Habari za Asubuhi wanajamii!
Jaji Augustino Ramadhani amelitumikia taifa kwa nafasi hiyo kwa miaka mitatu tu! Mabo ambayo najiuliza ni je, Kikwete alipomteua mwaka 2007 hakujua kwamba amebakiza miaka mitatu tu ya kustaafu kwake kwa mujibu wa sheria? na je kama alijua hakuona kwamba analiingizia Taifa Hasara kwa uteuzi huo kwa kuongeza idadi ya majaji wakuu wastaafu?
Lakini kutokana na kauli za Mwanasheria Mkuu wa serikali, mheshimiwa Jaji Werema, kwamba Tanzania haihitaji katiba mpya, ninapata wazo lingine kwamba huenda misimamo ya jaji Ramadhani ilikuwa tofauti na ya watawala wa serikali, kwani tayari Jaji Ramadhani keshasema katiba Mpya haikwepeki kwa sasa, huyu AG anasema 'haitakiwi' kwa sasa. Je anasoma alama za nyakati?
AG anasema wanaohitaji marekebisho (Viraka), wampelekee mapendekezo. Je, hivi yuko nchi ama dunia gani ambako ameshindwa hata kunong'onezwa kwamba movement iliyopo sasa Tz ni suala la katiba mpya na si marekebisho? na wanao dai hivyo ni wa Tanzania ambao ndiyo wenye katiba? Au anadhani nchi hii ni ya watawala kama ambavyo katiba iliyopo ilivyo?
Ndugu zangu watanzania, nadhani Tanzania sasa inahitaji uhuru wake halisi kutoka kwa serikali ya watawala, na hilo litawezekana kwa kuwa na katiba ya watanzania, Hivyo tunapaswa kuungana pamoja kudai katiba mpya na si marekebisho. Yanayotekea sasa na kauli za wapinga katiba mpya si mapya ni yale yale yaliyotumiwa na watawala wa kikoloni kwa waliokuwa wanadai uhuru enzi hizo.
Naomba kauli y a Jaji Mkuu Mstaafu Jaji Ramadhani inayoungana na Majaji wengine wastaafu na baadhi ya Viongozi kwamba Katiba mpya inahitaji iwe ndiyo kauli ya Jaji Mkuu mpya, Jaji Chande, vinginevyo hakuteuliwa kwa ajili ya watanzania.