Kutendwa kumeniondolea hamu ya kuingia kwenye mahusiano

Handsome boy 1

Senior Member
Joined
Jun 2, 2021
Posts
105
Reaction score
142
Mimi ni kijana wa miaka 26 nilikuwa na mpenzi wangu tuliyedumu kwa miaka 2 nolimpenda sana ila yeye aliniektia.

Tuliishi nikijua lengo la mahusiano yetu ni kuoana nilijitoa kwake kwa kiasi kikubwa sana lakini mwaka huu kwa masikitiko makubwa tukaachana maumivu niliyapata ofcourse mana sikutegemea kama tungeachana na ni mwanamke niliyemtegemea sana kuoana naye.

Nimekubali kuachana naye ila akili haisomi bado yan hata wale nlopita nao before nmejikuta sina mzuka nao naona afadhali nibaki tu alone nitafute tu maisha kwanza sina mzuka kabisa na mahusiano najiona mtu wa tofauti sana yani.

Naona afadhali nikae pembeni nifanye kazi zangu tu nijipatie kipato af mapenzi basi.
 
Yaani vitoto vya miaka.24-29 MNA TUCHEFUA SAANAAAA

Hivi huu umri waweza sema ume tendwa au ni utoto utoto wa kishule shule na chuo chuo ndio MNAITA MAPENZI???
JamiiForums-2020578957.jpg
 
Kwa kweli sina mahusiano maana nilijikuta niko na maumivu ambayo sikuyaekewa yanatokea wapi, Kumbe nilikua Kwenye mahusiano ambayo mimi ndio nayapigania halafu mwenzangu ananichukulia powa,Tulipoachana maumivu yameisha na sitamani kitu inaitwa mahusiano.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni kijana wa miaka 26 nilikuwa na mpenzi wangu tuliyedumu kwa miaka 2 nolimpenda sana ila yeye aliniektia.

Tuliishi nikijua lengo la mahusiano yetu ni kuoana nilijitoa kwake kwa kiasi kikubwa sana lakini mwaka huu kwa masikitiko makubwa tukaachana maumivu niliyapata ofcourse mana sikutegemea kama tungeachana na ni mwanamke niliyemtegemea sana kuoana naye.

Nimekubali kuachana naye ila akili haisomi bado yan hata wale nlopita nao before nmejikuta sina mzuka nao naona afadhali nibaki tu alone nitafute tu maisha kwanza sina mzuka kabisa na mahusiano najiona mtu wa tofauti sana yani.

Naona afadhali nikae pembeni nifanye kazi zangu tu nijipatie kipato af mapenzi basi.
umri bado ni mdogo sana ku give up now. jijenge kwanza kimaisha then mke atakuja mwenyewe
 
Acha hizo, tafuta mtoto mzuri mwenye sifa unazopenda kama ni chura, chukua mtoto mwenye chura ya maana mpende, yani penda kama vile haujawahi kupenda.
 
Kuna vitu vitatu hapo,wewe mpenzi wako na mahusiano yenu,kilichofeli ni mahusiano yenu sio wewe au yeye.Usiichukulie ni kushindwa kwako,kinachoumiza ni matarajio yako tu yameshindwa kutimia,with time utakuwa sawa.Pia labda umejaa lawama sana juu yake na kuona kakuonea sana,unasahau kuwa kama ni aliyeshindwa kujua kuwa alikuwa ni sahihi kwako au lah ni wewe.Hivyo kubali kuwajibika kwa kutokuweza kujua usahihi wa mwenza wako kwako,jifunze hilo ili usirudie tena,kubali maumivu,na songa mbele.Na kumbuka sote ni wahanga wa haya mambo katika nyakati na mazingira tofauti,wewe si wa kwanza na wala hutokua wa mwisho.
 
Dah aisee umenitia moyo sana nashukuru sana ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom