hivi watanzania mlitegemea hawa watu wataje mali zao na jinsi walivyopata? msahau kabisa! kwa maana kamwe haiwezekani hata siku moja, labda mjerumani arudi walau kwa miaka miwili tu. Kiongozi yupi anayeweza kufuatilia hili, ikiwa 80% ya matamko ya serikali yetu ni uongo. Ina maana kati ya viongozi wetu 80% ni waongo, na kwa kila mmoja kati ya waliobaki, kwa 80% ni mwongo.....
Lakini hawa viongozi hawana kasoro hata kidogo, bali miongoni mwetu, wengi ndio wajinga, maana wanaingia huko (madarakani) kwa kura zetu.
Kudanganywa mara ya kwanza sio ujinga, lakini kudanganywa mara ya pili, tatu, nne... ni kielelezo dhabiti cha ujinga.
Mwaka 1995, 2000, 2005, 2010... bila utekelezaji ni ujinga!