Kuta za ndani za nyumba na Sakafu kuwa na baridi

Kuta za ndani za nyumba na Sakafu kuwa na baridi

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Wadau naomba kuuliza hii imekaaje maana kuna nyumba moja naishi lakini kuta zake ni baridi sanaa pamoja na sakafu ya chini (tiles) baridi vilevile kiasi kwamba ktk hicho chumba lazima nivae soksi au kubazi.

Je, hii ni hitilafu ktk mfumo wa maji kupelekea kuta kulowa na kuwa baridi au imekaaje watalaam?
 
Ukuta ukiugusa kwa mkono unauonaje? Unahisi ni mkavu au umeloa? inawezekana ukuta unafyonza maji kutoka chini kutokana na kutotumika nailoni ya DPC (Damp Proof course) wakati wa kuinua kuta za boma.

Kwa upande wa tiles/sakafu, kuna uwezekano pia hiyo sehemu ikawa ina asili ya maji maji na wakati wa ujenzi wa msingi haikuwekwa ile nailon (Damp proof membrane) kabla ya kumwaga jamvi ambayo inasaidia kuzuia unyevu usipande juu.
 
Back
Top Bottom