Kusugua au kusigina meno wakati mtu yupo usingizini

Kusugua au kusigina meno wakati mtu yupo usingizini

Ni dalili za kulishwa chakula usiku akiwa amelala. Usishangae mtoto anapoamka asubuhi huwa ameshiba na hana hamu ya chakula.
 
Habari za leo wadau wa JF.? Nina mwanangu wa kiume miaka 2 na miezi 6,siku za karibuni ameanza tabia ya kutafuna MENO wakati akiwa USINGIZINI sielewi ni tatizo gani na TIBA yake nini..? Naomba msaada wenu kwa aliye na malelezo zaidi. Namba yangu 0752489529
 
Mkuu.@Emilias G Kusagika kwa meno (attrition)

Huku ni kulika kwa meno kwenye sehemu ambapo meno ya juu na chini hukutana (occlusal surfaces). Katika hali ya kawaida meno hulika sehemu hizi kutokana na kadri yanavyoendelea

kutumika kusaga vyakula. Hali hii huendelea polepole kadri mtu anavyoendelea kuishi (umri), kitaalamu inajulikana kama physiological attrition. Si rahisi kuhisi dalili zake kwani mwili

hujaribu kuziba vitundu vya mifereji midogo inayotoka kwenye kiini cha jino kwenda kwenye sehemu ngumu ya kati (dentine). Ni vitundu hivi ambavyo vikiwa wazi husababisha msisimko

(sensitivity). Kulika kwa meno sehemu ya kusaga huwa ugonjwa pale tu unapotokana na mambo mengine zaidi ya kule kwa kawaida kwa kuongeza umri.


Sababu za kusagika kwa meno (attrition)


Baadhi ya mambo yanayosabisha hali hii ni

Kusaga meno (bruxism):
- hii ni hali ambayo mtu husaga meno yake wakati hatafuni kitu

chochote na mara nyingi mtu huwa hajitambui kama ana tatizo hili. Hali hii mara nyingi

hujitokeza wakati wa usiku mtu akiwa amelala (nocturnal bruxism) japo kwa wachache

wanaweza saga mchana pia. Si rahisi mtu wa namna hii kujitambua mpaka pale

atakapoambiwa na mtu wanayelala pamoja au atakapo kwenda kwa mtaalamu wa meno na

kuelezwa.

Nini husababisha hali hii?

Yapo baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha tatizo hili ingawa zaidi linahusishwa na mabadiliko ya kisaikolojia. Watu wenye mawazo mengi wanaonekana kuwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili.

Tatizo hili pia linaweza kutokana na jino lililozibwa na kujazwa zaidi ya kawaida. Mwili hufanya harakati za kupungua sehemu iliyozidi kwa kuisaga na hatimaye kujikuta umejenga mazoea, kiasi kwamba hata jino likisha kuwa kiasi sawa bado mwili utaendelea kusaga tu.

Pia wale wanaokaa kwenye meza kwa muda mrefu wakisoma au vyovyote huku wameshikiria kidevu kwa nguvu, nao ni waathirika wa ugonjwa huu. Katika hali ya kawaida mtu ukiwa

umefunga mdomo umetulia meno ya juu na ya chini huwa hayakutani bali huacha nafasi kama milimita mbili hivi (resting space). Sasa ukiyabana pamoja kwa muda mrefu kwa kushikilia

kidevu, utayafanya yajenge mazoea ya kushikana hata pale ambapo hujashika kidevu na mwishowe kuanza kusagana

Dalili zake na viashiria vyake

Mgonjwa mwenyewe kuhisi msisimko wakati wa kunywa vitu vya baridi, maumivu kama kiwango cha uharibifu ni kikubwa kiasi cha kuacha kiini jino wazi (dental pulp exposure).

Ukiangalia meno utakuta yamelika sehemu ya kutafunia kwenye magego na visaidizi vyake (molars and premolars), sehemu za kukatia na kuchoma kwa meno ya mbele (canines and

incisors). Kusagika huanzia sehemu za meno zilizoinuka (cusps) ambazo hatimaye huondoka kabisa na kuwa bapa au flati. Meno huweza kusagika mpaka wakati mwingine kufikia kwenye

usawa wa fizi. Watu wenye tatizo hili huonekana kuwa na uso wa mraba kutokana na msuli

mkubwa wa kuvuta taya (masseter muscle) kunenepa kutokana na kutumika zaidi. Mgonjwa pia huweza kuchoka kirahisi misuli wakati wa kutafuna katika hali ya kawaida.

Tatizo linaweza kuathiri hata sehemu ya muunganiko wa taya la chini na fuvu

(temporomandibular joint - TMJ). Mgonjwa huweza kusikia maumivu kwenye kiungo (joint) hiki

na wakati mwingine kufyatuka fyatuka (TMJ dislocation) au kutoa sauti wakati wa kufungua na

kufunga kinywa (popping or cricking sound in TMJ).


Picha zikionehsa meno yaliyosagika

sagika.jpg



baa.jpg


picha ya juu-kinachoonekana kama kuvimba shavu ni msuli wa kuvuta taya (masseter muscle) ulioongezeka ukubwa

kutokana na kusaga meno. Picha ya chini mwezi mmoja baada ya kupata matibabu ya uhakika, msuli unarudi katika hali

ya kawaida.


Matibabu

Ni vizuri kujua chanzo cha tatizo hili na kukishughulikia kwanza kabla ya kufanya matibabu

zaidi ya meno kurekebisha uharibifu uliotaka na msagiko. Utafiti unaonesha wengi wenye

matatizo haya ni wenye mawazo yaliyozidi kiwango (stress). Lazima ujue kwanini mtu

anawaza sana ili ummpatie ushauri nasaha au hata kumpeleka kwa wataamu wa mambo ya

saikolojia ili waweze kumsaidia.

Wakati hayo yakiendelea inabidi kumfundisha mgonjwa kulegeza taya (relaxation exercise) na

kuachanisha meno kila anapohisi meno ya juu na ya chini yamekutana. Akifanya mazoezi haya

kwa muda mrefu mwili huweza kujenga mazoea kuwa kila meno yakikutana yaachanishwe

(conditioned reflex action). Mgonjwa akiacha kusaga basi matibabu ya kurekebisha madhara

yanaweza kufanyika kwa mafanikio makubwa, iwe kuziba, kuua mzizi wa jino na kuyavalisha

meno kofia ngumu hasa metal reinforced porcelain crown.

Kwa wale ambao ni vigumu kuacha tabia ya kusaga wanaweza kutengenezewa kifaa maalumu

cha kulinda meno wakati wa usiku (night guards), ambacho huvaliwa na mgonjwa usiku wakati

wa kulala kuzuia meno kugusana na baada ya muda atazoea pia na kuacha kusaga. Kifaa hiki

husaidia pia kuondoa matatizo yaliyokwisha jitokeza kwenye jointi.


kki.jpg


kifaa cha kukinga meno yasisagane (night guard) mgonjwa akiwa amevaa kifaa

Ni vizuri kumuuliza mwenzako kama amewahi kukusikia ukisaga meno usiku ili uweze kuchukua hatua za kuwaona

wataamu mapema. Kumbuka kujua tatizo mapema na kulitibu ni sehemu ya hatua za kinga.

Niishie hapa kwa leo, siku nyingine nitaongelea aina nyingine za kulika kwa kwa meno kama kuyeyuka kwa meno (tooth

erosion
), abrasion na abfraction wakati huo nitakuwa nimejaribu kupata maelezo ya “abfraction na abrasion” kwa

Kiswahili.

Makala hii imeandikwa na Dr. Augustine Rukoma, daktari bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno. Kwa makala

zaidi, maswali na ushauri mtembelee kwenye blog yake yahttp://rukomadentalanswers.blogspot.com
 
Asante kwa maelezo hayo sanjari na picha,lakini nimejaribu kumchunguza mwanangu na kugundua kuwa akiwa anaumwa ndio kasi ya kutafuna meno huongezeka ila akitibiwa hupungua au kuacha kwa muda..Nifanye nini ili hali ikome kabisa kwa mwanganu wa kiume miaka 2 na miezi 7 sasa..?
 
Asante kwa maelezo hayo sanjari na picha,lakini nimejaribu kumchunguza mwanangu na kugundua kuwa akiwa anaumwa ndio kasi ya kutafuna meno huongezeka ila akitibiwa hupungua au kuacha kwa muda..Nifanye nini ili hali ikome kabisa kwa mwanganu wa kiume miaka 2 na miezi 7 sasa..?
Mkuu Emilias G Mpeleke Hospitali ukamuone daktari ili aweze kupima na kujuwa ni nini chanzo chake hayo maradhi na ndio ataweza kutatuwa hilo tatizo lako pole sana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Emilias G Mpeleke Hospitali ukamuone daktari ili aweze kupima na kujuwa ni nini chanzo chake hayo maradhi na ndio ataweza kutatuwa hilo tatizo lako pole sana.

Asante,ila kama kuna mtu anayemjua daktari bingwa/mzuri wa tatizo hilo aliyeko Jijini Tanga,tafadhali aniPM.Au aweke wazi details zake hapa.Mbarikiwe sana.!
 
Tafadhali naomba msaada kwa mtu au doctor mwenye uelewa anisaidi kupata ushauri au dawa kwa nini natafuna meno ucku.
Umri nina miaka 50.
Mwanaume.
Naishi na kula vzr , kifupi sina shida ndogo ndogo za kusema labda lishe imepungua.
Nafanya mazoezi na afya yangu ni nzuri na nimepima.
Nimetoa maelezo haya ilimwenye uelewa wa tatizo langu aweze kupunguza wigo wa kujiuliza chanzo cha tatizo langu.
Historia yake.
Natafunaga meno usiku mpaka kelele zinasikika kama vile panya anavyokula vitu ucku mkilala.
Natafuna nikipata usingizi mzito.
Swali.
Je kuna dawa?
Ni ugonjwa?
Nifanyeje.
 
haya mkuu ngoja tusubiri wataalam waje watuambie!!

Thnx ngoja waje wajuzi manake ni shida. Kila ninaemuuliza anaona sio tatizo bt tu me naona ni tatizo coz namsumbua mtu nilie lala nae. I can imagine mtu anakoroma ucku binafsi siwezi kulala. So nasikia vibaya pia mm kusumbua.
 
Lala ukiwa umeweka kidole mdomoni hii itasaidia sana pindi ukitaka kupekenya meno utatafuna kidole ukisikia maumivu utaamka cku zikiendelea mwili utajijengea woga pindi taarifa za kutafuna meno zikitumwa kwenye ubongo so kutakuwa na taarifa zinakatza kutafuna meno kwa tuu ubongo utatafsiri kuwa kuna kidole mdomoni KAMA CIJAELEWEKA NITARUDIA TENA.
 
sasa kuna mtu ana tatizo kama lako ika yeye ankula jucha moaka vidole vinatoa damu,,nadhani ni kama tatizo la kukoroma labda uwe una pumzika mchana,au huotagi kama unatafuna usiku??
 
sasa kuna mtu ana tatizo kama lako ika yeye ankula jucha moaka vidole vinatoa damu,,nadhani ni kama tatizo la kukoroma labda uwe una pumzika mchana,au huotagi kama unatafuna usiku??

Mkuu ratiba yangu kwa kawaida iko hivi:
Saa 1 mpaka 9 jioni kazini.
9.30 mpaka 11 nalala.
11 mpaka 1 ucku gym.
Then home again. Unless kuna outing au kumuona mtu mahali.
Nakunywa pombe ocationally tu strictly not more than 3 castle light.
Kwa kawaida hayo ndo maisha yangu.
Sasa kupumzika gani zaidi ya hapo?
 
Dah...! Umenikumbusha nilivyokua nasoma shule ya msingi mkoa fulani kulikua na jamaa alikua na tatizo kama hilo. Lakini yeye ilikua inamtokea mara kwa mara tukiwa darasani. Kabla hajaanza kusaga meno yake lazima anakua anaongea ongea maneno fulani.

Ilikua inawapa shughuli walimu kwani ikimuanza hali hiyo ilikua lazima aitwe dada yake ambaye alikua darasa lingine amchukue jamaa kumrudisha nyumbani huku akisindikizwa na viranja wawili. Jamaa alikua anakua aggresive kimtindo.

Je umekua na tatizo hili kwa muda gani?
 
Dah...! Umenikumbusha nilivyokua nasoma shule ya msingi mkoa fulani kulikua na jamaa alikua na tatizo kama hilo. Lakini yeye ilikua inamtokea mara kwa mara tukiwa darasani. Kabla hajaanza kusaga meno yake lazima anakua anaongea ongea maneno fulani.

Ilikua inawapa shughuli walimu kwani ikimuanza hali hiyo ilikua lazima aitwe dada yake ambaye alikua darasa lingine amchukue jamaa kumrudisha nyumbani huku akisindikizwa na viranja wawili. Jamaa alikua anakua aggresive kimtindo.

Je umekua na tatizo hili kwa muda gani?

May be 8yrs hivi ila mimi sipo hivo ni mpaka nilale and sio kila cku. Mpaka nilale usingizi mzito hivi. U know mm sijijui kwa hilo coz naambiwa tu hua nimelala kwa muda huo.
 
Pole mkuu kwa tazizo lako..
- muone "dentist" atakusaidia...
- atakupima na utatengenezewa "frem" kava ya plastiki unavaa juu ya meno wakati wa kulala...
-tatizo hili mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo...
-athari zake ni kulika kwa "layer" ya juu ya meno hivyo kupata ukakasi mara kwa mara (yaani meno kuwa sensitive sana..
-yupo mtu mwenye tatizo kama lako yeye baada ya kushindwa gharama za hospitali aliamua kufikicha vipande vya magazeti na kuvijaza mdomoni kabla hajalala " ilimsaidia"
Kila la kheri
 
Kweli uzee mwisho chaliNze Babu mzima ni mwendo wa Ucku badala ya Usiku! Nenda ufanyiwe maombi babu!
 
Pole mkuu kwa tazizo lako..
- muone "dentist" atakusaidia...
- atakupima na utatengenezewa "frem" kava ya plastiki unavaa juu ya meno wakati wa kulala...
-tatizo hili mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo...
-athari zake ni kulika kwa "layer" ya juu ya meno hivyo kupata ukakasi mara kwa mara (yaani meno kuwa sensitive sana..
-yupo mtu mwenye tatizo kama lako yeye baada ya kushindwa gharama za hospitali aliamua kufikicha vipande vya magazeti na kuvijaza mdomoni kabla hajalala " ilimsaidia"
Kila la kheri

Thnx mkuu at least I got a starting point. Nitawaona wataalamu wa meno. I just thought kuna tiba permanent na sio ya kuvaa cover la plastic bt anyway its better than nothing!
 
Back
Top Bottom