Kutoa hela UTT changamoto CRDB

Sawa... Unaweza kunifafanulia hiyo 23,000 tsh uliyoambiwa ulipe kwanza ni ya nini?.
Ni KWamBA mwezi WA Saba nilikwenda bank crdb lengo likiwa ni kutoa pesa kwenye mfuko niliojiunga nao.
Nilipomaliza kujaza nikawakabidhi niliyemkabidhi akasema natakiwa kulipa tshs elfu 23 ETI ya gharama za usafirishaji WA fomu. Nikachukua karatasi ya Benki ya malipo akanielekeza niende kwa mhudumu dirishan nilipe.
Nilipofika Kwa mhudumu akasema nenda umwambie HUYO akupe akaunti namba yaani Yule niliyempa fomu. Nikarudi kwake nikashangaa naye ni kama anakuwa na wasiwasi baadae akanipa akaunti nikalipa.

Lakin Jana nimekwenda tena kujaza fomu bank ileile ili nitoe pesa nilipomaliza kujaza wàle wahudumu sjui walikuwa wapi maana nilisubiri sana nikaamua itelekeza fomu kwenye meza Yao jioni nashangaa wananipigia wakiniulza kwamba fomu yangu waitume au waiache nikawaambia itumeni Ila aliyenipigia hakuniambia Mambo ya malipo ndo nikabaki njiapanda mbona siku za nyuma niliambiwa kulipa ndo fomu itumwe Leo vp tena.
Inaonekana wale watu WA crdb ni wajanja wajanja Sana hivyo ndo nikaja huku kupata maoni ya raia je nao waliwahi kulipishwa.
 
Kama akaunti namba unaijua we wapigie uwaambie unahitaji kujua salio la akaunt yako. Mi ninayo namba ya MTU WA makao makuu kabisa
Mkuu naomba izo namba pm Asante sana
 
Pole sana mkuu umepigwa! Fuatilia hiyo 23000/= amelipwa nani na chukua akaunti namba iliyopokea pesa uwasiliane na UTT wakufafanulie kama kweli utaratibu uko hivyo unapotoa pesa.

Unataka kutoa pesa yako mwenyewe kutoka mfuko mmoja wa UTT, halafu unaambiwa ulipe 23000 ya kusafirisha fomu ? Hii imeanza lini? Itabidi tupate maelezo kwenye mkutano mkuu.
 
Takuwa nimepigwa aisee ngoja tamcheck Yule jamaa kukw makao.
Waliniweza maana pesa nilikuwaga natolea DSM makao nilipokuja huku mkoa ndo hivyo utt hawana ofisi ikabdi nitumie bank.
 
Labda utufahamishe kwanza;

Ulivyolipa mara ya kwanza walikupa account number inayosoma mwenye account ni nani? Au ulipewa account ya mtu binafsi? Halafu baada ya kupata majibu hayo sasa ndio nafikiri tutaendelea na mada yetu.
 
Labda utufahamishe kwanza;

Ulivyolipa mara ya kwanza walikupa account number inayosoma mwenye account ni nani? Au ulipewa account ya mtu binafsi? Halafu baada ya kupata majibu hayo sasa ndio nafikiri tutaendelea na mada yetu.
NiLipewa akaunti Tu bila Jina niliambiwa nijaze akaunti namba Tu kisha nipeleke dirishani nilipe.
Uwenda ni mchezo Tu walicheza maana hata kwenye kutoa akaunti namba walikuwa wanarushiana mpira uwenda hapo iliingia kwa Mtu akala 20 Ile bk tatu ya kutolea si unajua ATM inatoa kuanzia 10
 
Hahaha, duuuh!! 😂🤣

Mkuu hapa naona kama kuna shida yani, binafsi huwezi kunijazisha fomu ya ku deposit pesa afu usiniambie na deposit mzigo unaenda wapi.. afu inamana baada ya ku deposit si wanakupa copy moja kama reference kwako, je hiyo copy pia hawakukupa??

Yani nakuwa kama naona bado changamoto ipo kwako mkuu wangu.
 
Hongera mkuu kwa kuwa mkongwe wa utt, mm ninakaribia mwez wa pili tangu nijiunge. [emoji1]
 
Kama akaunti namba unaijua we wapigie uwaambie unahitaji kujua salio la akaunt yako. Mi ninayo namba ya MTU WA makao makuu kabisa
Ntakucheki nilipotea kidogo.... Tulinunuliwa na mama yetu watoto wote.. Wenzangu waliuza zote .. Am an Economist I knew they will value .. Nonetheless nilipuuza ... Nicheke kidogo ...lakini niliuza na kubakiza
 
Inategemea na aina ya account, inaonyesha wewe sio mteja wa liquid fund. Bond fund ni moja ya account zinazokaa hizo siku unazosema
Lakin bond fund ukishafikisha kiwqngo chako cha uwekezaji, si wanalipa ile faida moja kwa moja kwenye akaunti yako ya CRDB? Msaada please!
 
Lakin bond fund ukishafikisha kiwqngo chako cha uwekezaji, si wanalipa ile faida moja kwa moja kwenye akaunti yako ya CRDB? Msaada please!
Yes, wanalipa monthly au kila baada ya miezi sita. Inategemea na matakwa yako. Unakua kama umejitengenezea mshahara
 
Kookolikoo, naomba shule hii kuhusu UTT na hati fungani za BOT, tofauti zake
UTT ni nzuri kwa kudunduliza na kama sio mpenda ushindani. Kupata bonds kuna minada inafanyika. Sio kila unapoomba unapata. UTT unaweza ukawa unaweka huko kila senti unayoipata. UTT return ni 10 hadi 12 asilimia. Bonds ni hadi 15.75 asilimia, inategemea na bond iliyotangazwa na kipindi cha mrejesho wa uwekezaji (umri wa bond)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…