flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,860
- 6,390
Jana nikiwa kazini nikawaza 'Nina siku sijaenda kumsalimia bibi, sijui lini niende' Duh aisee nikakumbuka alishafariki mwaka huu miezi yamwanzoni kabisa.
Bibi yangu alinipenda sana nayeye ndie kwa asilimia kubwa alinilea. Jana hiyo nilijikuta machozi yananitiririka kazini maana nilimkumbuka. Nilikuwa nikikaa kimya bila yakwenda kumuona basi alipita kazini kwangu kuniulizia na kunijulia hali kwa madai kuwa kwenye simu haitoshi . Ila leo hii simuoni ndugu yangu yoyote anayenikumbuka hata kwa simu.
Ndugu akinipigia simu basi ujue ananitolea shida fulani. Toka bibi yangu afariki sijaona ndugu mwingine wakuja kuniulizia kazini. Hakika bibi yangu ulinipenda sanaaa....
Nilimzoea bibi yangu maana nilikuwa hata nikipata changamoto yoyote iwe kiafya au kikazi hata kimahusiano basi nilifunga safari kwenda kumueleza na hakika alikuwa ananipa nguvu sana, alikuwa ananiliwaza sana na kuniombea.
Jana hiyo kiukweli nilifunga safari mpaka makaburini nikapiga goti nakuomba huku machozi yakinitoka. Yaani nilijikuta nikilia sana juu ya kaburi nikiwa peke angu. Sijui kama huko alipo aliniona ila ipo hivyo. Upendo wa bibi juu yangu ni zaidi ya upendo wababa hakika.
Nakumbuka kuna kipindi niliitwa nyumbani kwamadai eti nimetafutiwa mchumba kitu ambacho sikukubaliana nacho ila bibi yangu alisimama upande wangu na kunitetea huku akifoka kuwa nisilazimishwe kitu ambacho sikubaliani nacho na hakika walimuelewa. Hakika bibi ulinipenda sana.
Sikuwahi kusikia wala kuhadithiwa kuwa ulishawahi nisema vibaya au kuniteta. Aisee bibi ulinipenda sanaaaa kuliko mimi nilivyokupenda.
Kuna kipindi nilipitia magumu fulani ila yale magumu yalikuwa kama yakwako maana ulipata mawazo sana nahata watu walikuwa wakikuuliza nini tatizo basi uliwajibu 'unamuomba sana Mungu mjukuu wangu flulanga awe na maisha mazuri yenye amani yeye na familia yake' ndicho ulichowajibu hicho. Pumzika kwa amani bibi yangu mpendwa.
Mimi kwenda kaburini nakulia machozi, naweza kuwa nilifanya makosa au naweza kuwa nimekufuru?