Kustaafu hakuji ghafla bin vuuu .Cha ajabu wengi huona kuwa siku za kustaafu bado ziko mbali sana.Kwa msingi huo hawafanyi maandalizi ya kutosha na kwa muda mrefu.Maisha ya binadamu ni mafupi sana na katika kila hatua mtu unapaswa kuangalia umetoka wapi , unaenda wapi na kila hatua umefanikisha nini.Kuna msemo unasena hivi:
If u r not handsome by age 20, strong by age 30, rich by age 40, wise by age 50 then foget it!
Hii inamaanishe kuwa katika vipindi hivi basi ujiandae kukamilisha kitu.,Siyo unasubiri hadi ufikishe umri wa kustaafu ambao TZ ni miaka 60 halafu uanze kukimbia kimbia kuanza kutafuta kiwanja, kufikiria utajenga vipi n.k.Ni vizuri maandalizi ya kustaafu mtu ukayaanza toka mwanzo unapopata fursa ya kuwa na kipato.Weka akiba, jiunge na mifuko ya hifadhi ya jamii, kata bima, nunua hisa, nunua au wekeza kwenye mali zisizohamishika, somesha watoto wako na ikiwezekana zaa mapema ili utakapofika muda wa kustaafu uwe umemalizana nao kwenye masuala ya shule, ishi vizuri na watu wakati wote kwa kuepuka kuwa na majivuno na kiburi kwa vile una cheo au fedha maana kuna siku utawahitaji uliokuwa unawadharau.
WOS......Kwa kweli nimeizimia sana hiyo message yako hapo juu.....ubarikiwe sana, I can't imagine utakuwa na haiba gani Kny jamii na familia yako WOS!
Maisha ya mstaafu to me yanaanza kuandaliwa pale tu mtu anapopata ufahamu wa kutambua mema na mabaya....ambayo to me right ukiwa hata Primary school.....ukishajimbua wewe nani, maisha maana yake ni nini? Basi inatakiwa kuanza maandalizi ya ustaafu mapema kabisa....!
Naweza nisieleweke kusema kwamba mchakato huanzia ukiwa mdogo kabisa...lakini maana yangu kama ukishatambua maisha ni nini...basi ukiwa shule hata ya msingi, utajitahidi kusoma kwa bidii sana ili kwanza upata maarifa ya kutosha ktk maisha yako, pili ufaulu mitihani ili uendelea mbele....so bidii ya kujisoma inatakiwa iendelee mpaka uwezo wako utakapo ishia.....then utakuwa na asset yako kichwani ready for converting it into liquid money kwa kuajiriwa au kujiajiri!
Sasa utaona kama uliinvest vizuri kny elimu, ukafaulu vizuri...ukiingia uraiani utapata kuchagua kibarua ambacho kinakulipa zaidi...coz u have excellent results....lkn kama wewe results zako zina matege...utachaguliwa kibarua!
Also ukiwa huko huko shuleni, unaweza kubahatika ukawa na wazizi au rafiki, jamaa wanaokupa vijisenti in excess....kama unajua maisha, basi utasave hutotuhela kwa namna nyingi....kwa kununua hisa, kijiwanja etc ukiwa bado shule.....!
Then ukiwa umeanza kazi (kujitegemea).....please try to tangibilize as much as you can any single coin you get.....nothing with value that its value can't increase! nina maana hata kama una Tshs 5,000 mkononi unaweza kupata kitu chenye thamani hiyo....so nunua hicho kitu, kaa nacho kuliko kukaa na hela mkononi! Kuna hii tabia huwa inanikera sana ya watu kulalamika ooh kipato kidogo, kipato kidogo...just ask them maswali...with kipato hicho kidogo wamefanya nini? nothing.....wengine wanashindwa hata kununua vitu vya ndani kwao..kisa eti kipato kidogo...haohao ni mabingwa wa michango ya chicken party, harusi, ubatizo, kipaimara etc!
Mi binafsi nakumbuka baada ya kumaliza form6 in 2000, nilipata kakibarua kakufundisha...walikuwa wananilipa Tshs 48,000 a month! But with this salary, nilinunua kiwanja che ukubwa wa 25m kwa 90m pale NJ....kwa Tshs 80,000...leo hii the same kiwanja naweza kukuuza kwa more than 10m!
So badala ya kulamikia vipato vyetu, tujiulize hicho kidogo unachopata umefanyia nini? Kama umeweza kumanage vizuri hicho kidogo hopeful ukipata kikubwa kitakupeleka mbali!
So kwa kifupi, maisha ya mstaafu hayajengwi baada ya kustaafu bali ni mchakato mrefu sana...ambao to me unawezakuwa unahusisha maisha yako ya utotoni as well!
Lakini kama hukuweza kuanza kuwekeza mapema, basi it is never late......so start now kujiwekea akiba kwa njia mbalimbali...kama vile kununua ardhi (ardhi bado ni cheap sana Tanzania ndugu zangu), vipande, kudeposit cash,kuwa mkarimu na kuwajali watoto wanakua sasa....kwa sababu hujui watakuja kuwa kina nani baadaye kuliko kuwaheshimu wazee waliokuzidi umri!