Kutegemea Kilimo kunashangaza MNO!!

Kutegemea Kilimo kunashangaza MNO!!

unazungumzia kilimo kipi mkuu ??? large scale ama small scale naona umebase kwenye small scale agr , zungumzia na large scale buddah .
acha kukaririsha
 
Wakuu,

Pamoja na ukweli kuwa kipato katika jamii kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, lipo jambo la kushangaa kila ninapowaona wakulima!! Haiingii akilini kuona kwamba, kuna waajiriwa ambao pia ni wajasiriamali wanaoishi hasa mijini, ambao mapato yao katika mwezi kwa wastani ni kati ya MILIONI MOJA mpaka MBILI. Hawa, katika Mwaka, wana uhakika wa kutengeneza kipato mpaka kufikia Milioni 12 au zaidi.

Lakini wengi kati ya hawa, wanalalamika kuwa MAISHA NI MAGUMU, MAISHA YAMEPANDA!!

Wala sipingani nao, hata mimi ni mmoja kati ya ambao kila kukicha nakiri, HERI YA JANA KULIKO LEO!!

Lakini ajabu ni kuwa, ninao NDUGU, JAMAA na MARAFIKI, ambao wanaishi Vijijini. Hawa, Shughuli pekee wanayoitegemea katika mwaka mzima ni KILIMO, tena CHA JEMBE LA MKONO..

Napata sana shida kujua, ni kwa namna gani watu hawa wanaweza kuuona tena kila MWAKA MPYA, au kuusubiri tena kila msimu wa kilimo huku WAKITEGEMEA KILIMO CHA JEMBE LA MKONO PEKE YAKE!!!

Tena basi misimu inatofautiana. Kuna misimu wanavuna sana, lakini kuna misimu inakuwa migumu kwao. Sasa fikiri mtu ambaye msimu umemwendea mrama, akauza vyote alivyopata, akapata MILIONI MBILI au wakati fulani pungufu ya hapo, tena kwa mbinde sana.. Mtu huyu anafikia vipi msimu unaofuata???

Lakini wakati mimi nawaza haya, Kuna mkulima wala halalamikii ugumu wa maisha pamoja na ukweli kuwa, kwa mtazamo wangu, namwona akiwa anakabiliwa na hali tete ya kiuchumi!!

Hii inanilazimu tu kukiri kuwa, KUTEGEMEA KILIMO PEKE YAKE KUNASHANGAZA MNO!!
Ulishaambiwa kuwa "Jembe halimtupi mkulima ".
 
Uchambuzi wako wa kiwango cha chini mkuu, kwani kijijini wanapanga nyumba?,wanasomesha international school?,wanalipa nauri kwenda kazini?,wanategemewa na ndg zao? Wananunua chakula? .kwa watu wa mjini wana matumizi makubwa kuzidi kijijini
 
Uchambuzi wako wa kiwango cha chini mkuu, kwani kijijini wanapanga nyumba?,wanasomesha international school?,wanalipa nauri kwenda kazini?,wanategemewa na ndg zao? Wananunua chakula? .kwa watu wa mjini wana matumizi makubwa kuzidi kijijini
Nisamehe sana kwa uchambuzi wa kiwango cha chini mkuu, Naahidi kutokurudia tena.. Walau nilitaka kujifunza, na bado nina lengo hilo.. Kuna misimu inakuwa mibaya Sana, mabadiliko ya hali ya hewa yanapotokea, wakulima WANAWEZAJE kuungoja msimu unaofuata?
 
Sasa hapa umekwenda mbali kwa wale walio na nafasi ya kuzifikia benki. Hasa nawalenga wale ambao TEGEMEO LAO NI JEMBE LA MKONO PEKE YAKE... Na ninachojiuliza.. Wanafanikiwaje kuungoja msimu mwingine wa kilimo hasa wanapopitia misimu migumu???
Hili swali nmekuwa nikijiuliza sana mpaka leo sojawahi kupata majibu
 
Na kwa kushangaza zaidi, wanayafurahia zaidi maisha yao ukilinganisha na wengine tunaokimbizana usiku na mchana kukuza vipato.. Ama kweli hili linashangaza...
ndio maisha mkuu, watu tunaolima tunaishi bila stress za boss
 
Unajua ni kwa nini wakulima tulio wengi Huwa tuachukulia hali hii POA?
Jibu ni kwamba katika kilimo Kuna KESHO TENA! ikiwa leo umekosa, basi KESHO UTAPA, yaani Hakuna mtu mwenye imani kama Mkulima. Na hiyo kesho akipata anapata Kweli kweli, wewe wa mjini unaweza tengeneza 12 per year yeye akaitengeneza hiyo 12M per 3 Months only so hiyo ndio Jeuri pekee alonayo Mkulima.
umeongea neno kubwa,,,, mkulima hio hela yake hapo chakula kala chake, kibanda chake,labda gharama ni maji na umeme......


hawa wenzetu wa ajira unasikia kodi ya nyumba,chakula anunue,nauli, bado wanapenda kuishi high life, etc etc ni lazima wapate stress.....


maisha ya ajira yana stress sn
 
Doh!! Umetandika msumari wa nguvu hapo!! Hili naliona kwa upana wake kabisa. Mjini toka kuamka Hadi kufumba jicho ni mwendo wa matumizi... Lakini Mimi ambacho kinanifikirisha ni kwamba, huyu wa "kuitwa mkulima wa kawaida", nguvu yake yote anaielekeza kwenye jembe, Tena la mkono.. Napata wakati mgumu Sana kuelewa "Ni kwa namna gani mtu huyu anaweza kuufikia msimu mwingine". Kwangu, pamoja na elimu pana kwenye mambo ya fedha, nauona ugumu mkubwa kikibadili kipato kidogo Cha msimu mzima kwenda kwenye matumizi ya mwaka mzima...
Samahani inaelekea hujawahi ishi kijijini...........


wengine wanasomesha watoto 6 mpk chuo kwa jembe la mkono, tena watoto wote hao unakuta wengine wapo private!
 
Samahani inaelekea hujawahi ishi kijijini...........


wengine wanasomesha watoto 6 mpk chuo kwa jembe la mkono, tena watoto wote hao unakuta wengine wapo private!
Mkuu, hili haswa ndilo linalonichanganya !!! INAWEZEKANAJE??? Mbinu Ipi inatumika kuwahudumia watoto 6 kwenye msimu unaokuwa mgumu, na usio na mazao ya kutosha? Mathalani, Kuna pahala nimewahi kufika, wanakwambia kwa misimu miwili mfululizo mambo hayakuwa mazuri.. Ni kipi kinawasaidia kuuona msimu mwingine baada ya msimu usio na mazao????
 
umeongea neno kubwa,,,, mkulima hio hela yake hapo chakula kala chake, kibanda chake,labda gharama ni maji na umeme......


hawa wenzetu wa ajira unasikia kodi ya nyumba,chakula anunue,nauli, bado wanapenda kuishi high life, etc etc ni lazima wapate stress.....


maisha ya ajira yana stress sn
Uko sawa kabisa, maisha ya kukinga mwisho wa mwezi kwakweli ni pasua kichwa... Lakini huyu ya "mwisho wa mwezi" ana walau uhakika wa vitu kama posho, salary advance, kukopa kwa akina"Mangi" na mengine.. MSIMU MMOJA UNAPOKUWA HAUNA MAVUNO, au yakapatikana ya chakula TU... Mkulima anawezaje kuungoja msimu unaokuja?
 
Back
Top Bottom