Kutegemea Kilimo kunashangaza MNO!!

unazungumzia kilimo kipi mkuu ??? large scale ama small scale naona umebase kwenye small scale agr , zungumzia na large scale buddah .
acha kukaririsha
 
Ulishaambiwa kuwa "Jembe halimtupi mkulima ".
 
Uchambuzi wako wa kiwango cha chini mkuu, kwani kijijini wanapanga nyumba?,wanasomesha international school?,wanalipa nauri kwenda kazini?,wanategemewa na ndg zao? Wananunua chakula? .kwa watu wa mjini wana matumizi makubwa kuzidi kijijini
 
Uchambuzi wako wa kiwango cha chini mkuu, kwani kijijini wanapanga nyumba?,wanasomesha international school?,wanalipa nauri kwenda kazini?,wanategemewa na ndg zao? Wananunua chakula? .kwa watu wa mjini wana matumizi makubwa kuzidi kijijini
Nisamehe sana kwa uchambuzi wa kiwango cha chini mkuu, Naahidi kutokurudia tena.. Walau nilitaka kujifunza, na bado nina lengo hilo.. Kuna misimu inakuwa mibaya Sana, mabadiliko ya hali ya hewa yanapotokea, wakulima WANAWEZAJE kuungoja msimu unaofuata?
 
Sasa hapa umekwenda mbali kwa wale walio na nafasi ya kuzifikia benki. Hasa nawalenga wale ambao TEGEMEO LAO NI JEMBE LA MKONO PEKE YAKE... Na ninachojiuliza.. Wanafanikiwaje kuungoja msimu mwingine wa kilimo hasa wanapopitia misimu migumu???
Hili swali nmekuwa nikijiuliza sana mpaka leo sojawahi kupata majibu
 
Na kwa kushangaza zaidi, wanayafurahia zaidi maisha yao ukilinganisha na wengine tunaokimbizana usiku na mchana kukuza vipato.. Ama kweli hili linashangaza...
ndio maisha mkuu, watu tunaolima tunaishi bila stress za boss
 
umeongea neno kubwa,,,, mkulima hio hela yake hapo chakula kala chake, kibanda chake,labda gharama ni maji na umeme......


hawa wenzetu wa ajira unasikia kodi ya nyumba,chakula anunue,nauli, bado wanapenda kuishi high life, etc etc ni lazima wapate stress.....


maisha ya ajira yana stress sn
 
Samahani inaelekea hujawahi ishi kijijini...........


wengine wanasomesha watoto 6 mpk chuo kwa jembe la mkono, tena watoto wote hao unakuta wengine wapo private!
 
Samahani inaelekea hujawahi ishi kijijini...........


wengine wanasomesha watoto 6 mpk chuo kwa jembe la mkono, tena watoto wote hao unakuta wengine wapo private!
Mkuu, hili haswa ndilo linalonichanganya !!! INAWEZEKANAJE??? Mbinu Ipi inatumika kuwahudumia watoto 6 kwenye msimu unaokuwa mgumu, na usio na mazao ya kutosha? Mathalani, Kuna pahala nimewahi kufika, wanakwambia kwa misimu miwili mfululizo mambo hayakuwa mazuri.. Ni kipi kinawasaidia kuuona msimu mwingine baada ya msimu usio na mazao????
 
Uko sawa kabisa, maisha ya kukinga mwisho wa mwezi kwakweli ni pasua kichwa... Lakini huyu ya "mwisho wa mwezi" ana walau uhakika wa vitu kama posho, salary advance, kukopa kwa akina"Mangi" na mengine.. MSIMU MMOJA UNAPOKUWA HAUNA MAVUNO, au yakapatikana ya chakula TU... Mkulima anawezaje kuungoja msimu unaokuja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…