Maisha yana hitaji akili zaidi ya akili za kukariri maandishi kadha wa kadha toka kwenye vitabu. Anyway, ukiona pia hio kazi amnayofanya huyo NGOSHA ni bora basi nawe nenda huko ukaifanye kibunifu zaidi.Salaam wakuu,
Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.
Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.
Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.
Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni.
Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakua amemaliza maji na anakwenda kupumzika.
Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakua ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakua nipesa nyingi zaid ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.
Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.
Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.
Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.
Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.
Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.
Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.
Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.
Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...
Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.
You are right!Pumba, hata changudoa muuza k anatengeneza pesa zaidi
Ujanja kupata sio kuwai,... Akili kumkichwa ata uyo mwenye degree akifikiria nje kidogo ya uwezo wake ata piga hela tuu,zaidi ya mshahara wakr
Mchanganuo wako ni mzuri,ila ngosha anapambana na hali yake naona hilo ndilo la msingi.Hizo hesabu zako hazijazingatia mambo yafuatayo:
1.Yeye ananunua ndoo moja shilingi ngapi huko anakoenda kuchota?
Tuchukulie ananunua ndoo moja 200.
Ukichukua 200*50=10,000 kwa siku, 300,000 kwa mwezi. Kwahiyo toa 300,000 kutoka kwenye ile 750,000. Inabaki 450,000
2. Bili ya msosi na bia uliyoweka ni sawa na 9,000 kwa siku. Kwa mwezi ni 270,000. Ukitoa inabaki 180,000
3.Vyumba alivyopanga vitatu, kodi tuchukulie 60,000 kwa mwezi. Ukitoa inabaki 120,000
4.Nauli ya mtoto kwenda shule na hela ya kula, tuweke 1,000 kwa siku, 30,000 kwa mwezi. Hapo inabaki 90,000
5.Vocha, weka 500 kwa siku. 15,000 kwa mwezi. Inabaki 75,000
6.Mkaa, Mafuta taa, Gesi weka 2,000 kwa siku, 60,000 kwa mwezi. Inabaki 15,000
7. Matengenezo ya dumu likitoboka au baiskeli ikiharibika weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 10,000
8.Weka ya saloon yeye na wife 5000 kwa mwezi. Inabaki 5000
9.Nauli nauli za bodaboda na daladala, weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 0.
10. Huyo jamaa kakuona wewe mbumbumbu akakujaza ujinga na wewe ukaubeba bila kuhoji, hana kiwanja mbezi wala mfano wake
.... kulia kama Nyau..mkuu kwa mimi sijaona cha ajabu hapo, wengi mshahara ni mdg ila malupulupu ya maana
wakati unaleta bandiko umefikiria mambo kama wakiumwa, wakipata dharura nani yuko kwenye nafasi ya kuendelea kuingiza pesa.
yaani wewe huna tofauti na mkuu wa mkoa wa zamani wa morogoro "lutengwe" akiwa katavi aliwahamasisha watu kulima kilimo cha maembe alipo fukuzwa ni kulia kama nyau
Ni hiyo mitaa ndio mitaa ya mbunge mstaafu wa Kino!wanajificha kwenye kuuza maji kumbe wana biashara nyingine haramu kama sio biashara basi ni chuma ulete uyo.....
Inaonekana kweli kipato chako ni duni,kuhama toka Sinza kwenda kuishi Makanya maana yake ni kwamba uchumi wako umeyumba. Pole sana mkuu..!!Salaam wakuu,
Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.
Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.
Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.
Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni.
Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakua amemaliza maji na anakwenda kupumzika.
Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakua ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakua nipesa nyingi zaid ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.
Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.
Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.
Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.
Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.
Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.
Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.
Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.
Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...
Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.
nimekupa uchambuzi wa maeneo yote ili ujue kwamb kipnd maji yakizngua ndo inakuwa dili xan.Sasa mimi sizungumzii upande wa daybreak huko
Mkuu, kama wewe unafuata maji kwa Idd Azan, siyo wote wana muda huo.. Jamaa anauza maji kuwe/kusiwe na shida ya majinimekupa uchambuzi wa maeneo yote ili ujue kwamb kipnd maji yakizngua ndo inakuwa dili xan.
mf hicho kitaa cha makanya maji yapo kwa idd azan hapo,kwa alex massawe pemben,msikitini,makanya bonden nk
*ikitokea maji yakizngua ndo inakuwa dili!