Bendera Esq
Member
- Dec 16, 2024
- 17
- 64
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuwa na uelewa sahihi wa kisheria kuhusiana na swala la kutembea (kufanya mapenzi) na mwanafunzi. Kwenye sheria za Tanzania, hakuna kosa la kutembea (kufanya mapenzi) na mwanafunzi. Ili jambo liwe kosa kisheria ni lazima kuwe na sheria inayopiga marufuku kutenda jambo hilo na kutamka wazi kuwa ukilitenda unakuwa umetenda kosa la jinai. Hii ni kanuni ya kikatiba ambayo inapatikana kwenye ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Yafuatayo ni makosa mawili ambayo watu wamekuwa wakijichanganya na kudhani kuwa kinachopigwa marufuku ni kutembea na mwanafunzi.
1. KUTEMBEA NA MSICHANA ALIYE CHINI YA UMRI WA MIAKA 18
Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania) kwenye kifungu cha 130(1) inakataza kutenda kosa la ubakaji dhidi ya mwanamke au msichana. Kifungu hicho cha 130(2) kinaeleza mazingira tofauti ambayo kwayo mwanaume akifanya mapenzi na mwanamke au msichana, mwanaume huyo anakuwa amebaka. Moja kati ya mazingira hayo ni kutembea na mwanamke bila ridhaa yake kama vile kwa kutumia nguvu. Mazingira mengine yanayotajwa kwenye kifungu cha 130(2)(e) ni kutembea na msichana aliye chini ya umri wa miaka 18. Hivyo, ukitembea na msichana wa miaka 17, 16, 15 au chini ya hapo unakuwa umebaka hata kama ni yeye mwenyewe aliutaka. Kigezo cha kuzingatia ni umri. Awe mwanafunzi, asiwe mwanafunzi; Ukimla binti wa chini ya miaka 18 umebaka.
2. KUMUOA AU KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI
Sheria ya Elimu (Sura 353 ya Sheria za Tanzania) chini ya kifungu cha 60A kama kilivyofanyiwa marekebisho na Sheria na 2 ya mwaka 2016 kinapiga marufuku kumuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari. Hivyo, bila kujali umri alio nao; Ukimuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi unakuwa umetenda kosa chini ya Sheria ya Elimu.
***
ZINGATIA
Ukitembea na msichana wa kidato cha 5 mwenye umri wa miaka 17 utashtakia kwa kosa la ubakaji chini ya Kanuni ya Adhabu. Unashtakiwa sio kwa sababu umetembea na mwanafunzi. La Hasha! Unashtakiwa kwa sababu ya umri wa huyo msichana. Umebaka! Adhabu yake inaanzia miaka 30 jela mpaka kifungo cha maisha.
Lakini ukitembea na mwanafunzi wa sekondari mwenye miaka 18 au zaidi huna kosa lolote. Ila hakikisha usimpe ujauzito. Akipata ujauzito utashtakiwa kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi kinyume na Sheria ya Elimu. Adhabu yake ni miaka 30 jela.
Ikitokea umetembea na mwanafunzi wa umri wa miaka 17, 16 au chini ya hapo na ukampa ujauzito basi utashtakiwa kwa makosa mawili. Kosa la kwanza ni ubakaji (sababu ya umri) na la pili ni kosa kumpa ujauzito mwanafunzi.
USHAURI
Usitembee kabisa na msichana wa chini ya miaka 18. Ni ubakaji. Awe anasoma au hasomi.
Usimpe ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari hata kama ana miaka 18 au zaidi. Ni kosa chini ya Sheria ya Elimu.
IMEANDIKWA NA;
Bendera Esq (Wakili)
Instagram: sheriaweb
Mobile : 0619008857