Kutaifisha Gari lililo beba mkaa, hii ikoje kisheria?

Kutaifisha Gari lililo beba mkaa, hii ikoje kisheria?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Wana jukwaa
kwa mtazamo wangu naona kuna kitu hakipo sawa hapa
hivi inakuwaje dereva mwenye Leseni sahihi uliyemtuma kazi apeleke mzigo mahali aamue kuchanganya na mkaa au pengine wakati anarudi abebe mkaa akamatwe halafu gari litaifishwe?
Naweza kuhusianisha kosa hilo na mifano ifuatayo;
  1. Hivi unaonaje kama umemwajiri Daktari atibu watu, akamwandikia mgonjwa dawa isiyo sahihi, adhabu iwe ni kutaifisha kwa Hospitali?
  2. Hivi unaonaje uajiri mwalimu mwenye sifa ila itokee kuwa hana maadili halafu adhabu iwe ni kutaifisha shule?
  3. Unaonaje kumkodishia mtu shamba alime mahindi halafu aamue kuchanganya na bangi adhabu iwe ni kutaifisha shamba?
Mimi sio mwana sheria ila nahisi kuna kitu hakipo sawa
Kwa mtazamo wangu adhabu ingekuwa kali kwa muhusika labda kama mmiliki/muajiri awe ameshirikiana na dereva wake.
 
Back
Top Bottom