Kutaka katiba mpya katika Mazingira ya Utawala usiojali Maoni ya wananchi ni kujitoa ufahamu!

Kutaka katiba mpya katika Mazingira ya Utawala usiojali Maoni ya wananchi ni kujitoa ufahamu!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,813
Reaction score
3,430
Malalamiko kila kona ya watu
1) Kutekwa
2) kubambikiwa kesi
3) kupoteza wenye mawazo tofauti,Mh Polepole n.k
4) kufuta hotuba/ maudhui yanayokera viongozi kwenye media
5) kutishia Wakosoaji/ Mawazo Kinzani
6) Wizi wa kura
7) kuua watu 29/10/25
8) Bunge lilipatikana kwa hila kuzinga
9) Kutoheshimu Haki za Watu na kutumia vyombo vya Ulinzi na usalama kwa manufaa ya kikundi kinachokula keki ya Taifa

Hayo yote anayelalamikiwa kuyatenda ndiye atakaye ratibu na kusimamia mchakato wa katiba mpya?!

Atadhibitiwa vipi ili haki itendeke na ionekane ikitendeka?
Tuwe na muafaka wa namna ya kufanya uchaguzi uliohuru na haki ndio tukipata viongozi wanaliochaguliwa na wananchi ndio waratibu zoezi la katiba!
Sio kuwaachia hawa vibaka Wanasiasa wote ni Wanafiki hata Chadema tisiwaamini!

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Mi nlivyosoma...hakuna nchi inayokombolewa kwa makaratasi...
Kama ni waoga msisumbue watu na mitandao.
Hakuna utawala wowote Duniani uliondolewa just simple kwa karatasi..Never ever
 
Ukitaka kila wazo la mtu liwe kwenye katiba;

Tutakuwa na kitabu kikubwa sana.

Ndio maana kuna watu maalum wa kukusanya mawazo kuyacompile na kutoka na kitu kizuri ambacho kinareflect mawazo ya watu.
 
Malalamiko kila kona ya watu
1) Kutekwa
2) kubambikiwa kesi
3) kupoteza wenye mawazo tofauti,Mh Polepole n.k
4) kufuta hotuba/ maudhui yanayokera viongozi kwenye media
5) kutishia Wakosoaji/ Mawazo Kinzani
6) Wizi wa kura
7) kuua watu 29/10/25
8) Bunge lilipatikana kwa hila kuzinga
9) Kutoheshimu Haki za Watu na kutumia vyombo vya Ulinzi na usalama kwa manufaa ya kikundi kinachokula keki ya Taifa

Hayo yote anayelalamikiwa kuyatenda ndiye atakaye ratibu na kusimamia mchakato wa katiba mpya?!

Atadhibitiwa vipi ili haki itendeke na ionekane ikitendeka?
Tuwe na muafaka wa namna ya kufanya uchaguzi uliohuru na haki ndio tukipata viongozi wanaliochaguliwa na wananchi ndio waratibu zoezi la katiba!
Sio kuwaachia hawa vibaka Wanasiasa wote ni Wanafiki hata Chadema tisiwaamini!

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Mkuu BOB LUSE, pongezi kwa uzi huu unaochochea fikra na kujadili mambo mazito ya mustakabali wa nchi yetu.
Umetupa uchambuzi mzuri unaogusa kiini cha mkwamo wa kisiasa Tanzania. Nakubaliana nawe kwa 100% kwenye sehemu kuu ya hoja yako, hususan katika mambo yafuatayo:
  1. Mazingira Mabaya ya Kisiasa: Ni kweli kabisa, huwezi kuzungumzia kupata sheria mama (Katiba) kukiwa na matukio ya utekaji, kubambikiwa kesi, na kuminya uhuru wa mawazo kinzani. Mazingira haya hayatoi utulivu wa kiakili kujenga nchi.
  2. Mgongano wa Maslahi (Conflict of Interest): Una mantiki kubwa unapohoji kuwa mtawala anayetuhumiwa kuminya demokrasia hawezi kuwa mratibu muaminifu wa katiba itakayokuja kumbana yeye mwenyewe.
  3. Tahadhari dhidi ya Wanasiasa: Uko sahihi kuwakumbusha wananchi kuwa wanasiasa wote (hata wa upinzani) wanaongozwa na maslahi ya kisiasa na unafiki upo kila upande.
Hata hivyo mkuu, kuna maeneo mawili ambayo naona umeenda mrama ki-mantiki na ki-mikakati, na hapa ndipo ninapokukosoa:
Kwanza, kuhusu suala la kifalshafa na ki-mantiki (Logical Contradiction):

Umeshawishi kuwa tusimwamini mtawala wa sasa kuratibu Katiba Mpya, lakini papo hapo unapendekeza kuwa "tuwe na muafaka wa namna ya kufanya uchaguzi uliohuru na haki." Swali langu la msingi kwako ni hili: Kama mtawala huyu haaminiki katika kutengeneza Katiba Mpya, utamwamini vipi aketi kwenye meza moja na nyinyi kufanya muafaka wa kupatikana kwa Uchaguzi Huru na wa Haki unaoenda kumtoa madarakani? Kama ni mbinafsi na dikteta kwenye katiba, atabadilikaje na kuwa muungwana kwenye muafaka wa uchaguzi? Hapa unajipinga mkuu.
Pili, kuhusu mbinu ya uratibu wa Katiba (Operational Strategy):
Umekwama kwa kudhani kuwa mchakato wa Katiba Mpya lazima uratibiwe na kusimamiwa na serikali au wanasiasa pekee. Katiba bora duniani haziandikwi na wanasiasa waliopo madarakani. Mchakato unaweza kuandaliwa na kuratibiwa na Kamati Maalum ya Kitaifa inayoundwa na watu wanaoheshimika, waaminifu, na wasio na upande (Neutral Experts)—kama vile viongozi wa taasisi za kidini, asasi za kiraia (NGOs), na wanasheria waandamizi walio huru.
Mbona wenzetu kule Kenya waliweza? Kenya walipitia vipindi kigumu sana cha utawala wa kiimla na mifumo mibovu, lakini kupitia shinikizo la umma na ushiriki wa jopo huru la wataalamu (Committee of Experts), walifanikiwa kupata Katiba Mpya ya mwaka 2010. Katiba hiyo mpya ndiyo iliyozaa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) na Mahakama Huru, mifumo ambayo sasa inalinda demokrasia yao. Kama Kenya waliweza kuweka wanasiasa pembeni na kutumia asasi za kiraia na wanasheria kupata katiba mpya, kwa nini sisi Watanzania tushindwe na kuishia kujikatia tamaa?
Hitimisho: Kulia lia na kusubiri "uchaguzi huru" chini ya sheria hizi hizi na katiba hii hii inayompa Rais mamlaka ya kuteua kila mkurugenzi na kila mjumbe wa tume ya uchaguzi, ndiko kujitoa ufahamu halisi. Katiba Mpya ndiyo inayotakiwa ianze ili itengeneze uwanja sawa (Level playing field), na inawezekana tukiwanyang'anya wanasiasa mchakato huu na kuwapa wataalamu huru na viongozi wa kijamii.
Nawasilisha mkuu, tupe miongozo yako kwenye hili!
 
Serikali inayoamini wananchi wote ni ng'ombe, manyani, nyumbu, misukule, makunguru, wajinga, wasio na akili, watoto, wasio na upeo wa kufikiri na kuhoji, nk. Kamwe haiwezi kukupatia katiba yenye tija kwa nchi na wananchi wake.
 
Back
Top Bottom