Mkuu kasigazi, hii kesi ya waalimu bado ni ngoma nzito sana kuicheza! yani ni sawa mziki upigwe Rnb, Bongo flavour, Hip Hop, charanga na Reggae kwa pamoja halafu unaambiwa uicheze hiyo miziki at a time!!!
Waalimu wa arts wametosha?? Kivipi?? Mijini ama wapi? Mbona kwetu huku mikoani tuna waalimu wawili tu wa sanaa wanahudumia watoto zaidi ya 400?? Huko ndiko kutosha kunakosemwa na serikali ya Jamhuri ama vipi?
Aliyefanya Research na kusema waalimu wametosha ni nani?? Hiyo research aliifanyia eneo sahihi kweli ama vipi??
Mi ningeishauri serikali kwamba, waalimu wote watakaajiriwa waambiwe mapema kwamba, ninyi mnapelekwa vijijini mwakani, no matter what! Hapo atakayekubali, atasoma! Atakayegoma, atajitafutia ajira yake!!!
Achilia mbali suala la huduma za kijamii.
Kiufupi bado sana waalimu kutosha!!