Kutembelea, kulia kwenye kaburi la ndugu kuna ubaya?

The best Uzi,,, toka nimefiwa na wanangu wawili na baba yangu mzazi makaburi ni part ya maisha yangu yaaani nikihisi upweke huzuni muda wowote basi nnaenda zangu juu ya kaburi nalia naongea mpka kifua kinasinyaa na nikijihisi kulala nalala mpk nachoka then taratibu natoka nikiwa fresh kabisa

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Pole aiseee inafikirisha sanaaa kilichobaki tuishi nawapendwa wetu katika mioyo yetu
 
MHU. :9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Kuna Kitabu cha wamakabayo ambacho katika biblia yenye vitabu 72 kipo...wewe unatumia biblia yenye vitabu 66.
 
Jana nikiwa kazini nikawaza 'Nina siku sijaenda kumsalimia bibi, sijui lini niende' Duh aisee nikakumbuka alishafariki mwaka huu miezi yamwanzoni kabisa.

Bibi yangu alinipenda sana nayeye ndie kwa asilimia kubwa alinilea. Jana hiyo nilijikuta machozi yananitiririka kazini maana nilimkumbuka. Nilikuwa nikikaa kimya bila yakwenda kumuona basi alipita kazini kwangu kuniulizia na kunijulia hali kwa madai kuwa kwenye simu haitoshi . Ila leo hii simuoni ndugu yangu yoyote anayenikumbuka hata kwa simu.

Ndugu akinipigia simu basi ujue ananitolea shida fulani. Toka bibi yangu afariki sijaona ndugu mwingine wakuja kuniulizia kazini. Hakika bibi yangu ulinipenda sanaaa....

Nilimzoea bibi yangu maana nilikuwa hata nikipata changamoto yoyote iwe kiafya au kikazi hata kimahusiano basi nilifunga safari kwenda kumueleza na hakika alikuwa ananipa nguvu sana, alikuwa ananiliwaza sana na kuniombea.

Jana hiyo kiukweli nilifunga safari mpaka makaburini nikapiga goti nakuomba huku machozi yakinitoka. Yaani nilijikuta nikilia sana juu ya kaburi nikiwa peke angu. Sijui kama huko alipo aliniona ila ipo hivyo. Upendo wa bibi juu yangu ni zaidi ya upendo wababa hakika.

Nakumbuka kuna kipindi niliitwa nyumbani kwamadai eti nimetafutiwa mchumba kitu ambacho sikukubaliana nacho ila bibi yangu alisimama upande wangu na kunitetea huku akifoka kuwa nisilazimishwe kitu ambacho sikubaliani nacho na hakika walimuelewa. Hakika bibi ulinipenda sana.

Sikuwahi kusikia wala kuhadithiwa kuwa ulishawahi nisema vibaya au kuniteta. Aisee bibi ulinipenda sanaaaa kuliko mimi nilivyokupenda.

Kuna kipindi nilipitia magumu fulani ila yale magumu yalikuwa kama yakwako maana ulipata mawazo sana nahata watu walikuwa wakikuuliza nini tatizo basi uliwajibu 'unamuomba sana Mungu mjukuu wangu flulanga awe na maisha mazuri yenye amani yeye na familia yake' ndicho ulichowajibu hicho. Pumzika kwa amani bibi yangu mpendwa.

Mimi kwenda kaburini nakulia machozi, naweza kuwa nilifanya makosa au naweza kuwa nimekufuru?
Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwaambia Masahaba: "Watuzeni maiti wenu? Wakauliza, "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu tuwatuze nini maiti?" Akajibu Sadaka na Dua, tena akaendelea kusema, "Hakika roho za wenye imani siku ya Ijumaa kwenye mbingu ya kwanza sawa na mahala walipokuwa wakikaa majumba yao na kila mmoja wao hupiga kelele kwa sauti ya kuhunisha na kulia na husema, Enyi watu wangu, watoto wangu, baba na mama yangu na majamaa zangu, tuonee huruma na Mwenyezi Mungu Atakuoneeni huruma, kwa mali hiyo mliyo nayo ilikuwa mikononi mwetu, sasa haipo mikononi mwetu, mateso na hesabu tunafanyiwa sisi na faida yake wanafaidi wengine". Na kilamoja (roho) humpigia kelele jamaa zake.
Tuonee huruma kwa kutoa sadaka 'dirham' moja (pesa za zama zile) au kwa kutoa mkate kumpa maskini, au kwa nguo kumvisha asiekuwa na nguo, na Mwenyezi Mungu atakuvisheni nguo za "Janah" (Pepo). Baadaye Mtukufu Mtume (s.a.w) akalia na Masahaba pia wakalia, na kilio kilimshika kwa wingi hata hakuweza kusema. Baadaye akasema "Hao ni ndugu zenu katika dini (Imani) sasa wameshageuka udongo na mifupa imesagika baada ya kuishi humu duniani kwa raha na furaha, basi wanapiga kelele na kusema, "Ole juu yetu, laiti katika uhai wetu tungali toa sadaka na kutenda mazuri kwa (pesa zetu) hizo tulizokuwanazo katika njia ya Mwenyezi Mungu leo tusengelikuwa muhutaji wenu". Basi wanarudi wanyonge na huku wanpiga kelele, "Haraka toeni Sadaka kwa maiti wenu".
Inafaa kwa Mwislamu kila wiki kwa uchache hasa siku AIhamisi awakumbuke wafu wake kwa kufika kwenye makaburi yao, hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) akiwaamrisha Masahaba wake kuzuru makaburi.
Amepokea Bi Aisha (R.A.) na Abu Hurayrah (R. A.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) amesema, "Amekuja Jibrili kwangu na akaniambia kwamba "Mola wako Anakuamrisha uende kwa watu wa 'AL-BAQEE' makaburini mwa watu wa Madina na uwaombee waghufuriwe". Nikasema (Aisha), "niseme nini ninapofika makaburini?" Akasema, Sema, "AS-SALAA-MU ALAA AHLID-DIYAAR, MINAL MU'MINEE-NA- WAL MUS-LIMEEN. YARHAM UL-LAA-HUL MUSTAK-DIMEE-NA-MIN-NAA, WAL MUS-TA'A-KHIREEN, WA IN-NAA IN-SHAA-AL-LAAHU Bl-KUM, LAA-HI KUUN.
Licha ya kuwepo wapokezi wa hadithi kuhusu jambo hilo kutokana na wanachuoni, wa Ki-Shia vile vile wamepokea hadith hizo wanachuoni wa Ki-Sunni nao ni: Bwana Muslim katika Saheeh yake, na Bwana Bayhaki katika 'Sunan' yake na pia Bwana Ahmad Bin Hambal, Bwana Abudaud, Bwana Tirmizi, Bwana Nasaina Bwana Baghawi.
Ni sunna unapofika kwenye kaburi uelekee Qibla, weka mkono kwenye hilo kaburi na soma mara saba (7) sura ya Innaa Anzalnahu (5:97) na pia bora usome sura ya AL-FAATlHA (S:1) na sura ya AL-FALAQ (5:113) na WAN-NASI (S:114) na sura ya QUL-HUWL-LAAHU (S:112) na Ayatul-Kursi kila moja mara tatu.
Ni sunna unapoingia makaburini usome:
"BlS-MIL-LAA-HIR-RAH-MAA-NIR RAHEEM, ASSALAA-MU ALAA AHLI LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, MIN AH-LI LAA-ILAA-HA IL-LAL LAAHI YAA AH-LA LAA-Llaa-HA, IL-LAL-LAAH, BI-HAK-KI- LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, KAY-FA WAJAD-TUM KAULA LAA-ILAA-HA-IL-LAL-LAAH MIN LAA ILAA-HA IL-LAL-LAAH, YAA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH, BI HAK-KI LA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, IGH-FIR LIMAN KAA-LA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH WAH-SHUR NAA, FIY ZUM-RATI MAN KAA-LA, LAA-ILAA HA IL-LAL-LAA-HU, MUHAM-MADUN RASUU-LUL-LAAH ALY-YUN WALIY-YUL-LAAH
Kwa kusoma haya Mwenyezi Mungu atambarikia msomaji thawabu ya kutenda mema ya miaka hamsini na kumsamehe madhambi yake na ya wazazi wake ya miaka hamsini.
Tunaomba kwa Mola Atupe tawfiki ya kuwakumbuka wafu wetu hasa wazazi kwa kuwatendea mambo ya heri kwa thawabu yao na kuwazuru makaburini kwa kuwa somea Fatha Amin. Na kwa kuzuru makaburi tutakumbuka kuwa kuna kufa (mauti), hao
 
Inshaaallah Mungu akubariki
 
Mtu anapofariki ni roho kuachana na mwili tunazika mwili wa mpendwa wetu sio roho yake baada ya hapo mwili tuliozika haujui chochote, kamwe roho haifi na haitakufa
 
Si
Jana nikiwa kazini nikawaza 'Nina siku sijaenda kumsalimia bibi, sijui lini niende' Duh aisee nikakumbuka alishafariki mwaka huu miezi yamwanzoni kabisa.

Bibi yangu alinipenda sana nayeye ndie kwa asilimia kubwa alinilea. Jana hiyo nilijikuta machozi yananitiririka kazini maana nilimkumbuka. Nilikuwa nikikaa kimya bila yakwenda kumuona basi alipita kazini kwangu kuniulizia na kunijulia hali kwa madai kuwa kwenye simu haitoshi . Ila leo hii simuoni ndugu yangu yoyote anayenikumbuka hata kwa simu.

Ndugu akinipigia simu basi ujue ananitolea shida fulani. Toka bibi yangu afariki sijaona ndugu mwingine wakuja kuniulizia kazini. Hakika bibi yangu ulinipenda sanaaa....

Nilimzoea bibi yangu maana nilikuwa hata nikipata changamoto yoyote iwe kiafya au kikazi hata kimahusiano basi nilifunga safari kwenda kumueleza na hakika alikuwa ananipa nguvu sana, alikuwa ananiliwaza sana na kuniombea.

Jana hiyo kiukweli nilifunga safari mpaka makaburini nikapiga goti nakuomba huku machozi yakinitoka. Yaani nilijikuta nikilia sana juu ya kaburi nikiwa peke angu. Sijui kama huko alipo aliniona ila ipo hivyo. Upendo wa bibi juu yangu ni zaidi ya upendo wababa hakika.

Nakumbuka kuna kipindi niliitwa nyumbani kwamadai eti nimetafutiwa mchumba kitu ambacho sikukubaliana nacho ila bibi yangu alisimama upande wangu na kunitetea huku akifoka kuwa nisilazimishwe kitu ambacho sikubaliani nacho na hakika walimuelewa. Hakika bibi ulinipenda sana.

Sikuwahi kusikia wala kuhadithiwa kuwa ulishawahi nisema vibaya au kuniteta. Aisee bibi ulinipenda sanaaaa kuliko mimi nilivyokupenda.

Kuna kipindi nilipitia magumu fulani ila yale magumu yalikuwa kama yakwako maana ulipata mawazo sana nahata watu walikuwa wakikuuliza nini tatizo basi uliwajibu 'unamuomba sana Mungu mjukuu wangu flulanga awe na maisha mazuri yenye amani yeye na familia yake' ndicho ulichowajibu hicho. Pumzika kwa amani bibi yangu mpendwa.

Mimi kwenda kaburini nakulia machozi, naweza kuwa nilifanya makosa au naweza kuwa nimekufuru
Hukulia alipokufa?
 
Back
Top Bottom