GE2025 Kutoa magari kwa wagombea ndiyo kunatumika kama kipimo cha usawa?

GE2025 Kutoa magari kwa wagombea ndiyo kunatumika kama kipimo cha usawa?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Chama cha ACT Wazalendo kimefafanua sababu zilizopelekea kukataa kupokea gari maalum alilokuwa amekabidhiwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Luhaga Mpina na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya makao makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Septemba 13.2025, Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo Omar Said Shaaban amesema chama hicho hakiwezi kupokea gari la kifahari wakati wananchi wengi wakiwa maskini na kwamba gari haiwezi kuwa kipimo cha usawa kwenye uchaguzi

 
Utoaji wa hayo magari, ni moja ya matumizi mabaya kabisa ya fedha za walipa kodi!
 
Hilo Gari likichunguzwa limejaa makamera, masipika sijui wanaita vinasa sauti, yote ni mbinu za kumpleka akamsalimie mwenzake yule wa risas 16 kule aliko...
 
Wenzao ADA TADEA wameishukuru INEC kwa kuwapa gari, wasema huo ndio usawa
 
Chama cha ACT Wazalendo kimefafanua sababu zilizopelekea kukataa kupokea gari maalum alilokuwa amekabidhiwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Luhaga Mpina na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya makao makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Septemba 13.2025, Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo Omar Said Shaaban amesema chama hicho hakiwezi kupokea gari la kifahari wakati wananchi wengi wakiwa maskini na kwamba gari haiwezi kuwa kipimo cha usawa kwenye uchaguzi

View attachment 3471259
KInachonishangaza tu INEC wamepata wapi pesa zakununulia wagombea magari.

Je huu utakuwa muendelezo au ni kwaajili tu ya uchaguzi wa mwaka huu.

Kama wagombea 18 wanapatiwa zero kilomita basi hii nchi ina pesa sana za kuchezea.

Fair play inapaswa kuonekana kwenye utangazaji wq mgombea alieshinda kwa halali katika sanduku la kura sio hiyo yakupeana magari.Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Back
Top Bottom