Uchaguzi 2020 Kutangaza maandamano pekee hakutoshi, kunahitaji maandalizi. Tujiulize kwanini maandamano ya Seif Zanzibar hayakufanikiwa

Kama haupo nchini rudi uyaone. Na kama upo nchini utakuwa ushajionea mwenyewe. Usinipotezee muda kuyarudia. Soma hata humu JF Kuna threads kibao zimeyaeleza.
Hakuna pahala panaonesha dhuluma bali watu wana lalama tuu
 

HATURUHUSU MAANDAMANO
 
Waandamanaji hapa kwetu Tz walio na nia ama uwezo wa kuacha shughuri zao kwa ajili ya maabdamano ni wachache mno,
Unaweza kujitoa kuandamana ukajikuta upo na watu wasiofika mia.
Haya ni mazungumzo yatakayoishia hapahapa,
Na mambo mengine yataendelea kama siku zote.
 
Hapa sioni maandamano yakitokea,
Uchaguzi umeisha na maisha yataendelea kama kawaida!
Lakini pia ieleweke wanaohitaji maandamano ni wachache kuliko wasioyahitaji!
 
Watanzania waishio nje ya nchi (TANZANIA DIASPORA) wameanza kuandamana kupinga UCHAFUZI uliofanyika juzi hapo nyumbani Tanzania!

Hawa ni ndugu zetu kutoka Ulaya ya Kaskazini (Sweden 🇸🇪, Norway 🇳🇴 na Denmark 🇩🇰) ambao tayari wameanza maandamano yao nje ya Ubalozi wetu uliopo Stockholm, Sweden...

Watanzania waishio nchini Ufaransa 🇫🇷 wanaandaa maandamano hayo kesho Jumatatu, November 2, 2020 nje ya Ubalozi wa Tanzania 🇹🇿 nchini Ufaransa 🇫🇷.

Maandamano yataanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana!

Baada ya maandamano, WAZANZIBARI waishio nchini hapa, kwa kuongozwa na Balozi wetu (BABU MZANZIBARI), watazindua Ubalozi wetu (Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar nchini Ufaransa)... Ofisi za Ubalozi wetu zipo mitaa ya TROCADÉRO, karibu sana na mnara wa EIFFEL...

Kwa niaba ya Wazanzibari wote waishio nchini hapa Ufaransa, mimi, BABU MZANZIBARI, Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa, natumia fursa hii kuwakaribisha ndugu zetu Watanzania waishio nchini hapa, katika uzinduzi wa Ubalozi wetu!

Usafiri, kula, kunywa ni kwa gharama yangu mwenyewe!...

Kwa kauli moja, tumekubaliana kuwa hatuitambui serikali haramu ya John Pombe Joseph Magufuli! Hatuitambui serikali haramu ya Hussein Ali Hassan Mwinyi!

Rais wa Zanzibar tunayemtambua ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar!... Na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayemtambua ni Tundu Antipas Lissu, aliyechaguliwa na Watanzania!...

Mungu ibariki Zanzibar yenye mamlaka kamili, Mungu ibariki Tanzania!... 🙏🏾

👉🏾👉🏾👉🏾 Sambaza ujumbe huu umfikie kila Mtanzania mpenda haki!...👍🏾
 
Maandamano yapo tulikwambieni mapema uhanisi sasa basi
Sawa si kesho tarehe 2 au tarehe 2 ya mwezi upi?

Hii nchi hadi kufikia hapa kuna watu wameumiza vichwa sio genge la wahuni wachache waje kuvuruga AMANI.
 
Hahah!


Endelea kujidanganya
 
Hivi ninyi wapinzani akili huwa mnaweka wapi?Maana tayari kitendo cha ccm kujikuta wako wao peke yao,kimewafanya waanze kufedheheka.Hawana furaha kamwe.Tunaishi nao na tunawasikia.
Maana ushindi wao sio dhidi ya wapinzani,ila ni dhidi ya Tanzania.
Akili za kuku hizi..!!!
 
Sasa hivi tunapinga Magufuli kuwa rais maana hakupata ridhaa ya watanzania.
Hamna na wala uwezo wa kumpinga Rais mteule. Kesho rasmi anaapishwa na viongozi wenu wajiandae
 
Sisi huku Zanzibar tumechoka maandamano yasio na tija
tunaomba tuletewe silaha tupambane na hawa wanajeshi wa Burundi
tumechoka kona damu zetu zinamwagika

Kuna maelfu ya vijana wapo tayari kupambana mpaka wafe
 
Kama haupo nchini rudi uyaone. Na kama upo nchini utakuwa ushajionea mwenyewe. Usinipotezee muda kuyarudia. Soma hata humu JF Kuna threads kibao zimeyaeleza.
Pamoja na hayo yote je,huko mitaani kwa raia hali ikoje kwamba watu wana hasira au wako bize na mambo yao?
 
Hakuna jeshi la Burundi wala nn Burundi hawawez kutoa wana jeshi wake wakat wao mwenyewe wako hatarini jirani zao kongo kila uchao mambo hovyo na kumbuka wamepakana na majimbo ambayo hayako salama so lazma watie nguvu kulinda maeneo yao
Lugha zao mbona ni za kiswahili cha kifaransa?
 
Hamna na wala uwezo wa kumpinga Rais mteule. Kesho rasmi anaapishwa na viongozi wenu wajiandae
Kesho!!!
Hivi unafanya nn humu mtu mjinga kama wewe? JF siku hizi imejaa watu ambao ni less informed kama wewe?? Kesho anaapishwa yule mkuu wa mkoa kule visiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…