Kuteuliwa kwa Dkt. Nchimbi: Rais Samia sasa kunywa chai yako kwa raha zako

Kuteuliwa kwa Dkt. Nchimbi: Rais Samia sasa kunywa chai yako kwa raha zako

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Kuteuliwa kwa Dr. Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama ni turufu kubwa sana, chama kimerudi mikononi mwa wenyenacho, wenye uchungu nacho, ambao hawategemewi kuezua nyasi ili nyumba ivuje.

Mtu mwenye tamaa ya kuiona Tanzania inaendelea kung'ara na kuwa kielelezo cha Amani na mshikamano, mtu ambaye hategemewi kuona muungano unateteleka, mtu ambaye hawezi kuvuka mto bila kupima mto kwa kijiti, kwa ufupi wewe kunywa chai yako kwa raha zako chaguzi zote na zile za uchaguzi mkuu ni Mseleleko.
 
Yani akili ccm zipo kwenye vyeo, pamoja na matatizo nchi iliyonayo bado waona ni mda wa Samia kunywa chai, kwamba kwake chama na madaraka ndo kila kila kitu kuliko shida za watanzani.

Kwa nchi ilipofikia kama Rais anawezaje kunywa chai kwa kunyosha miguu
 
Kuteuliwa kwa Dr Nchimbi kuwa Katibu mkuu wa chama ni turufu kubwa sana, chama kimerudi mikononi mwa wenyenacho, wenye uchungu nacho, ambao hawategemewi kuezua nyasi ili nyumba ivuje, mtu mwenye tamaa ya Kuiona Tanzania inaendelea kugh'ara na kuwa kielelezo cha Amani na mshikamano, Mtu ambaye hategemewi kuona muungano unateteleka, mtu ambaye hawezi kuvuka mto bila kupima mto kwa kijiti, kwa ufupi wewe kunywa chai yako kwa raha zako chaguzi zote na zile za uchaguzi mkuu ni Mseleleko.
Edit jina lake ni Emmanuel John Nchimbi. Chimbi umelipata wapi?
 
Mungu akujaalie utembelee majirani zetu wote wa EA, nina hakika utajifunza mengi na utajipiga kifua kwamba sisi tuko vizuri, maandamano ya Waganda (kwa mfano) kuamua kupanda migomba barabarani, kuishinikiza serikali itengeneze barabara ambayo ni mahandaki ya mashimo imeiona wapi Tz. !!! wewe ndo wale mnaotamani kande kwa kukinahiwa na pilau.
 
kwani si haki yake kama Mtanzania hata wewe jiandae 2030, 2025 Mama Samia ametoheleza vigezo na masharti tunakwenda naye hadi 2030 Inshallah.
 
Nasubiri apige MARUFUKU makada wa ngazi zote walioanza compaign kabla ya muda.
 
Kikwete ofisi za ccm na serikali tusahau kustaafu amestafu kiutendaji kwenye makaratasi kiutendaji yumo

Nchimbi kijana wake kazi maalum enzi na enzi
 
Nasubiri apige MARUFUKU makada wa ngazi zote walioanza compaign kabla ya muda.
Hapo kwa 'ngazi zote' sio sahihi 😂😂. Kuna ngazi moja lazima iwahi ili iwaonye ngazi ya chini yake kuwa mchujo utaangalia kazi walizofanya kwenye chama na hivyo wafanye kazi za chama.
 
Kikwete ofisi za ccm na serikali tusahau kustaafu amestafu kiutendaji kwenye makaratasi kiutendaji yumo

Nchimbi kijana wake kazi maalum enzi na enzi
Jamani,hampendi amani. Mama huyu Kina Kirefu asikunyime amani. Kazi maalum na wenyewe wawekee kazi maalum. Principle ni ile ile you trust no one. Hii nchi ngumu sana.
 
Kuimba kupokezana, walioshangilia mwamba akiwekwa mbali na mfumo enzi ya jiwe, sasa wanaimba wimbo wao.

Nchimbi "awafyeke" kisiasa taratibu lakini kwa uhakika. Dotto James alikuwa anamcheleweshea malipo yale akiwa Balozi Brazil ili kumkomesha, na yeye sasa akomeshwe, kwa kuwa alifanya kwa makusudi.

Kisasi kwenye siasa ni sunna
 
Kuteuliwa kwa Dr. Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama ni turufu kubwa sana, chama kimerudi mikononi mwa wenyenacho, wenye uchungu nacho, ambao hawategemewi kuezua nyasi ili nyumba ivuje.

Mtu mwenye tamaa ya kuiona Tanzania inaendelea kung'ara na kuwa kielelezo cha Amani na mshikamano, mtu ambaye hategemewi kuona muungano unateteleka, mtu ambaye hawezi kuvuka mto bila kupima mto kwa kijiti, kwa ufupi wewe kunywa chai yako kwa raha zako chaguzi zote na zile za uchaguzi mkuu ni Mseleleko.
CCM iko strong na very comfortable this time around. Ina uhakika wa kila kitu, kila idara kila sehemu 🐒
 
Back
Top Bottom