Kutana na Mwanamke Maarufu mwizi zaidi duniani Phoolan Devi,

Kutana na Mwanamke Maarufu mwizi zaidi duniani Phoolan Devi,

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kutana na Mwanamke Maarufu mwizi zaidi duniani Phoolan Devi,

Kutoka kwenye unyanyaswa kijisia, kuwa mwizi, kuingia jela na hadi kuwa mbunge kutetea wanawake nchini india.

Anakumbukwa kwa famous qoute inayosema.

"If there were justice in the world, I would have been a nobody"

Na hii ndio strory yake, shu
20241103_101320.jpg
20241103_101317.jpg
ka nayo
Phoolan Devi alizaliwa katika familia maskini huko Uttar Pradesh, India, na alikabiliwa na ubaguzi wa kijinsia na kijamii kutokana na hali yake ya umaskini na kabila lake.

Akiwa msichana mdogo, alipitia unyanyasaji mkubwa, ikiwa ni pamoja na ndoa ya mapema na dhuluma za kijinsia. Haya yote yalimsukuma kuasi na kujiunga na kundi la majambazi wa mitaani (bandits), akawa miongoni mwa majambazi wakuu wa India.
 
2.Phoolan Devi aliongoza mashambulizi dhidi ya vijiji, hasa akiwalenga wale waliomdhulumu au kudhulumu watu wa jamii yake.

Mojawapo ya matukio yake maarufu ni mauaji ya Behmai mwaka 1981, ambapo kundi lake liliwaua wanaume kadhaa kutoka kijiji hicho, likiwa ni kisasi kwa unyanyasaji alioupitia mikononi mwa watu wa kijiji hicho. Hii ilimletea umaarufu na hofu kote nchini India.
Baada ya miaka kadhaa ya maisha ya uwizi na kuwindwa na polisi, Phoolan Devi alijisalimisha kwa serikali mnamo 1983 mbele ya maelfu ya watu na waandishi wa habari.

Baadaye alifungwa lakini aliachiliwa huru mwaka 1994, na baadaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la India, akipigania haki za wanawake na watu wa jamii za hali ya chini.

Phoolan Devi aliuawa mwaka 2001, lakini hadithi yake iliendelea kuwa ya kuvutia na yenye utata, akijulikana kama "Bandit Queen" kutokana na maisha yake ya uwizi na mapambano kwa ajili ya haki.
20241103_101429.jpg
20241103_101542.jpg

Phoolan Devi aliuawa mnamo Julai 25, 2001. Alipigwa risasi na mhalifu aitwaye Sher Singh Rana, ambaye alidai kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanaume wa kijiji cha Behmai yaliyofanywa Phoolan na kundi lake miaka ya nyuma💔
20241103_101429.jpg
 
Simulizi hii ni kwa mujibu wa Unite wa Twitter
 
Ndo imeisha!?
Stelingi alikufwa

Phoolan Devi aliuawa mnamo Julai 25, 2001. Alipigwa risasi na mhalifu aitwaye Sher Singh Rana, ambaye alidai kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanaume wa kijiji cha Behmai yaliyofanywa Phoolan na kundi lake miaka ya nyuma💔
 
Back
Top Bottom