Kutana na muuza maji ya madumu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi zaidi ya mtu mwenye shahada

Kutana na muuza maji ya madumu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi zaidi ya mtu mwenye shahada

mkuu kwa mimi sijaona cha ajabu hapo, wengi mshahara ni mdg ila malupulupu ya maana

wakati unaleta bandiko umefikiria mambo kama wakiumwa, wakipata dharura nani yuko kwenye nafasi ya kuendelea kuingiza pesa.

yaani wewe huna tofauti na mkuu wa mkoa wa zamani wa morogoro "lutengwe" akiwa katavi aliwahamasisha watu kulima kilimo cha maembe alipo fukuzwa ni kulia kama nyau

Hahahahaaaaa
Kulia kama nyau tena.
 
Kuna mama muuza mandazi mmoja yeye anaingiza zaidi ya 50,000/= per day as net profit.
Kwa siku anapika mandazi 200, chapati 200, na donat 200

Kila andazi 1 anapata 50 as profit ( 50*200 = 10,000 )
Kila chapati 1 anapata 150 as profit ( 150 * 200 = 30,000)
Kila donalt 1 anapata 150 as profit ( 150 * 200 = 30,000)

Jumla kuu > 70,000 ingawa inaweza kuwa chini ya hapo.
Chukua ni 50,000/= ( 50,000 * 30 = 1,500,000/=)
Muda wa kazi ni 12: 30 asubuhi hadi 5:30 asubuhi.
Saa 12:00 jioni hadi 5 :00 usiku.

Soko lake : Kakwaa tenda zote za kwenye mashule ya msingi na sekondari
: Vyuo karibu vitatu amazambaza huduma yake
: Watu wa mtaani kwake karibu wote wanamtegemea yeye.

Ushauri :

-- Usidharau kazi ya mtu,
-- Elimu sio pesa ila ikusaidie kuitafuta pesa.
-- Elimu sio lazima ukalishe matako darasani.
-- Maskini wakubwa dunia hii ni wasio na kazi wakifuatiwa na waajiriwa wakimalizia waajiri.

Kama hukubaliani na mimi kunya gunzi.
 
Wewe jamaa hiyo kazi kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 3 usiku si Ni kifo hicho??
Then unapata 750,000!!
Bora huyo mwenye degree anayepewa take home ya 500,000
OhahahahaOhahahahaaa umejua kujitetea
 
Salaam wakuu,
Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.

Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.

Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.

Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni. Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakuwa amemaliza maji na anakwenda kupumzika.

Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakuwa ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakuwa ni pesa nyingi zaidi ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.

Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.
Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.

Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.

Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.

Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.
Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.
Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.

Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...
Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.

Mbona umefanya hesabu rahisi hayo maji anayapata bure? Hapo anapouza hapalipii? Ghalama za matengenezo ya mkokoteni kwa mwezi sh ngapi?
Punguza tamaa kila kitu kinachangamoto zake
 
Pia ujatuambia siku akiumwa hesabu hiyo inafika vp au akiwa na dharula inayomfanya asiuze maji siku hiyo na pia utuambie kipindi cha mvua zinaponyesha uwa anauza maji kwa watu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mama muuza mandazi mmoja yeye anaingiza zaidi ya 50,000/= per day as net profit.
Kwa siku anapika mandazi 200, chapati 200, na donat 200

Kila andazi 1 anapata 50 as profit ( 50*200 = 10,000 )
Kila chapati 1 anapata 150 as profit ( 150 * 200 = 30,000)
Kila donalt 1 anapata 150 as profit ( 150 * 200 = 30,000)

Jumla kuu > 70,000 ingawa inaweza kuwa chini ya hapo.
Chukua ni 50,000/= ( 50,000 * 30 = 1,500,000/=)
Muda wa kazi ni 12: 30 asubuhi hadi 5:30 asubuhi.
Saa 12:00 jioni hadi 5 :00 usiku.

Soko lake : Kakwaa tenda zote za kwenye mashule ya msingi na sekondari
: Vyuo karibu vitatu amazambaza huduma yake
: Watu wa mtaani kwake karibu wote wanamtegemea yeye.

Ushauri :

-- Usidharau kazi ya mtu,
-- Elimu sio pesa ila ikusaidie kuitafuta pesa.
-- Elimu sio lazima ukalishe matako darasani.
-- Maskini wakubwa dunia hii ni wasio na kazi wakifuatiwa na waajiriwa wakimalizia waajiri.

Kama hukubaliani na mimi kunya gunzi.
Vyuo,shule,mtaani hajaajiri watu wa kusambaza ? Kama ameajiri anawalipa sh ngapi ? kama anasambaza mwenyewe anapika sa ngapi na anasambaza sa ngapi , kwa usafiri gani, bure au anaulipia ? anapika peke ake ? Kama ana msaidizi anamlipa sh ngapi ?
Acheni biashara za makaratasi, ingekua hivyo wauza maandazi wote wangekua matajiri, kweli maandazi yana faida ila tusipaishe namna hiyo

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Msomi ktk ubora wako naona umeshakokotoa working hours hapo. I love us
Wewe jamaa hiyo kazi kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 3 usiku si Ni kifo hicho??
Then unapata 750,000!!
Bora huyo mwenye degree anayepewa take home ya 500,000
 
Vyuo,shule,mtaani hajaajiri watu wa kusambaza ? Kama ameajiri anawalipa sh ngapi ? kama anasambaza mwenyewe anapika sa ngapi na anasambaza sa ngapi , kwa usafiri gani, bure au anaulipia ? anapika peke ake ? Kama ana msaidizi anamlipa sh ngapi ?
Acheni biashara za makaratasi, ingekua hivyo wauza maandazi wote wangekua matajiri, kweli maandazi yana faida ila tusipaishe namna hiyo

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app

Kabla ya kuandika chochote soma kwa makini.
Unajua maana ya "net profit"? Au hujapita shule?
Mambo ya uchumi uliwahi kuyasomasoma labda.?
 
Hela si kila kitu kumbukeni......

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Hela si kila kitu kumbukeni......

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app

Hhaaha, usitake kuchekesha jukwaa weye.
Kabla ya kusema pesa sio kila kitu hakikisha unakua nazo za kutosha.
 
Hhaaha, usitake kuchekesha jukwaa weye.
Kabla ya kusema pesa sio kila kitu hakikisha unakua nazo za kutosha.
Sawa nimekuelewa,akili yako niile ya kufanya kazi ya kuzibua vyoo kwa mwaka 1 kwa mshahara wa 1,000,000 kwa mwezi na kuacha kazi ya ofisini ya 500,000 .
Mmetekwa mawazo,akili yenu yote inaona PESA ndio the end wakati ni means to an end.

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Sawa nimekuelewa,akili yako niile ya kufanya kazi ya kuzibua vyoo kwa mwaka 1 kwa mshahara wa 1,000,000 kwa mwezi na kuacha kazi ya ofisini ya 500,000 .
Mmetekwa mawazo,akili yenu yote inaona PESA ndio the end wakati ni means to an end.

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app

Acha nizibue choo wanilipe 1,000,000/= kwa mwezi.
Baada ya mwaka nikuajiri kama technician, nikuingize ofisin nikupe kiyoyozi, chai, na usafiri.
Nikunyonye ubaki na nguo tu, Mwisho wa siku ndo akili inakufunguka unastaafu una nyumba tu ya kuishi, kifuatacho :
Kufa na pressure.
 
Sawa nimekuelewa,akili yako niile ya kufanya kazi ya kuzibua vyoo kwa mwaka 1 kwa mshahara wa 1,000,000 kwa mwezi na kuacha kazi ya ofisini ya 500,000 .
Mmetekwa mawazo,akili yenu yote inaona PESA ndio the end wakati ni means to an end.

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app

Hujuoni ulivyoongea mapumba na mashudu, huko ofisini unajiona umefika kiasi cha kumdharau mzibua choo anayeingiza faida badala ya mshahara? Unataka kutuambia uko tayari kulipwa mshahara nusu kisa tu kuna viyoyozi na chai?
Think again bro.
 
Kabla ya kuandika chochote soma kwa makini.
Unajua maana ya "net profit"? Au hujapita shule?
Mambo ya uchumi uliwahi kuyasomasoma labda.?
Watu wengi wanatoa mapovu kwenye uzi huu kwa kutoelewa maana ya hiyo net profit
 
Back
Top Bottom