Kutatua changamoto ya maji nchini

Kutatua changamoto ya maji nchini

Dibwi Method

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
31
Reaction score
28
March 11, 2022.

Mwenyekiti wa Taasisi ya ushirikiano uwekezaji katika sekta ya maji Kusini mwa Afrika (Global Water Partnership) ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete;

Benki ya Maendeleo ya Afrika imesema kwamba dola za Kimarekani bilioni 64 zitahitajika kila mwaka ili kufanikisha Dira ya Upatikanaji Maji Safi na salama Afrika kufikia mwaka 2025.

Lakini pia, ili kutatua shida ya maji, dola bilioni 30 zitapaswa kupelekwa kwenye miradi ya maji mpaka mwaka 2030 kwa upatikanaji wa maji safi na salama.

Mpaka sasa, michango kutoka kwa chi zote za Afrika pamoja na Wahisani kwenye sekta za maji barani Afrika, inakadiriwa kuwa dola bilioni 10 mpaka 19.

Ni wazi kwamba kuna pengo kubwa linalohitaji kuzibwa.
Mataifa ya Arika hayana budi kuamka na kuipa sekta ya maji kipaumbele kikuu kwani maji ni uhai.

MAONI

Zipangwe bajeti mahsusi kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kimkakati hasa nyakati hizi ambapo hali ya hewa haitabiliki na mvua zimekuwa haba sana.

Wahisani pia wanahimizwa kujitoa mara dufu na wawekeze zaidi kwenye miradi ya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama barani Afrika.

Nchi za Afrika hazina budi kuunda mifumo mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha michango yote pamoja na bajeti za maji zinafika mahala husika kwa nyakati sahihi zaidi.

Serikali ziwekeze zaidi kwenye tafiti ili yapatikane mawazo ya kibunifu, mapya na endelevu, yatakayosaidia kutengenezwa kwa miradi yenye tija na ya kisasa.

Miundo mbinu ya maji iboreshwe zaidi, yatengenezwe maghala ya kuhifadi maji kwenye ntyakati za mvua ili nyakati za ukame maji hayo yatumike kuhudumia wananchi na wahitaji wote wa maji.

Serikali ziachane na mawazo mgando kwa kujenga miradi ile ile ambayo imekuwepo toka enzi na enzi bila kuwa na msaada kifikapo kipindi cha ukame. Hamna haja ya kumimina mabilioni ya fedha kwenye miradi gumba isiyokuwa na tija kwa wananchi, mifano hai tunayo,

Tubadilike!
 
Back
Top Bottom