Kuthibitishwa kazini kwa utumishi wa umma

Kuthibitishwa kazini kwa utumishi wa umma

BWANA MISOSI

Member
Joined
Feb 11, 2020
Posts
39
Reaction score
24
Habari wana JF.

Naomba kuuliza kwa wale watumishi walioajiriwa kwenye taasis ya umma, baada ya mwaka unatakiwa kuthibishwa kazini, swali, je kuna taratibu zipi zinapitiwa ili uthibishwe?

Je, unaweza kukatariwa usithibitishwe? Kwa sababu zipi?
 
Upo sahihi kabisa mkuu mpima mstaafu , kimsingi lengo la probation ni kukupima utendaji kazi wako kama unafit kwa ajira uliyoajiriwa nayo. Endapo mwajiri atakuwa hajaridhika na utendaji wako anaweza ku-extend muda wako wa matazamio. Na kumbuka hutakiwi kumuandikia barua mwajiri ya kutaka uthibitishwe kazini. Kwa rejea zaidi, kwa sababu mleta mada anaonekana ni mwajiriwa mpya, tafuta kitu inaitwa "Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma" (Standing Orders for the Public Service) Toleo la Tatu la 2009, pitia vifungu kuanzia D.38 hadi D.47 imefafanuliwa vizuri kabisa
 
Habari wana JF.
Naomba kuuliza kwa wale watumishi walioajiriwa kwenye taasis ya umma, baada ya mwaka unatakiwa kuthibishwa kazini, swali, je kuna taratibu zipi zinapitiwa ili uthibishwe? je unaweza kukatariwa usithibitishwe? kwa sababu zipi?
Ili uthibitishwe kazini mwajiri wako lazima aridhike na utendaji kazi wako na pia aridhike na tabia zako mahala pa kazi. Maana unaweza kuwa mchapakazi lakini mgomvi au unakiburi.
kwa ushauri zaidi soma vision ya taasisi ulikoajiriwa na pia soma job descriptions na standing order muhimu
 
Back
Top Bottom