Kustaafu kunaathiri vipi maisha ya mstaafu?

Limbukeni

Senior Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
117
Reaction score
1
Inawezekana mtu baada ya kustaafu akajihisi au akajitambua kwamba yeye hana tena thamani katika jamii. Hali hii itamsononesha sana. Alipokuwa akifanya kazi mambo yake yote yalikuwa akienda vizuri kwani kila mtu alikuwa akimsaidia shida zake kwa kuwa yeye pia atawasaidia shida zao. Sasa baada ya kustaafu misaada aliyokuwa akiipata ina kwama mara mojo. Kusononeka huku kunasababisha upweke na kunauwezekano wa kiwango cha uzee kuja kwa kasi. Je hii inaweza kuhusishwa kukatishwa kwa maisha ya wastaafu wetu kwa visa mchanganyiko kama hivyo. Je kuwe na utaratibu wa kuhakkisha wastaafu wetu hawakutwi na vitu kama hivyo? Tujadiliane wadau
 
limbukeni nadhani kama serikali tayari imekwisha weka sera zake na kuna taasisi zinaangalia maslahi ya wastaafu lakini ni muhimu sisi pia mmoja mmoja tukajiandaa na kukubali kuwa kujiajiri ndio suluhusho la kudumu...
 
Sasa hivi NIP pamoja na taasisi mbalimbali za mafunzo wanaendesha kozi fupi za maisha baada ya kusataafu ili kumfanya mstaafu ajiandae vizuri kisaikolojia na namna nyingine na utaratibu wa maisha tofauti na ule aliokuwa ameuzoea ili kusogeza mbele uhai wake. Lakini kama mstaafu atachukulia suala la kustaafu kama JANGA, basi walahi hachukui miaka miwili - KWISHA.

Hata hivyo, wewe mwajiriwa fanya kazi yako kwa bidii na uaminifu.
 
pia ikumbukwe kwamba kila mtu atakutwa na hili swala miaka inavuta pandezote.
 
limbukeni nadhani kama serikali tayari imekwisha weka sera zake na kuna taasisi zinaangalia maslahi ya wastaafu lakini ni muhimu sisi pia mmoja mmoja tukajiandaa na kukubali kuwa kujiajiri ndio suluhusho la kudumu...

hili swali nimeuliza kwa mtanzania wa kawaida kabisa, mdau umenijibu kama tuko bungeni ningependa zaidi kupata maoni yako binafsi kwani nyakati zijazo mambo mengi tutaweka kando ili tuwe na ufanisi wa haki ,wakudumu na kujivunia kwa vizazi vyote. asante
 
Last edited:
Kustaafu ni wajibu kwa kila atakaejaliwa kutoa huduma hadi wakati huo. Tatizo linalokuja ni vipi ulitumia muda wako ukiwa katika ajira na zaidi ya hapo ni mafao gani unaondoka nayo. Haya mashirika yanayotoa mafao mengi ni utata mtupu kwa mfano PPF, NSSF nk. Hawa wanatumia pesa za wafanyakazi kuanzisha miradi bila ya kuwajali waliochangia. Pesa wanayolipa haina riba kwa kuwa wameitumia katika miradi yao. Huu ni Wizi Mtupu!!!
 
Kusononeka kwa mstaafu kunaletwa na kutokujiandaa kimaisha,unajua mwingine mpaka muda wa kustaafu unafika unakuta hana nyumba yaani mambo yanakuwa shaghalambaghala,lakini kama mtu amejiandaa sidhani kama itamsumbua,na sababu nyingine ni kucheleweshewa mafao yake,hiyo nayo pia ni sababu kubwa inayosababisha wastaafu wengi kusononeka maana unakuta muda aliotegemea kupata mafao yake umepita na akiangalia haoni mwelekeo kwa hiyo hapo pia anapata sononeko la moyo na ghafla utaona mtu anaanza kuzeeka.

ushauri taasisi zinazoshughulika na mafao ya wastaafu waache kupenda rushwa,maana wastaafu wengi wakienda huko wanaishia kuzungushwa njoo kesho mara njoo baada ya wiki na usumbufu mwingi .
 
Kustaafu hakuji ghafla bin vuuu .Cha ajabu wengi huona kuwa siku za kustaafu bado ziko mbali sana.Kwa msingi huo hawafanyi maandalizi ya kutosha na kwa muda mrefu.Maisha ya binadamu ni mafupi sana na katika kila hatua mtu unapaswa kuangalia umetoka wapi , unaenda wapi na kila hatua umefanikisha nini.Kuna msemo unasena hivi:
If u r not handsome by age 20, strong by age 30, rich by age 40, wise by age 50 then foget it!
Hii inamaanishe kuwa katika vipindi hivi basi ujiandae kukamilisha kitu.,Siyo unasubiri hadi ufikishe umri wa kustaafu ambao TZ ni miaka 60 halafu uanze kukimbia kimbia kuanza kutafuta kiwanja, kufikiria utajenga vipi n.k.Ni vizuri maandalizi ya kustaafu mtu ukayaanza toka mwanzo unapopata fursa ya kuwa na kipato.Weka akiba, jiunge na mifuko ya hifadhi ya jamii, kata bima, nunua hisa, nunua au wekeza kwenye mali zisizohamishika, somesha watoto wako na ikiwezekana zaa mapema ili utakapofika muda wa kustaafu uwe umemalizana nao kwenye masuala ya shule, ishi vizuri na watu wakati wote kwa kuepuka kuwa na majivuno na kiburi kwa vile una cheo au fedha maana kuna siku utawahitaji uliokuwa unawadharau.
 
WOS......Kwa kweli nimeizimia sana hiyo message yako hapo juu.....ubarikiwe sana, I can't imagine utakuwa na haiba gani Kny jamii na familia yako WOS!

Maisha ya mstaafu to me yanaanza kuandaliwa pale tu mtu anapopata ufahamu wa kutambua mema na mabaya....ambayo to me right ukiwa hata Primary school.....ukishajimbua wewe nani, maisha maana yake ni nini? Basi inatakiwa kuanza maandalizi ya ustaafu mapema kabisa....!

Naweza nisieleweke kusema kwamba mchakato huanzia ukiwa mdogo kabisa...lakini maana yangu kama ukishatambua maisha ni nini...basi ukiwa shule hata ya msingi, utajitahidi kusoma kwa bidii sana ili kwanza upata maarifa ya kutosha ktk maisha yako, pili ufaulu mitihani ili uendelea mbele....so bidii ya kujisoma inatakiwa iendelee mpaka uwezo wako utakapo ishia.....then utakuwa na asset yako kichwani ready for converting it into liquid money kwa kuajiriwa au kujiajiri!

Sasa utaona kama uliinvest vizuri kny elimu, ukafaulu vizuri...ukiingia uraiani utapata kuchagua kibarua ambacho kinakulipa zaidi...coz u have excellent results....lkn kama wewe results zako zina matege...utachaguliwa kibarua!

Also ukiwa huko huko shuleni, unaweza kubahatika ukawa na wazizi au rafiki, jamaa wanaokupa vijisenti in excess....kama unajua maisha, basi utasave hutotuhela kwa namna nyingi....kwa kununua hisa, kijiwanja etc ukiwa bado shule.....!

Then ukiwa umeanza kazi (kujitegemea).....please try to tangibilize as much as you can any single coin you get.....nothing with value that its value can't increase! nina maana hata kama una Tshs 5,000 mkononi unaweza kupata kitu chenye thamani hiyo....so nunua hicho kitu, kaa nacho kuliko kukaa na hela mkononi! Kuna hii tabia huwa inanikera sana ya watu kulalamika ooh kipato kidogo, kipato kidogo...just ask them maswali...with kipato hicho kidogo wamefanya nini? nothing.....wengine wanashindwa hata kununua vitu vya ndani kwao..kisa eti kipato kidogo...haohao ni mabingwa wa michango ya chicken party, harusi, ubatizo, kipaimara etc!

Mi binafsi nakumbuka baada ya kumaliza form6 in 2000, nilipata kakibarua kakufundisha...walikuwa wananilipa Tshs 48,000 a month! But with this salary, nilinunua kiwanja che ukubwa wa 25m kwa 90m pale NJ....kwa Tshs 80,000...leo hii the same kiwanja naweza kukuuza kwa more than 10m!

So badala ya kulamikia vipato vyetu, tujiulize hicho kidogo unachopata umefanyia nini? Kama umeweza kumanage vizuri hicho kidogo hopeful ukipata kikubwa kitakupeleka mbali!

So kwa kifupi, maisha ya mstaafu hayajengwi baada ya kustaafu bali ni mchakato mrefu sana...ambao to me unawezakuwa unahusisha maisha yako ya utotoni as well!

Lakini kama hukuweza kuanza kuwekeza mapema, basi it is never late......so start now kujiwekea akiba kwa njia mbalimbali...kama vile kununua ardhi (ardhi bado ni cheap sana Tanzania ndugu zangu), vipande, kudeposit cash,kuwa mkarimu na kuwajali watoto wanakua sasa....kwa sababu hujui watakuja kuwa kina nani baadaye kuliko kuwaheshimu wazee waliokuzidi umri!
 
Mkuu,
nashukuru kuwa kama kawaida umedhihirisha ule msemo usemao kuwa:
'Give a dog a bad name and hang him.' Once we have labelled someone, our- and even their - expectations of their behaviour from then on seem to be almost wholly determined by that label!! HAPA umeishi kufuatana na jina lako kwa maana umechukua mtiririko wa mada hadi ngazi ngyingine - NEXT LEVEL.
Hiyo iliyoko kwenye bold imenigusa sana kwa maana ni ukweli - Watoto hawakawii na hawasahau.Ukimfanyia jema hata kama ni dogo vipi basi hukaa kichwani.Baya nalo halifutiki.Ukiwekeza wema wako kwa watoto huwezi kukosea.Mimi leo hii nakutana na watu kama waalimu wangu na wengineo na hufurahi kuwafanyia jambo jema kwa kukumbuka yale mazuri waliyonifanyia enzi hizooooo!
 
Mi nimeona kwa sasa wazee wengi wanajikita sana katika maswala ya mapenzi hawa walio staafu eti nakula Pension yeye anaangalia hana mtoto mdogo anaye msomesha watoto wake wote wamekuwa wakubwa na wana kazi zao sasa hiyo pension anakula na visichana ambavyo ni nyumba ndogo wengi tumewaona wanatumbua vitu mitaani na wababu.
 
Hiyo iliyoko kwenye bold imenigusa sana kwa maana ni ukweli - Watoto hawakawii na hawasahau.Ukimfanyia jema hata kama ni dogo vipi basi hukaa kichwani.Baya nalo halifutiki.Ukiwekeza wema wako kwa watoto huwezi kukosea!

WOS, Nimejifunza mengi sana mazuri na mabaya kutoka kwa elders wangu....so huwa sipendi kurudia makosa waliyofanya wao....pengine nafanya makosa mengine but si yale waliyofanya wao kabisa!

Niko na uncle (kakake na mama) who was the first graduate in Economics -UDMS from our village miaka ya 1980 hivi....mi nikiwa mdogo hata primary sijaanza! Lkn tulikuwa tunamsikia mambo yake akija home mara moja moja sana....but he was of no help kabisa materially & morally kwetu sisi wala familia yake though alikuwa na uwezo sana kifedha na kitaalum!

Maskini kumbe uwezo wake kifedha ulikuwa ni mshahara......na mshahara wote ulikuwa unaishia kupombelea na kufanya mambo ya sifa tu......! 1999 akasimamishwa kazi....mpaka leo hii, hana kibanda si kijijini wala huku mjini wala popote...alikuwa anaishi nyumba ya kampuni...katimuliwa na huko...so kajibanza kny nyumba aliyepewa mkewe kama mwalimu!

Huyu jamaa kule kijijini si vijana wala wazee wanaomtaka hata kwa bure.....aliwadisourage sana wazee huko bush wasiwapeleke watoto wao shule coz through him they couldn't realise the benefits of schooling!

Mi mwenyewe joining instructions za form5 zilipitia kwake....coz huko bush tulikuwa hatuna address so nikatumia ya kwake wakati najaza selforms kwani yeye alikuwa mjini.....cha kushangaza baada yakupata forms zile alikaa nazo miezi mitano hivi, kaenda kumpelekea dadake (mama) kule bush mwezi wa kumi na moja, wakati school ilishafuinguliwa mwezi wa saba!.....iliniuma sana mimi hii kitu!

So huwanatamani nimlipizie kisasi bt can't coz na mimi sijui nitaishia wapi pengine watoto wake watakuja kuniokota one day or watoto wangu wataokotwa one day etc. So better kundaa maisha ya ustaafu mapema iwezekanavyo na kila unapopata oppotunity ya kufanya hivyo......tukiweza kufanya hivyo bila shaka....tutakuwa tunatamaani kustaafu badala ya kuhifia kustaafu!
 
Nina wazo la kuingia katika biashara ya kusaidia wajasiriamali ikiwa ni pamoja na wastaafu " Jinsi ya kuendeleza wazo la kibiashara kuwa biashara inayolipa"

Nina lenga kuwafikia wenye mitaji midogo midogo na ambao wanataka kuanza kwa kiwango kidogo.

Je wadau, kuna mawazo yeyote kama watu wanahitaji huduma hii ya biashara?

Asanteni kwa mawazo yetu.
 
Mi nimeona kwa sasa wazee wengi wanajikita sana katika maswala ya mapenzi hawa walio staafu eti nakula Pension yeye anaangalia hana mtoto mdogo anaye msomesha watoto wake wote wamekuwa wakubwa na wana kazi zao sasa hiyo pension anakula na visichana ambavyo ni nyumba ndogo wengi tumewaona wanatumbua vitu mitaani na wababu.

F80

Hapo kny bold, umeona mwisho wao unavyokuwa mbaya lakini? mi na mifano mingi sana ya watu wa aina hiyo...!
 
hapa siyo sehemu ya mada hapa post ya matangazo ya kazi,hamjasoma nini? jalini post
 
Back
Top Bottom