kutathimini biashara NPV, IRR, MIRR, DiscPBP na PI Je zinatumika mitaani ? ?

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Posts
1,092
Reaction score
1,118
Wakuu salama ? nimekuwa nikijiuliza zile mbinu za kutathimini miradi au biashara kama inalipa au la kama ville NPV, IRR, MIRR, PI, n.k wabongo mitaani zinatumika ? maana kila niki – test sioni mradi unalipa, na kama unalipa unakuta risk yake ni kubwa sana na hakuna sustanability tafadhali naomba maoni yenu kwa wale wanaozitumia na aina ipi ya miradi inakubali kwa hizo test.....
 

Mkuu na ndio maana matajiri wengi wa bongo hayo mambo hawayajui (lugha wanayoielewa wao ni practical, theory hawaielewi kabisa) ila ndio wana hela chafu. Wanaoyajua ndio woga umewajaa kiasi cha kushindwa kufanya kitu.

Ila ukimpata anaeyajua na akaamua kufanya biashara anakua kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuendesha biashara kisomi na ufanisi zaidi kiasi cha kuweka ushindani ngazi za kimataifa.
 
Mmmh...umenikumbusha hayo madude In Financial Management..
 
to be fair hizi formula zinatumika zaidi kwenye kampuni zinazo trade stock public. Kampuni nyingi sana Tanzania ni ndogo sana Mom & Pop shops ambazo zinaangalia dro kama inapesa au la!. Kwenye Mom and Pop shops the main focus is to make a profit while in corporation the main focus is to increase shareholders value. Hii inatofautisha sana approach za utendaji.
 
Kiukweli ukiangalia hayo mambo ya ma NPV sijui ma cost benefit analysis hutafanya biashara yoyote bongo. Cha ajabu sasa.. pale ambapo wewe unaona kabisa mahesabu yanaonyesha biashara hailipi, utashangaa mswahili anafungua hapo the same business na inamlipa! Cha maana we angalia uwepo wa wateja fungua kijiwe mambo mengine utapiga kimagumashi, kodi utakwepakwepa, mzigo utanunua kijanjajanja.. n.k mwishoni utapiga profit tuu unapeta..
 
Biashara za bongo hazina formula. Ili upate faida inabidi uchezeshe akili sana, kama kukwepa kulipa ushuru, kodi etc kulingana na aina ya biashara. Pia wakati mwingine inabidi uwabambike baadhi ya wateja na mambo mengine ya aina hiyo. Ila ukianza kukokotoa hizo mavitu hutakaa ufanye biashara.

Kwa biashara kubwa yenye mtaji kuanzia 100m unaweza kukokotoa irr, roi, npv etc. Na ni muhimu kufanya hivyo ili kupata picha ya mwenendo wa biashara na kuweka target za mauzo, minimum sales kwa mwezi ambazo hazitakupa hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…