Kutaniko kubwa la vijana wa vyuo uwanja wa Taifa

Kutaniko kubwa la vijana wa vyuo uwanja wa Taifa

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,203
Reaction score
35,840
Wakuu,

Vijana ndio nguvu ya nchi na tegemeo kusukuma maendeleo ya nchi kuanzia ngazi ya familia. Taifa lenye vijana wacha Mungu kikamilifu litajengwa kwenye misingi bora na kuepuka maovu mengi.

Umoja wa vyuo Karistimatiki Katoliki umeandaa Usiku wa Sifa ijumaa hii pale uwanja wa Taifa ambao vijana kutoka vyuo vyetu vyote watakutana kumsifu Mungu na kupata mahubiri kutoka kwa Mwl Dr Arbogast Kanuti na Askofu mkuu mstaafu Mhashamu Josephat Lebulu.

Usiku huu umeandaliwa na umoja wa vyuo kwaajili ya watu wote kutoka dini zote na si wanachuo pekee.

Kwaya zitazohudumu ni Lord's grace praise team, Ebenezer praise and worship team, kwaya ya shirikisho TMCS Dar Zone na Dona Jr.

Theme; Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu 1 Yohana 2:14

Usafiri kutoka na kurudi utakuwepo vyuo vyote. Maelezo zaidi piga 0719 131013

IMG-20190511-WA0010.jpeg
 
Naona uvccm munaandaa kikongamano chenu indirect
Imeandaliwa na Kanisa Katoliki kupitia umoja wa vyuo Karistimatiki Katoliki. Askofu mkuu mstaafu Mhashamu Josephat Lebulu atakuwepo pia.
 
Asante Mtumishi ,,tatizo lenu RC hamna nyimbo za kuabudu.
Si kweli zipo kwaya za Praise and worship kama ulivyoona kwenye tangazo. Hao Ebeneza praise and worship wana miaka zaidi ya 25 katika huduma. Karibu ushuhudie mwenyewe.
 
Back
Top Bottom