Kutana na muuza maji ya madumu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi zaidi ya mtu mwenye shahada

Kutana na muuza maji ya madumu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi zaidi ya mtu mwenye shahada

Kwahio watu wote wenye degree wanapata chini ya 750k/month?
 
Salaam wakuu,

Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.

Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.

Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.

Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni.

Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakua amemaliza maji na anakwenda kupumzika.

Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakua ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakua nipesa nyingi zaid ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.

Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.

Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.

Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.

Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.

Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.

Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.

Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.

Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...

Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.
Maisha yana hitaji akili zaidi ya akili za kukariri maandishi kadha wa kadha toka kwenye vitabu. Anyway, ukiona pia hio kazi amnayofanya huyo NGOSHA ni bora basi nawe nenda huko ukaifanye kibunifu zaidi.
 
kwahiyo watu waache shule wakabebe maji au ? hata kama angekuwa anapata 2mln bado ni mateso ya hali ya juu.
 
vipi akiumwa au kupata dharula wateja wanampa advance ili akipona awapelekee huduma?elimu ni elimu tu haifananishwa na pesa hata siku moja!unaweza kuwa bilionea mjinga na unaweza kuwa msomi fukara lkn baadae ukapata pesa!je mjinga wa miaka arobaini huko atapata elimu ya secondary lini na lini atakuwa graduate acheni masihara na elimu nyie!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya maguvu sana-quite labour intensive! Maisha ya shida sana, ndio maana ziligunduliwa mashine kupunguza mwanadamu kuumia na kazi ngumu. Sitaki hiyo kazi. Kwanza haina hadhi !
 
Hizo hesabu zako hazijazingatia mambo yafuatayo:
1.Yeye ananunua ndoo moja shilingi ngapi huko anakoenda kuchota?
Tuchukulie ananunua ndoo moja 200.
Ukichukua 200*50=10,000 kwa siku, 300,000 kwa mwezi. Kwahiyo toa 300,000 kutoka kwenye ile 750,000. Inabaki 450,000

2. Bili ya msosi na bia uliyoweka ni sawa na 9,000 kwa siku. Kwa mwezi ni 270,000. Ukitoa inabaki 180,000

3.Vyumba alivyopanga vitatu, kodi tuchukulie 60,000 kwa mwezi. Ukitoa inabaki 120,000

4.Nauli ya mtoto kwenda shule na hela ya kula, tuweke 1,000 kwa siku, 30,000 kwa mwezi. Hapo inabaki 90,000

5.Vocha, weka 500 kwa siku. 15,000 kwa mwezi. Inabaki 75,000

6.Mkaa, Mafuta taa, Gesi weka 2,000 kwa siku, 60,000 kwa mwezi. Inabaki 15,000

7. Matengenezo ya dumu likitoboka au baiskeli ikiharibika weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 10,000

8.Weka ya saloon yeye na wife 5000 kwa mwezi. Inabaki 5000

9.Nauli nauli za bodaboda na daladala, weka 5000 kwa mwezi. Inabaki 0.

10. Huyo jamaa kakuona wewe mbumbumbu akakujaza ujinga na wewe ukaubeba bila kuhoji, hana kiwanja mbezi wala mfano wake
Mchanganuo wako ni mzuri,ila ngosha anapambana na hali yake naona hilo ndilo la msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanajificha kwenye kuuza maji kumbe wana biashara nyingine haramu kama sio biashara basi ni chuma ulete uyo.....
 
mkuu kwa mimi sijaona cha ajabu hapo, wengi mshahara ni mdg ila malupulupu ya maana

wakati unaleta bandiko umefikiria mambo kama wakiumwa, wakipata dharura nani yuko kwenye nafasi ya kuendelea kuingiza pesa.

yaani wewe huna tofauti na mkuu wa mkoa wa zamani wa morogoro "lutengwe" akiwa katavi aliwahamasisha watu kulima kilimo cha maembe alipo fukuzwa ni kulia kama nyau
.... kulia kama Nyau..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nafikiri lengo la mleta mada sio kulinganisha pato la huyu na degree, hapana lengo lake ni kwamba vijana waliomaliza degree wawe tayari kupambana na maisha wakitumia uwezo wao wote ikiwemo shule yao wasiwekeza zaidi katika kusubiri ajiri yaani wazisuburi huku wanaweza kutengeneza mawazo yao mazuri yaliyoenda shule wakaweza kufikia malengo wanayotaka. mfano kama huyu anaweza kuuza dumu hamsini za maji kwa siku kwa shillingi mia tano kwa dumu wao waweze kuuza dumu miatatu kwa siku kwa shillingi 300 kwa kuwauzia jumla hao wakina ngosha nao wauze mia tano. badala ya kutumia mkokoteni yeye akodi pick up akianagalia gharama za usafiri ukilinganisha na yeye kukaa bure home. ikiwa usafiri 20,000 anaweza kupata 70,000 toa gharama za maji 5000 anabaki 65,000 kwa muda wa masaa machache sana akiwa hajaumia.
 
Salaam wakuu,

Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.

Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.

Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.

Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni.

Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakua amemaliza maji na anakwenda kupumzika.

Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakua ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakua nipesa nyingi zaid ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.

Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.

Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.

Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.

Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.

Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.

Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.

Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.

Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...

Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.
Inaonekana kweli kipato chako ni duni,kuhama toka Sinza kwenda kuishi Makanya maana yake ni kwamba uchumi wako umeyumba. Pole sana mkuu..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni upuuzi umalze degree alaf uanze kuuza maji! Hiyo ni laana na matumizi mabaya ya taaluma.
 
Sasa mimi sizungumzii upande wa daybreak huko
nimekupa uchambuzi wa maeneo yote ili ujue kwamb kipnd maji yakizngua ndo inakuwa dili xan.
mf hicho kitaa cha makanya maji yapo kwa idd azan hapo,kwa alex massawe pemben,msikitini,makanya bonden nk

*ikitokea maji yakizngua ndo inakuwa dili!
 
Mkuu, kama wewe unafuata maji kwa Idd Azan, siyo wote wana muda huo.. Jamaa anauza maji kuwe/kusiwe na shida ya maji
 
Back
Top Bottom