KateMiddleton
JF-Expert Member
- Mar 15, 2021
- 3,883
- 4,676
Usingekubali utumishi wa ummaTatizo watu wanaendekeza umasikini.
Kuna watu wana wito wa ualimu, hawana wito wa Ukuu wa Wilaya.
Ukiwateua kazi ambayo hawana wito nayo umewaharibia mipango yao.
Yani, kitu cha msingi ni maelewano.
Ukiteuliwa kazi bila hata kuulizwa, umedharauliwa.
Umeonekana kwamba wewe huna maoni katika uamuzi huo.
Wewe ni mtu wa kupangiwa tu.
Hapana,Usingekubali utumishi wa umma
Kakae sekta binafsi ujipangie maisha
Hapa sasa mtaona ukubwa wa madaraka ya RaisHapana,
Kwani hata hiyo kazi ya sasa ya utumishi wa umma mtu hana haki ya kuacha?
Kama mtu ana haki ya kuacha kazi yake ya sasa, kazi aliyoichagua mwenyewe katika utumishi wa umma, kwa nini unamlazimisha akubali kazi mpya ambayo hajaikubali?
Mbona unataka kuturudisha enzi za utumwa?
Watu wana haki ya kibinadamu ya kufanya kazi wanazopenda, ambazo wana ujuzi nazo na pengine wamezisomea. Hii ni haki ya kibinadamu.
Rais kumpangia mtu kazi asiyoitaka, na jamii kulazimisha mtu afanye kazi hiyo kwa sababu rais kapanga tu, ni kumvunjia haki ya kibinadamu mtu asiyeitaka hii kazi.
Narudia tena, rais kuteua watu kabla ya kuwasiliana nao kujua kama watakubali teuzi ni dharau na ujinga.
Marais wote wanaofanya hivi wana dharau na ujinga.
Kama mtu ana umuhimu mpaka kazi yake inafanyiwa uteuzi na rais, basi ana umuhimu wa kuulizwa kama ataikubali hiyo kazi.
Hata kama ni kwa kumuepusha rais na aibu ya kukataliwa teuzi tu.
Ona sasa rais mzima anapata aibu, kateua watu, wamemkatalia teuzi zake.
Kwa sababu ndogo ya kijinga tu, watu wa Ikulu wameshindwa kupiga simu tu kupata uhakika kama aliyetaka kuteukiwa akiteuliwa atakubali uteuzi.
Yani suala dogo tu la mawasiliano kuhakiki uteuzi utaenda vizuri linaishinda Ikulu mpaka rais anapata aibu hivi.
Ukubwa au udogo wa nadaraka ya rais hauondoi ukweli kwamba kumteua mtu cheo bila hata kumuambia unamteua ni dharau na ujinga.Hapa sasa mtaona ukubwa wa madaraka ya Rais
Tangu atoke CAG na Spika hii nchi[emoji1430][emoji1430]
Hivi unajizima data mkuu kuhusu mikataba ya kazi?Ukubwa au udogo wa nadaraka ya rais hauondoi ukweli kwamba kumteua mtu cheo bila hata kumuambia unamteua ni dharau na ujinga.
Kuna watu wengine ndiyo kwanza wamejua wana magonjwa, hawataki teuzi, wanapanga kukaa na familia zao kufurahia maisha yao bila stress za kazi za serikali ambazo zitawaharibia afya zao.
Na hao utawalazimisha wafanye kazi za teuzi kwa sababu rais kasema?
Watu wenye busara, heshima na maarifa, hata akijua kazi utaikubali on the spot, anakupa japo siku moja ukafikirie, ukashauriane na familia yako, halafu angalau kesho utoe jibu kama kazi utaikubali ama la, kabla ya kutangaza.
Sisi bado tuna ulimbukeni wa kuona teuzi za rais hazina mjadala.
Kwa ujinga huu mtateua mtu halafu mtaambiwa huyo mbona kashafariki majuzi.Hivi unajizima data mkuu kuhusu mikataba ya kazi?
Huwa hamna kipengele cha kufanya majukumu yoyote kwa maelekezo ya mwajiri?
Ukisoma huu uzi na kuona watu wanavyotetea serikali kuteua watu bila hata kuwataarifu kabla, utaona Watanzania wengi bado wana mawazo ya kitumwa.Kazi za kuteuana ni utumwa na upuuzi. Leo upo Kasulu kesho unapelekwa Kyela keshokutwa unatemwa. Mtu timamu hawezi kubali huu utumwa.
More power kwa wote waliokataa huu upuuzi
Hawa ni kama sangara; tayari wameshajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Kwanza ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana kwa Nchi na kwa mamlaka ya uteuzi pia. Assuming wasingekuwa na kazi, je wangeweza kukataa uteuzi? Na kama wana kazi, je kazi hizo ni kubwa kuliko u-DC. Kuna kitu nyuma ya paziaKama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.
Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?
Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?
Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na
1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.
2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?
3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?
Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania
Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
View attachment 2501128
Funguka vizuri. Walimu siku hizi wanalipwa hadi mil 7.8?Mshahara wa milioni 4 na kutokuwa na uhakika na cheo Vs Mshahara M 7.8 na uhakika wa cheo utaenda wapi?
Utovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.Hawa ni kama sangara; tayari wameshajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Kwanza ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana kwa Nchi na kwa mamlaka ya uteuzi pia. Assuming wasingekuwa na kazi, je wangeweza kukataa uteuzi? Na kama wana kazi, je kazi hizo ni kubwa kuliko u-DC. Kuna kitu nyuma ya pazia
Wakoloni hawajawahi kuwa watawala halali wa nchi hii kwa sababu siyo nchi yao. Nyerere aliwakataliwa wakoloni kwa sababu alikuwa anawadharau, walikuwa wamejimilikisha nchi ambayo ni yake yeye (Nyerere) huku wakati huo huo nao wakidai kuwa ni nchi yao.Nyerere alikataa serikali ya ukoloni na kazi yake, kwa sababu ya uzalendo kwa nchi yake.
Yajayo yanafurahisha, ninawaonea hurumiaUtovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.
Huo si utovu wa nidhamu tu, pia ni dharau na ujinga.
Sasa kama mtu anaona utawala wa sasa si halali utamlazimisha autumikie?Wakoloni hawajawahi kuwa watawala halali wa nchi hii kwa sababu siyo nchi yao. Nyerere aliwakataliwa wakoloni kwa sababu alikuwa anawadharau, walikuwa wamejimilikisha nchi ambayo ni yake yeye (Nyerere) huku wakati huo huo nao wakidai kuwa ni nchi yao.
Tofauti na ilivyo sasa, wanaotouliwa wanateuliwa kwenye nchi yao na anayewatuea, naye pia anawateua akiwa kwenye nchi yake. Usifananishe mamlaka za sasa za uteuzi na wakoloni; wakoloni si walikuwa wezi tu?
That is neither here nor there.Yajayo yanafurahisha, ninawaonea hurumia
Sekta binafsi mna tamboThat is neither here nor there.
Unaweza kuwaonea huruma kwa sababu serikali inaweza kufanya mambo kibabe.
Lakini kwa haki kabisa, watu wana haki ya angalau kupewa taarifa kuhusu teuzi, wapate nafasi ya kuzikubali au kuzikataa, kabla hazijatangazwa kwa umma.
Busara hii ingeiepushia serikali aibu ya sasa.
Kwani lazima?Sekta binafsi mna tambo
Utadhani huko boss wako hawezi kukupangia kituo
Boss una mawazo mazuri sana: Ila nakukumbusha uzingatie hizi principle mbili,Utovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.
Huo si utovu wa nidhamu tu, pia ni dharau na ujinga.