SoC01 Kusuasua kwa miradi huchelewesha maendeleo ya jamii

SoC01 Kusuasua kwa miradi huchelewesha maendeleo ya jamii

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Serikali ina wajibu wa kulisimamia swala hili ambapo tunahitaji mradi ulioanzishwa katika eneo fulani utekelezwe katika muda uliopangwa.

Kwa mfano, tukiangazia katika miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, shule, barabara, na maeneo mbalimbali ya uchukuzi mfano bandari na viwanja vya ndege.

Sisi kama wananchi tunahitaji barabara zijengwe ili kazi izidi kusonga mbele ambapo tutaweza kusafirisha marighafi kwenda viwandani pia kusafirisha mizigo na abiria ili kujipatia riziki zetu za kila siku.

Sambamba na sekta za afya vivyo hivyo kwamba zahanati na hospitali zijengwe haraka kuondoa na kupunguza kero za matibabu.

Hivyo ni vitu miongoni katika miradi ambapo wakandarasi wanakua wanashindwa kusimamia vyema wajibu wao waliopewa badala yake wanajikita kwenye shughuli zingine zisizohusiana na wananchi

Hivyo serikali inalo jukumu kubwa katika kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inafanyika katika muda uliopangwa na siyo vinginevyo. Na kwa anayekaidi atolewe kwenye nafasi au kunyang'anywa kibarua hicho. Hii itasaidia katika ujenzi wa taifa katika kutekeleza mahitaji ya wananchi.

Asante
 
Upvote 0
Back
Top Bottom