Kutana na muuza maji ya madumu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi zaidi ya mtu mwenye shahada

Hizo hesabu zako hazijazingatia mambo yafuatayo:
1.Yeye ananunua ndoo moja shilingi ngapi huko anakoenda kuchota?
Tuchukulie ananunua ndoo moja 200.
Ukichukua 200*50=10,000 kwa siku, 300,000 kwa mwezi. Kwahiyo toa 300,000 kutoka kwenye ile 750,000. Inabaki 450,000

2. Bili ya msosi na bia uliyoweka ni sawa na 9,000 kwa siku. Kwa mwezi ni 270,000. Ukitoa inabaki 180,000

3.Vyumba alivyopanga vitatu, kodi tuchukulie 60,000 kwa mwezi. Ukitoa inabaki 120,000

4.Nauli ya mtoto kwenda shule na hela ya kula, tuweke 1,000 kwa siku, 30,000 kwa mwezi. Hapo inabaki 90,000

5.Vocha, weka 500 kwa siku. 15,000 kwa mwezi. Inabaki 75,000

6.Mkaa, Mafuta taa, Gesi weka 2,000 kwa siku, 60,000 kwa mwezi. Inabaki 15,000

7. Matengenezo ya dumu likitoboka au baiskeli ikiharibika weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 10,000

8.Weka ya saloon yeye na wife 5000 kwa mwezi. Inabaki 5000

9.Nauli nauli za bodaboda na daladala, weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 0.

10. Huyo jamaa kakuona wewe mbumbumbu akakujaza ujinga na wewe ukaubeba bila kuhoji, hana kiwanja mbezi wala mfano wake
 
Is there any job security kwake , vipi akiugua ? Changamoto za tabia nchi? Nk
 
UCHAMBUZI WA KIMAZABE KAMA HUU HUFANYWA NA WATU WALIOKIMBIA UMANDE.

YANI UNACOMPARE DEGREE NA NGUVU ZA KUBEBA MADUMU YA MAJI?

HALAFU KUMBE NI 750,000 KWA MWEZI

NA ANAVYOLALA ANAOMBEA SHIDA YA MAJI ISITATULIWE.

ANAAMKA SAA 10 ALFAJIRI NA ANAFANYA KAZ HADI SAA 5 USIKU (HATARI)...
 
Ina maana hii biashara haina gharama za uendeshaji? Hayo maji anayapata bure? Mkokoteni hauna matengenezo? Hii story ni kutoka kwenye vijiwe vya gahawa
 
sema sio kila siku kuna changamot ya maji mitaa ya makanya,daybreak,kwa bonge nk
ngosha,kiziwi,ostadh,msambaa nk
bt uchambuzi wako ni mwanasesere
*hii ni fallacy
 
Ha ha ha ha nashukuru kwa taarifa, kesho na mimi nitapita apo
 

Mbona umejibu kwa hasira sana?
 
Wewe jamaa hiyo kazi kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 3 usiku si Ni kifo hicho??
Then unapata 750,000!!
Bora huyo mwenye degree anayepewa take home ya 500,000
Kumbuka huyu kuna muda anakua free mchana mwingi tu
 
Kwanza mazoezi mazuri tu, pili anawapa maji raia ambayo ni uhai, tatu anatunza familia yake na kufanya maendeleo..hongera zake, nawajuwa 4 au 5 mitaa ya Sinza Lion Hotel na Queen of Sheba, wako kama huyu..
Yeah mkuu. Unaeza dharau kaz ndogo kumbe ndo yenye hela
 
Hayo maji anaenda kuchota bure.? Maana sijaona ukitoa hizo gharama.

Je siku akiumwa.? Umetoa hesabu hizo.?

Siku mvua ikinyesha, watu wanakinga maji ya kwenye mabati.
Maji anachota bure pale magomeni usalama
 
Kwamba mwenye degree haya matumizi hayafanyi?

Maji wanapewa bure magomeni usalama.

Wewe hujaelewa Nilichoandika.

Sijasema matumizi yake bali nimesema anachoingiza.

Mtoto wake anasoma turiani primary... Ipo karibu na home, anatembea kwa miguu.
 
Ina maana hii biashara haina gharama za uendeshaji? Hayo maji anayapata bure? Mkokoteni hauna matengenezo? Hii story ni kutoka kwenye vijiwe vya gahawa
Nimezungumzia anaingiza shilingi ngapi... Hayo mengine ni uyatolee uzi wako
 
Kuna wafanyakazi call center ya Vodacom wana degree na wanapokea take home ya 340,000 kwa mwezi. Huwezi linganisha na huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…