuna dada mmoja mpaka akaniuliza, hivi, ule ubishi unaofanya darasani, ni kweli unaamini vile au unafanya figisu za kuchangamsha darasa tu? Nikamwambia naamini kweli.

Basi, siku ya mtihani wa mwisho ikasogelea, nikawa najiandaa kwa mtihani.

Nilikuwa maktaba ya chuo nasoma, nikaona email imeingia kutoka kwa huyu Profesa. Ananiambia usije kwenye mtihani wa mwisho.

Nikasema loooh salaaaleh, hapa ndipo napata ujira wa ubishi wangu wa kila siku darasani. Profesa ananifelisha kabla sijaingia kwenye chumba cha mtihani.

Nikamuuliza Profesa, vipi? Kwa nini nisije?

Akasema ushapasi mtihani kwa coursework yako.

Nikasema sasa nimepasi kwa alama gani?

Akaniambia A+, zile nindo ulizokuwa unatoa darasani si nondo za degree ya kwanza (undergraduate). Zile ni nondo za degree ya pili.

Jambo hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu uhuru uliopo katika mfumo wa elimu wa Marekani.

Nikajiuliza sana, kama ningekuwa katika vyuo vyetu vya nyumbani, je, ningeweza kudiriki kubishana na Profesa vile? Je, Profesa angeniachia nibishane naye vile? Je, angeweza kunipongeza kwa ubishi wangu kwa kuwa umebeba mantiki? Je, angeweza kunipa A+ na kuniambia nisije katika mtihani wa mwisho?

Profesa yule alikuja kutaka kuwa rafiki yangu sana, alitaka niende kuwa msemaji katika mikutano yao na kujenga network zaidi.

Kuna faida nyingi za kusoma nje, kuona dunia, kujenga network (kuna mdogo wangu alipata kazi Dar, kwa kampuni ya Wa South Africa, kwa kuwa tu waliona amehitimu University of Cape Town, chuo ambacho wao wanaamini ni "Harvard of Africa".

Ila pia, kusoma nje ni gharama kubwa, kama suala la gharama linakuwa mzigo mkubwa, mtu anaweza kuanza kusoma nyumbani, halafu akajiendeleza kusoma nje hata mitandaoni tu, siku hizi teknolojia inaruhusu.
The experience I gained from going to a 4-year liberal arts college in the US, was/is invaluable.

I think I’m a better person because of it.

I have better interpersonal skills because of it .

I’m less judgmental. More open minded. No longer closed minded

I’m very understanding and accepting of others’ points of views. And so much more.

These experiences were mostly gained outside the classroom.

For those seeking to study overseas, especially in the US for their undergrad, I recommend they go to a liberal arts college that puts an emphasis on diversity and one that has a decent sized international students’ student body.

For the first two years, the school I went to did not allow international students to reside off-campus.

So for my freshman year, first semester , I was assigned a Norwegian roommate.

Then during summer school, I was paired with a Haitian dude from South Florida.

Sophomore year, I had an Ethiopian. In my Junior and Senior years, I opted to reside off- campus.

Hiyo experience ya kuishi na hao roommates pamoja na kushiri katika extracurricular activities, vilinijenga sana. Ni experience ambayo mpaka leo bado naitumia.

Experience kama hiyo sidhani kama mtu anaweza kuipata endapo atasoma vyuo vya ndani tu.

UDSM haina international students body iliyo kubwa na iliyo diverse.

Nakumbuka during orientation ambapo kila mtu alijitambulisha na kutaja anapotoka, mabara yote ya dunia yaliwakilishwa.

Kabla ya hapo sikuwahi kukutana na mtu yoyote kutoka Armenia, Peru, Afghanistan, Cyprus, wala Panama.

But through college, I got to meet and go to school with people from all of those places and more.

Interaction na watu walio tofauti na wewe na wanaotokea pande zingine za dunia nayo ni elimu nzuri sana.
 
Kusoma Nje ya Nchi: Is It Worth it?

If you have traveled out to obtain another degree, could you please share your experience around the points below:

- What major difference did you notice in the education system that you think should be implemented in the Tanzanian education sector?

- Je? utawahimiza wanafunzi kuchukua mkopo kwa ajili ya kusoma nje ya nchi?

- Kusoma nje ya nchi kuliku badilishaje kama mtu? na una hisi ilikuwa na athari gani ya moja kwa moja kwenye maendeleo yako binafsi ya ki kazi na ki maisha.

Let's hear from you...
Tumia lugha moja tafadhali
 
Ni wazi elimu ya nje ni bora sana , hebu angalia elimu ya Tanzania haimjengi mtu kuwa mbunifu au kufikiri nje ya kilichokuwepo .

Mwalimu hajengi urafiki na mwanafunzi bali kutengeneza hofu na kuogopwa , mwalimu anaweza kufaulisha wanafunzi vilaza kwa rushwa ya ngono au kufelisha wanafu zi asiowapenda.

Nimeongea kwa uzoefu maana nimesoma katika mifumo yote miwili na wa nje kwangu ni bora zaidi hata ukanivutia kuendelea kuendesha maisha .
 
Kusoma Nje ya Nchi: Is It Worth it?

If you have traveled out to obtain another degree, could you please share your experience around the points below:

- What major difference did you notice in the education system that you think should be implemented in the Tanzanian education sector?

- Je? utawahimiza wanafunzi kuchukua mkopo kwa ajili ya kusoma nje ya nchi?

- Kusoma nje ya nchi kuliku badilishaje kama mtu? na una hisi ilikuwa na athari gani ya moja kwa moja kwenye maendeleo yako binafsi ya ki kazi na ki maisha.

Let's hear from you...
Ntasoma comments, exposure is always good
 
The experience I gained from going to a 4-year liberal arts college in the US, was/is invaluable.

I think I’m a better person because of it.

I have better interpersonal skills because of it .

I’m less judgmental. More open minded. No longer closed minded

I’m very understanding and accepting of others’ points of views. And so much more.

These experiences were mostly gained outside the classroom.

For those seeking to study overseas, especially in the US for their undergrad, I recommend they go to a liberal arts college that puts an emphasis on diversity and one that has a decent sized international students’ student body.

For the first two years, the school I went to did not allow international students to reside off-campus.

So for my freshman year, first semester , I was assigned a Norwegian roommate.

Then during summer school, I was paired with a Haitian dude from South Florida.

Sophomore year, I had an Ethiopian. In my Junior and Senior years, I opted to reside off- campus.

Hiyo experience ya kuishi na hao roommates pamoja na kushiri katika extracurricular activities, vilinijenga sana. Ni experience ambayo mpaka leo bado naitumia.

Experience kama hiyo sidhani kama mtu anaweza kuipata endapo atasoma vyuo vya ndani tu.

UDSM haina international students body iliyo kubwa na iliyo diverse.

Nakumbuka during orientation ambapo kila mtu alijitambulisha na kutaja anapotoka, mabara yote ya dunia yaliwakilishwa.

Kabla ya hapo sikuwahi kukutana na mtu yoyote kutoka Armenia, Peru, Afghanistan, Cyprus, wala Panama.

But through college, I got to meet and go to school with people from all of those places and more.

Interaction na watu walio tofauti na wewe na wanaotokea pande zingine za dunia nayo ni elimu nzuri sana.
Universalization and internationalization through education, grateful for the opportunity I had, I can't complain, imagine the entire class full of representation from diverse cultures, Bosnia, Slovenia, Montenegro, Serbia, India, Colombia, China, Mongolia, Uzbekistan, Tanzania, Italy, Germany, France, Ukraine, Russia, Croatia, Austria, UK, Hungary, Romania, Golden chance I loved it.
 
The experience I gained from going to a 4-year liberal arts college in the US, was/is invaluable.

I think I’m a better person because of it.

I have better interpersonal skills because of it .

I’m less judgmental. More open minded. No longer closed minded

I’m very understanding and accepting of others’ points of views. And so much more.

These experiences were mostly gained outside the classroom.

For those seeking to study overseas, especially in the US for their undergrad, I recommend they go to a liberal arts college that puts an emphasis on diversity and one that has a decent sized international students’ student body.

For the first two years, the school I went to did not allow international students to reside off-campus.

So for my freshman year, first semester , I was assigned a Norwegian roommate.

Then during summer school, I was paired with a Haitian dude from South Florida.

Sophomore year, I had an Ethiopian. In my Junior and Senior years, I opted to reside off- campus.

Hiyo experience ya kuishi na hao roommates pamoja na kushiri katika extracurricular activities, vilinijenga sana. Ni experience ambayo mpaka leo bado naitumia.

Experience kama hiyo sidhani kama mtu anaweza kuipata endapo atasoma vyuo vya ndani tu.

UDSM haina international students body iliyo kubwa na iliyo diverse.

Nakumbuka during orientation ambapo kila mtu alijitambulisha na kutaja anapotoka, mabara yote ya dunia yaliwakilishwa.

Kabla ya hapo sikuwahi kukutana na mtu yoyote kutoka Armenia, Peru, Afghanistan, Cyprus, wala Panama.

But through college, I got to meet and go to school with people from all of those places and more.

Interaction na watu walio tofauti na wewe na wanaotokea pande zingine za dunia nayo ni elimu nzuri sana.
Umeandika vizuri kwa wengi kuelewa kirahisi safi sana Mkuu kwa maandishi haya naona kweli una vitu tofauti vijana wanatakiwa wapate kutoka Exposure uliyoipata..
 
Ndiyo.

Kuna faida nyingi sana. Exposure. Kuiona dunia ilivyo na jinsi wenzetu walikofikia. Pia unaona elimu ya wenzetu ilivyo mpaka unatambua kuwa hawajaendelea kwa kubahatisha bali wamewekeza sana kwenye elimu. Na ualimu ni taaluma inayoheshimika sana kiasi kwamba siku Mpwayungu Village akienda kule itabidi atubu na kuwaomba msamaha walimu wote.

Ni vizuri zaidi ukipata full scholarship wewe kazi yako inabaki kupiga kitabu tu na ukiamua kufanya kazi basi iwe ni kwa hiari yako kwa ajili ya kupata vijisenti vya ziada.

Kama una mpango wa kurudi home baada ya masomo pengine siyo wazo zuri kuchukua mkopo maana hata ukirudi na degree yako nzuri nobody cares huku nyumbani labda ubahatishe kwenye international NGOs/organizations ambako malipo kidogo ni nafuu. Vinginevyo itakubidi uwe na connection nzuri bila ya hapo utakutana na vizee vya vitengo huko vimekakawana vitakufanyia figisu na hata kukurestisha ini pisi ukizubaa.

Na ukiwa mtundu unaweza kuja na wazo zuri la kujiajiri japo itakulazimu ujiandae kwa vipingamizi na ukiritimba utakaokutana nao. Ni vyema ukienda kusoma mambo ya afya, kompyuta, uhandisi, uchumi, sheria na mambo yanayohusiana na finances.

Oooh...na mademu wa kizungu unawachakaza unavyotaka na kulipiza kisasi japo kidogo kwa waliyofanyiwa mababu zetu akina Kijenketile Ngwale, Mkwawa na Mangungo...[emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099]

Elimu, elimu, elimu....hakuna siri nyingine ya maendeleo ya kweli!

View attachment 2471248
Mkwe kumbe huwa mnawapilizia mabeberu😀
 
Hii full scholarship inapatikanaje
 
The experience I gained from going to a 4-year liberal arts college in the US, was/is invaluable.

I think I’m a better person because of it.

I have better interpersonal skills because of it .

I’m less judgmental. More open minded. No longer closed minded

I’m very understanding and accepting of others’ points of views. And so much more.

These experiences were mostly gained outside the classroom.

For those seeking to study overseas, especially in the US for their undergrad, I recommend they go to a liberal arts college that puts an emphasis on diversity and one that has a decent sized international students’ student body.

For the first two years, the school I went to did not allow international students to reside off-campus.

So for my freshman year, first semester , I was assigned a Norwegian roommate.

Then during summer school, I was paired with a Haitian dude from South Florida.

Sophomore year, I had an Ethiopian. In my Junior and Senior years, I opted to reside off- campus.

Hiyo experience ya kuishi na hao roommates pamoja na kushiri katika extracurricular activities, vilinijenga sana. Ni experience ambayo mpaka leo bado naitumia.

Experience kama hiyo sidhani kama mtu anaweza kuipata endapo atasoma vyuo vya ndani tu.

UDSM haina international students body iliyo kubwa na iliyo diverse.

Nakumbuka during orientation ambapo kila mtu alijitambulisha na kutaja anapotoka, mabara yote ya dunia yaliwakilishwa.

Kabla ya hapo sikuwahi kukutana na mtu yoyote kutoka Armenia, Peru, Afghanistan, Cyprus, wala Panama.

But through college, I got to meet and go to school with people from all of those places and more.

Interaction na watu walio tofauti na wewe na wanaotokea pande zingine za dunia nayo ni elimu nzuri sana.
Hongera sana Buda
 
Tupeni madini tuone njia ya kuongeza ujuzi na si ili mradi kupoteza muda na Elimu za bongo, Hapo kwenye full scholarship tupeni connection wazee.
 
Kupata elimu ya nje kuna manufaa yake. Ukifanikiwa kupata scholarship hutaingia gharama yoyote, pia ukipata kazi huko ughaibuni usiiache...ukija huku bongo unaweza kuishia kupata frustrations kama hauna connection za kutosha. Scholarship zipo nyingi hasa kama unataka kuchukua Master's na kuendelea mfano Uingereza kuna Chevening, Common Wealth Scholarships, Sweden kuna scholarship za SIDA, Denmark pia wanatoa scholarship chini ya DANIDA, USA kuna Fullbright Scholarship etc. Elimu utakayoipata itakupa confidence katika eneo unalosomea, utafanya tafiti zinazoakisi mahitaji ya jamii/soko.

Utakutana na watu wa mataifa tofauti watakao kufungua macho na akili kuhusu dunia ilivyo, kujifunza tamaduni zao, changamoto etc. ni kitu kinachobadilisha mtazamo wako kuhusu dunia. Japo inabidi pia ujifunze kuvumilia utofauti wa baadhi ya mambo utakayokutana nayo, kwa nchi za Ulaya ni kawaida kukutana na wapenzi wenye jinsia moja wakionyeshana mahaba ama mara chache unaweza kukutana na watu ambao watakuletea ubaguzi kutokana na rangi yako ya ngozi. Mwisho wa yote uende kusoma ukiwa na malengo na mipango inayoeleweka ndio utapata manufaa zaidi !
 
Hii full scholarship inapatikanaje
Mi niliangukiwa na zali tu yaani mtu aliyekuwepo huko akaniunganisha na shirika fulani (lilishakufa) nikapata full ya miaka mitano na option ya kuongeza mmoja. Full kwa maana ya full mpaka nyumba, chakula na monthly stipend unalipiwa...

International students nadhani walikuwa wanalipa kama $39K kwa mwaka. Na hapo bado mambo mengine. Mtoto wa mkulima wa dengu kutoka Misungwi mi ningeweza wapi?

Kwa scholarships za US Google EBM Scholars utapata mwanga kidogo
 
Back
Top Bottom