Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Tatizo watu wanaendekeza umasikini.

Kuna watu wana wito wa ualimu, hawana wito wa Ukuu wa Wilaya.

Ukiwateua kazi ambayo hawana wito nayo umewaharibia mipango yao.

Yani, kitu cha msingi ni maelewano.

Ukiteuliwa kazi bila hata kuulizwa, umedharauliwa.

Umeonekana kwamba wewe huna maoni katika uamuzi huo.

Wewe ni mtu wa kupangiwa tu.
Usingekubali utumishi wa umma
Kakae sekta binafsi ujipangie maisha
 
Usingekubali utumishi wa umma
Kakae sekta binafsi ujipangie maisha
Hapana,

Kwani hata hiyo kazi ya sasa ya utumishi wa umma mtu hana haki ya kuacha?

Kama mtu ana haki ya kuacha kazi yake ya sasa, kazi aliyoichagua mwenyewe katika utumishi wa umma, kwa nini unamlazimisha akubali kazi mpya ambayo hajaikubali?

Mbona unataka kuturudisha enzi za utumwa?

Watu wana haki ya kibinadamu ya kufanya kazi wanazopenda, ambazo wana ujuzi nazo na pengine wamezisomea. Hii ni haki ya kibinadamu.

Rais kumpangia mtu kazi asiyoitaka, na jamii kulazimisha mtu afanye kazi hiyo kwa sababu rais kapanga tu, ni kumvunjia haki ya kibinadamu mtu asiyeitaka hii kazi.

Narudia tena, rais kuteua watu kabla ya kuwasiliana nao kujua kama watakubali teuzi ni dharau na ujinga.

Marais wote wanaofanya hivi wana dharau na ujinga.

Kama mtu ana umuhimu mpaka kazi yake inafanyiwa uteuzi na rais, basi ana umuhimu wa kuulizwa kama ataikubali hiyo kazi.

Hata kama ni kwa kumuepusha rais na aibu ya kukataliwa teuzi tu.

Ona sasa rais mzima anapata aibu, kateua watu, wamemkatalia teuzi zake.

Kwa sababu ndogo ya kijinga tu, watu wa Ikulu wameshindwa kupiga simu tu kupata uhakika kama aliyetaka kuteukiwa akiteuliwa atakubali uteuzi.

Yani suala dogo tu la mawasiliano kuhakiki uteuzi utaenda vizuri linaishinda Ikulu mpaka rais anapata aibu hivi.
 
U-DC na U-RC umeshapoteza hadhi yake hasa kwa hiyo miaka 7 ya mwendazake, yaani unachukua cheo unakwenda kufanya kazi za CCM utake usitake.

Kuweka watu ndani, kuonea watu wewe mwenyewe kusemwa hadharani - kwa kweli ukiwa mtu mwadilifu kabisa hivi vyeo havina maana.
 
Hapana,

Kwani hata hiyo kazi ya sasa ya utumishi wa umma mtu hana haki ya kuacha?

Kama mtu ana haki ya kuacha kazi yake ya sasa, kazi aliyoichagua mwenyewe katika utumishi wa umma, kwa nini unamlazimisha akubali kazi mpya ambayo hajaikubali?

Mbona unataka kuturudisha enzi za utumwa?

Watu wana haki ya kibinadamu ya kufanya kazi wanazopenda, ambazo wana ujuzi nazo na pengine wamezisomea. Hii ni haki ya kibinadamu.

Rais kumpangia mtu kazi asiyoitaka, na jamii kulazimisha mtu afanye kazi hiyo kwa sababu rais kapanga tu, ni kumvunjia haki ya kibinadamu mtu asiyeitaka hii kazi.

Narudia tena, rais kuteua watu kabla ya kuwasiliana nao kujua kama watakubali teuzi ni dharau na ujinga.

Marais wote wanaofanya hivi wana dharau na ujinga.

Kama mtu ana umuhimu mpaka kazi yake inafanyiwa uteuzi na rais, basi ana umuhimu wa kuulizwa kama ataikubali hiyo kazi.

Hata kama ni kwa kumuepusha rais na aibu ya kukataliwa teuzi tu.

Ona sasa rais mzima anapata aibu, kateua watu, wamemkatalia teuzi zake.

Kwa sababu ndogo ya kijinga tu, watu wa Ikulu wameshindwa kupiga simu tu kupata uhakika kama aliyetaka kuteukiwa akiteuliwa atakubali uteuzi.

Yani suala dogo tu la mawasiliano kuhakiki uteuzi utaenda vizuri linaishinda Ikulu mpaka rais anapata aibu hivi.
Hapa sasa mtaona ukubwa wa madaraka ya Rais

Tangu atoke CAG na Spika hii nchi🙌🏽🙌🏽
 
Hapa sasa mtaona ukubwa wa madaraka ya Rais

Tangu atoke CAG na Spika hii nchi[emoji1430][emoji1430]
Ukubwa au udogo wa nadaraka ya rais hauondoi ukweli kwamba kumteua mtu cheo bila hata kumuambia unamteua ni dharau na ujinga.

Kuna watu wengine ndiyo kwanza wamejua wana magonjwa, hawataki teuzi, wanapanga kukaa na familia zao kufurahia maisha yao bila stress za kazi za serikali ambazo zitawaharibia afya zao.

Na hao utawalazimisha wafanye kazi za teuzi kwa sababu rais kasema?

Watu wenye busara, heshima na maarifa, hata akijua kazi utaikubali on the spot, anakupa japo siku moja ukafikirie, ukashauriane na familia yako, halafu angalau kesho utoe jibu kama kazi utaikubali ama la, kabla ya kutangaza.

Sisi bado tuna ulimbukeni wa kuona teuzi za rais hazina mjadala.
 
Hivi unajizima data mkuu kuhusu mikataba ya kazi?
Huwa hamna kipengele cha kufanya majukumu yoyote kwa maelekezo ya mwajiri?
 
Kwa ujinga huu mtateua mtu halafu mtaambiwa huyo mbona kashafariki majuzi.

Yani watu wakiangalia tarehe ya uteuzi wanaona mtu kateuliwa wakati kashafariki kitambo tu kabla ya uteuzi.

Halafu watu watapata headline kuubwa.

"Rais wa Tanzania amteua marehemu kuwa Mkuu wa Wilaya". -Ikulu Haikufanya Mawasiliano Hata ya Kumjulia Hali Mteule.

Mfanyakazi wa serikali naye ana haki ya kujulishwa kuhusu uteuzi, aujadili na familia yake, wakubaliane. Teuzi zinahamisha watu, zinatenganisha familia. Familia zina haki ya kuzijadili, kuzikubali au kuzikataa, kabla rais hajatangaza majina.

Sio unamkurupusha mtu na uteuzi, tena uteuzi wa kumhamisha kituo cha kazi, kwa habari za kusikia redioni tu.

Kuna mtu mwingine anaweza kuona hii kazi haiwezi, sasa wewe unataka kulazimisha aiweze kabla hujamsikiliza?
 
Hofu ni kutumbuliwa! Ni kazi ya heshima na kama umekaa kiupigaji unapiga kwa kutumia cheo chako. Ujue wewe ni raisi wa sehemu husika, kila kitu kipo chini yako. Hata hao wateule wengine hapo wilayani wewe ni bosi wao.
 
Kazi za kuteuana ni utumwa na upuuzi. Leo upo Kasulu kesho unapelekwa Kyela keshokutwa unatemwa. Mtu timamu hawezi kubali huu utumwa.

More power kwa wote waliokataa huu upuuzi
Ukisoma huu uzi na kuona watu wanavyotetea serikali kuteua watu bila hata kuwataarifu kabla, utaona Watanzania wengi bado wana mawazo ya kitumwa.
 
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2501128
Hawa ni kama sangara; tayari wameshajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Kwanza ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana kwa Nchi na kwa mamlaka ya uteuzi pia. Assuming wasingekuwa na kazi, je wangeweza kukataa uteuzi? Na kama wana kazi, je kazi hizo ni kubwa kuliko u-DC. Kuna kitu nyuma ya pazia
 
Utovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.

Huo si utovu wa nidhamu tu, pia ni dharau na ujinga.
 
Nyerere alikataa serikali ya ukoloni na kazi yake, kwa sababu ya uzalendo kwa nchi yake.
Wakoloni hawajawahi kuwa watawala halali wa nchi hii kwa sababu siyo nchi yao. Nyerere aliwakataliwa wakoloni kwa sababu alikuwa anawadharau, walikuwa wamejimilikisha nchi ambayo ni yake yeye (Nyerere) huku wakati huo huo nao wakidai kuwa ni nchi yao.
Tofauti na ilivyo sasa, wanaotouliwa wanateuliwa kwenye nchi yao na anayewatuea, naye pia anawateua akiwa kwenye nchi yake. Usifananishe mamlaka za sasa za uteuzi na wakoloni; wakoloni si walikuwa wezi tu?
 
Utovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.

Huo si utovu wa nidhamu tu, pia ni dharau na ujinga.
Yajayo yanafurahisha, ninawaonea hurumia
 
Sasa kama mtu anaona utawala wa sasa si halali utamlazimisha autumikie?
 
Yajayo yanafurahisha, ninawaonea hurumia
That is neither here nor there.

Unaweza kuwaonea huruma kwa sababu serikali inaweza kufanya mambo kibabe.

Lakini kwa haki kabisa, watu wana haki ya angalau kupewa taarifa kuhusu teuzi, wapate nafasi ya kuzikubali au kuzikataa, kabla hazijatangazwa kwa umma.

Busara hii, licha ya kuwatendea haki wateule na familia zao, pia ingeiepushia serikali aibu ya sasa ya kukataliwa teuzi zake.
 
That is neither here nor there.

Unaweza kuwaonea huruma kwa sababu serikali inaweza kufanya mambo kibabe.

Lakini kwa haki kabisa, watu wana haki ya angalau kupewa taarifa kuhusu teuzi, wapate nafasi ya kuzikubali au kuzikataa, kabla hazijatangazwa kwa umma.

Busara hii ingeiepushia serikali aibu ya sasa.
Sekta binafsi mna tambo
Utadhani huko boss wako hawezi kukupangia kituo
 
Utovu wa nidhamu wameanza Ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata kufanya mawasiliano nao kabla.

Huo si utovu wa nidhamu tu, pia ni dharau na ujinga.
Boss una mawazo mazuri sana: Ila nakukumbusha uzingatie hizi principle mbili,
1:Boss hakosei
2:Endapo boss akikosea rejea principle namba 1.
Kwahiyo hao ndg zetu wanaweza kupoteza vyote kwa pamoja. Mfano tu mdogo mimi nimpe kazi ya kufanya mwanangu halafu akatae aniambie mimi hiyo kazi sitaki nina kazi nyingine na wakati huo kazi zote ziko chini ya mamlaka yangu, sitakubali, huo ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu
 
Back
Top Bottom