Yapata wiki sasa nahangaika na tatizo la Kuku kuvimba macho na kuwa vipofu kabisaa mpaka sasa ni Kuku 22 ndio wamepatwa na tatizo hilo, nimewahamisha banda kabisa ili wasichangamane na Kuku wengine wakaleta maafa zaidi nimeshajaribu kutumia antibiotics mbali mbali kama Piperazine citrate, sevin , Akheri powder kuwatibu lakini wapi yaani tatizo liko palepale kinachoniumiza zaidi hawa Kuku walishaanza kutaga na wengine ndio wanaelekea kuanza kutaga.
Kama kuna wataalamu humu naomba msaada wa cha kufanya maana mambo yanakua magumu sasa,hii ndio biashara pekee ambayo hakika haikuwahi kuniangusha sasa kama nitaanguka kwenye hii Nayo miti yote itakua inateleza kwangu hivyo chini nitaanguka