Kutoa fungu la kumi unamtolea Mungu sio mwanadam. Toa ukutane na Mungu

Kutoa fungu la kumi unamtolea Mungu sio mwanadam. Toa ukutane na Mungu

Ndio mana wachungaji wana miliki RANGE, CADILLACS, VX, V8, PRADO TX halafu waumini hata baiskeli ya miti Hakuna .
 
Mungu yuko wapi nikamkabidhi yeye mwenyewe hela zake?

Kama hayupo niende kumkabidhi yeye mwenyewe basi hayo mengine ni utapeli kama utapeli mwingine.

Dini ni utapeli kama utapeli mwingine Mungu hayupo.
 
Swali kuu : Unampa nani aiwasilishe kwa Mungu?

unamwamini?
 
Kwahiyo ambao hatuna cha kutoa hatutakuja kukutana naye?
 
Dunia imejaa uongo mwingi.
Jiulize yeye aliyeumba ulimwengu na kila kitu, anahitaji kisenti chako Ili iweje?
Tutumie akili hiyo ni miradi ya watu, amkeni amkeni
 
Back
Top Bottom