MAMESHO
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 1,432
- 1,738
Kutenganisha taka kutarahisisha urejelezaji na ushughulikiaji salama wa taka ili kuokoa mazingira
Taka ni tatizo kubwa. kila mwaka kuna kiwango kikubwa cha taka kinaingia katika mazingira. Hali hii inaleta athari kubwa kwa viumbe pamoja na mimea duniani. Kwa mfano karatasi za nailoni zinazosambaa baharini na kwenye maeneo yenye maji huleta athari kubwa sana kwa mimea na viumbe ambavyo huishi kwenye mazingira hayo pamoja na mazalia yake.
Hivyo ili mazingira yasiathirike ni muhimu sana kuwa na namna ya kurejeleza takataka kuwa malighafi au kuweza kuzalisha bidhaa zingine ili kupunguza athari kwenye mazingira. Chupa zilizotumika za kioo, za plastiki, mifuko ya sandarusi, maboksi, vyuma, mabati, betri zilizotumika, taka zitokanazo na mabaki ya vyakula na taka zinginezo ni vyema zikahifadhiwa vyema au kuteketezwa kwa namna ambayo itayaacha mazingira kubaki salama.
Kwa bahati mbaya, suala hili halijapewa kipaumbele na bajeti ya kutosha, kuelimisha na kuweza kuweka miundombinu rafiki ya kufanya kazi hii. Wengi mtakuwa mashahidi jinsi ukusanyaji, uhifadhi na ubebabaji wa taka unavyoleta kero. Harufu kali kusambaa, uchafu unavyochuruzika na kumwaga maji machafu barabarani wakati wa ubebaji.
Inasikitisha kwamba bado wanaotoa huduma hizo hawajaelimishwa kuhusu vifaa vya kuwakinga na namna ya kuvitumia kwa usahihi. Jambo ambalo linahatarisha afya za wanaofanya kazi hizo. Kazi hizi zinafanyika pasipo kufuata miongozo na taratibu husika.
Sheria inawataka wafanyabiashara kuzingiatia, Kuweka taka sehemu salama, Kuweka taka kwenye vyombo ambavyo vitazuia uchafu kutapakaa. Kwa zile biashara ambazo zina husika na taka hatarishi wana jukumu kubwa la kutenganisha na kuhifadhi vyema kwa mfano kemikali, vifaa vya umeme, betri za aina zote ili ziweze kurejelezwa au kuharibiwa bila kuleta athari kubwa kwenye mazingira.
Sheria za miji pia zianaelekeza wakazi kuchangia huduma ya uondoshaji wa taka kwa viwango maalumu ambavyo vimepangwa. Kwa wanaokaidi agizo hilo hatua za kisheria zianchukuliwa. Pia zipo sheria ndogo ndogo za miji ambazo zinasaidia katika utunzaji wa mazingira. Endapo mwananchi atazivunja itamlazimu kulipia au kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.
Kwanini ni muhimu kutenganisha taka?
Umuhimu wa kutenganisha taka ni kurahisiha urejelezaji wa taka na kutumia njia sahihi ya kuziharibu ili zisilete athari kwa mazingira. Kushindwa kutenganisha taka husababisha taka kuchanganyikana na hivyo kuishia kwenye ardhi. Unapochanganya taka wakati wa kuziharibu kwenye tanuru hutoa hewa yenye kamikali mmchanganyiko na kuchafua hali ya hewa.
Taka zitokanazo na eneo la ujenzi zinaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kwa mfano kundi moja matofali chakavu, sakafu na marumaru kundi la pili mbao vioo fremu na plastiki kundi la tatu chuma pamoja na nyaya, kundi la nne udongo pamoja na kifusi. Kwa vile vitu ambavyo vitafaa vitu viterejelezwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi kwa wenye uhitaji kununua au kuona namna sahihi ya kuvitumia kwa namna ambayo hakutakuwa na madhara kwenye mazingira.
Taka zitokanazo na vifaa vya magari pamoja na oili chafu. Kwa mafano matairi, shockup, diski za breki na betri vinaweza kurejelezwa viwandani. vimiminika kama oili za injini na vilainishi vya gia na vinginevyo vinaweza kuhifadhiwa kwenye vyombo imara na kuuzwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa nyingine kama vile dawa za wadudu na bidhaa nyinginezo.
Taka zitokanazo na vifaa vya umeme. Taka aina hii inaweza kuwa kama vile; Runinga za zamani, kompyuta mpakato, mashine za kufulia, nyaya mbalimbali, majiko ya umeme, taa zilizoungua pamoja na betri aina mbali mbali zilizokwisha matumizi.
Taka zitokanazo na vifungashio. Taka hizi zinaweza kuwa chupa za maziwa, makopo ya siagi, makaratasi ya pipi, biskuti , karatasi za mikate, magazeti, maboksi na chupa za mvinyo. Kwenye taka hizi unaweza kuwa na vyombo tofauti ni vyema ukatenganisha maboksi, chupa, na karatasi za nailoni.
Taka zitokanazo na matibabu au huduma za kiafya. Taka hizi hutolewa maelekezo maalumu ya namna ya kuziteketeza na kufuatiliwa na wakaguzi wa huduma za afya. Umakini unahitajika sana kunapokuwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na Uviko. Vifaa kama barakoa, nepi na bandeji za vidonda huteketezwa kwa utaratibu maalumu.
Taka zitokanazo na vyakula vilivyoharibika. Hapa namaanisha uchafu utokao masokoni kutokana na mabaki au mazao yaliyoharibika, uchafu wa mabaki ya vyakula wa hotelini na majumbani, mabucha ya nyama na machinjioni. Taka hizi ni zile zinazooza hivyo zinaweza kutengeneza bidhaa kama mbolea asili au kupelekwa mbali na makazi ya watu kwa lengo la kuharibu taka hizo.
Ni dhahiri kuwa kazi hii inaweza kufanyika kwa weledi na tija ili iwe na faida kubwa kwa nchi yetu. Kwa njia hii miradi mbali mbali inayoweza kutumia taka hizo inaweza kuanzishwa na kuwa na manufaa. Mfano mzuri ni mradi ambao uliweza kutumia taka zitokanazo na zao la katani kuzalisha umeme.
Vilevile, tunaweza kutumia wataalamu tulionao katika namna ya kurejeleza au kutumia taka hizi kuweza kutushauri Zaidi ili kupunguza au kuondoa kabisa athari zinazoletwa na taka katika mazingira.
Natoa shukrani kwako kwa kuweza kusoma andiko hili. Niombe utoe mawazo yako tuweze kuboresha maisha yetu, afya zetu, taifa letu na uchumi wetu.
Kielelezo kuonyesha namna ambavyo taka zinaweza kutenganishwa. Mfumo huu unaweza kutumika wakati wa ukusanyaji. Chanzo halisi cha mchoro ni mtandao wa istock. (istockphoto 909111180)

Attachments
Upvote
7