Let_Clarity
New Member
- Aug 26, 2022
- 1
- 0
Mwaka 2019 ulionesha ya kwamba asilimia 13.6 ya pato la Tanzania (Kitomari, 2019) lilitokana na sekta ya sanaa na burudani. Hii ni kujumulisha sanaa ya kuigiza, muziki, uchoraji na michezo. Katika robo ya kwanza ya mwaka huo huo wa 2019, nchi ya Nigeria ilipata asilimia 0.27% ya pato la taifa kutoka sekta ya sanaa na burudani. Kwa takwimu hizi chache tu tunaona ya kwamba sekta ya sanaa na burudani ya Tanzania inauwezo na nafasi kubwa sanaa ya kuteka uchumi kwa kasi ndani ya nchi na barala Afrika. Makala hii itazungumzia faida na changamoto ya sekta ya sanaa na burudani kwa ajili ya jamii na uchumi. Pia itaangalia namna gani kama jamii tunaweza kuchangia kuboresha sekta hii kwa ajili ya maendeleo yake.
Kwanza kabisa, kwa nchi zinazoendelea sekta ya sanaa na burudani inaleta uhuru wa kifedha au uchumi yaani financial freedom and independence. Kwa mfano mwaka 1950, baada ya kupoteza kazi kwenye shamba la katani huko Tanga, hayati Edward Saidi Tingatinga alianza kuwa msanii wa uchoraji. Hadi sasa sanaa yake ya Tingatinga imevuma nchini kote na kuleta faida za kikazi zaidi kati ya wachoraji wadogo wadogo nchini. Tingatinga imesambaa duniani kote, hata kujulikana kama aina ya uchoraji wa kimila.
Kumaanisha ya kwamba baada ya kukosa kazi ya kuajiriwa, Bw. Tingatinga alijiajiri na kujipatia kipato kupitia kazi zake za sanaa. Vivyo hivyo basi, kwa kulinganisha na takwimu zinazoonesha kuwa mwaka wa 2014 asilimia 13.7 ya vijana Tanzania walikuwa hawana kazi, tunaona kwamba kupitia sanaa takwimu hizi zinaweza kuboreka. Jambo hili sio jipya sana, ila kwa kutoa elimu bora ya uchoraji na fursa za maonesho ili kuleta utandawazi wa kazi za sanaa, sekta hii inaweza kukua zaidi.
Cha pili, sekta ya sanaa na burudani inaweza kusisimua jamii kwa kuelezea matukio na hadithi tofauti yasiyoweza kuelezeka kwa maneno tu. Kwa kupitia majumba ya kuhifadhi sanaa kwa ajili ya historia na uwekevu wa utamaduni, watu wanaweza kujifunza. Kwa mfano, ndani ya jumba la sanaa liliopo huko Ufaransa, Louvre. Sanaa za kale zimehifadhiwa huko kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Mojawapo za aina za sanaa za kihistoria ni picha za kuchorwa za vita vya mapinduzi vya Ufaransa mnamo 1600.
Kwa kupitia sanaa ya uchoraji, leo hii tunaweza kuelewa nini haswa kilichokuwa kinaendelea Ufaransa majira hayo. Lakini kwa kuongeza tunaweza kujadili mada tofauti kwa kuangalia picha za michoro na namna mchoraji alisimulia matukio yaliyo endelea kijamii ya kisiasa. Kwa hivyo, kupitia majumba ya hifadhi za sanaa tunaweza kutunza historia za kitanzania kwa ajili ya faida ya vizazi vijavyo. Pia, majumba ya kuhifadhi na kuonesha sanaa, yanaweza kuleta kipato nchini na kwa watu binafsi. Kwa maana inakuwa sehemu ya kutoa elimu, burudani, kipato na pia kuleta uelewa wa jamii tofauti.
Pia,sekta ya sanaa na burudani ikishirikiana na sekta ya tekonolojia na sayansi inaweza kuleta mabadiliko makubwa sana. Kwa kadri ya takwimu zinaonesha takribani asilimia 90% ya filamu zenye faida kubwa zinatumia teknolojia ya CGI yaani Computer Generated Imagery. CGI ni aina ya michoro inayotumia kompyuta katika mifumo ya 2D na 3D. CGI inasaidia katika utengenezaji wa katuni za watoto au za watu wazima. Zaidi ya hapo, CGI inaruhusu msanii alieandika hadithi kujielezea na kufafanua mawazo yake kwa hali ya uhalisia zaidi hata kama ni kitu kisichoelezeka, yaani kama ndoto.
Jambo hili basi linatoa fursa kubwa sana kwa watanzania kujifunza na kuvumbua namna yakukuza sekta ya sanaa na burudani kupitia teknolojia hii. Kwa mfano, Ingawa facebook ilianza kama kampuni ya tekonolojia na mitandao ya kijamii mwaka wa 2004, leo hii imekua na kujitambulisha kama Metaverse. Metaverse ambayo karibia asilimia 100% ya ulimwengu huu wa mtandaoni inatumia CGI katika mifumo ya Virtual Reality na Artificial Intelligence ndio ubaadaye wa mawasiliano ya baadae duniani(McGheehan, 2022).
Je, Unaonaje vijana was sasa wakiwezeshwa kuelewa namna ya kusimamia tekonolojia kama hizi. Ikiwezekana, basi vijana wengi wataweza kuwekwa huru kiuchumi na pia kuwezesha nchi yetu kuendelea katika sekta ya teknolojia na ya sanaa na burudani.
Sanaa na burudani ni vitu ambavyo haviishi tu kwenye makaratsi au mabango na runinga pia redio. Burudani na sanaa pia ni namna mji ulivyopangiliwa, majengo yalivyojengwa, nguo zinazovaliwa bila kusahau vyombo vya usafiri. Vyote vilivyotajwa hua vinaleta burudani kwa binadamu maana vinavutia kwa macho na sanaa iliyotumika pamoja na sekta za aina nyengine ili kuboresha muonekano ya vitu kwa ajili ya mtumiaji. Kwa mfano, jengo la cultural heritage centre la Arusha.
Jengo hili linavutia kwa mambo mengi. Kwanza ili kubuniwa ilichorwa na msanii mwenye uelewa wa ukandarasi, pili likaingizwa kwenye kompyuta na kwa kutumia software yenye uwezo wa CGI likaboreshwa iliwaandisi waelewe namna linge jengwa. Pia baada ya kukamilika, linavutia kwenye macho kwa watu wote iwe wananchi au wageni. Zaidi ya hapo limehifadhi bidhaa za sanaa zakuchorwa na vinyago. Kwa vyote hivyo, jengo la Cultural heritage linaleta kipato kwa ajili ya watu wa ngazi tofauti (Kilonzo, 2016).
Sambamba na hayo yote yaliosemwa awali, sekta ya sanaa na burudani ina changamoto, haswa kwenye swala la uwekezaji wa kifedha hata na vifaa. Tanzania kwa asilimia kubwa bado ipo nyuma kwenye kutengeneza burudani yenye viwango vya juu. Filamu na tamthilia za kitanzania bado zinabaki nyuma kwa sababu ya vikwazo vinavyowekwa mbele ya watengenezaji filamu.
Kwa mfano, filamu ya black panther ni filamu ya kuhusu waafrika lakini imeandikwa na mmarekani na kutengezwa na vifaa vyao. Je? Kungekuwa na watu wenye kuona umuhimu wa filamu na pia wangewekeza si ubora wa filamu zetu zingekuwa bora? Si pia tungetoka katika dimbwi lakufanya hadithi za maisha ya kawaida na kujaribu kutengeneza filamu zengine zenye uzito na mifano ya ndoto?
Hitimisho ni bila sanaa na burudani tusingekuwa na filamu wala muziki, bila sanaa hadithi na picha za filamu na michoro zisingefanya vizuri. Burudani na sanaa ni sekta ambayo watu wanapuuzia ingawa ni kitu kinachotumika kila siku. Kwa kuweka jitihada za kuikuza na kuithamini inaweza kuleta mabadaliko makubwa nchini. Pia kwa kuboresha kazi za sanaa na kutafuta wawekezaji, sekta hii inaweza kubadilisha maisha ya jamii na uchumi wake.

Upvote
0