Kutekeleza ilani: Nyumba 1500 za NSSF zilizokosa wanunuzi kupewa Vyuo vikuu

Bei za nyumba haziendani na thamani halisi ya soko, zilijengwa kwa gharama kubwa sana za kipigaji, zinatakiwa ziuzwe kwa gharama kubwa kitu ambaco hakiwezekani.

Mbongo anaona bora ajenge mwenyewe kwa gharama nafuu hata kama itakuwa kwenye squatter area.
Au anunue kiwanja kilichopimwa ajenge mwenyewe.
 
Hivi kuna mtu mwenye akili anunue nyumba hizo? Yaani akaishi KoTa. Full uswahili, wazipangishe bei kama zile za NHC zamani zile
 
Utashangaa Dr. Dau anasifiwa kwa miradi ya ujenzi kama hii.
Bado yule Nehemia wa NHC nae ndio walewale.
 
Unamaanisha AVIC TOWN?
 
Nyumba za kawaida sana bei kibwa mno. Walijenga bila akili for sure maana hata ukikopeshwa hazikopesheki watu wakaamua waingie mtaa wajenge wenyewe. Wizi tu huu pesa kibao ya govt imepotea
Pesa za wafanyakazi sio za serikali.wafanyakazi ndio pesa zao hufanyiwa uwekezaji bila ya wao kushirikishwa,mwisho wa siku miradi isipolipa ndio zinakuja zile sheria kandamizi za "mafao yenu mpaka mkikaribia kufa".
 
Nyumba za kawaida sana bei kibwa mno. Walijenga bila akili for sure maana hata ukikopeshwa hazikopesheki watu wakaamua waingie mtaa wajenge wenyewe. Wizi tu huu pesa kibao ya govt imepotea
Siyo pesa ya govt ni michango ya wafanyakazi hiyoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…