Kutoa mali kwa mtoto wa nje ya ndoa

NATIONALISM

Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
24
Reaction score
1
naomba wataalamu wa humu ndani juu ya hili
Ni kwamba baba alizaa mtoto wa nje mwanaume,sasa baba analazimisha kumpa shamba bila sie watoto wakubwa kuridhia.
Kisheria likoje!
 
naomba wataalamu wa humu ndani juu ya hili
Ni kwamba baba alizaa mtoto wa nje mwanaume,sasa baba analazimisha kumpa shamba bila sie watoto wakubwa kuridhia.
Kisheria likoje!

Tafuta chako mkuu , katu usiishi kwa kuvizia au kutegemea mali ya
urithi kwani mwenye mali ni mshua na anaruhusiwa kugawa
kadri yeye atavyopendekeza, maadamu hajakata kamba.

NB: Wimbo wa kima marehemu TX mosh Wilium,
Tutatoana roho yarabiii....kwa mali alizoacha baaaa.....
 
Huoni aibu kulilia vya baba yako. Kama wewe ni me una matatizo.
 
Huoni aibu kulilia vya baba yako. Kama wewe ni me una matatizo.

By nationalism
Mimi nilihitaji msaada wa kisheria na sihitaji ushauri wenu,matusi wala mabango.
SI KILA MAONI YAWE NI YA KIHIVYO,ELIMU YENU IWAKOMBOE KIFIKRA
 
Mshua keshaamua sasa nyie mnachopinga ni nini? Acheni wivu na ubaguzi, huyo ni ndugu yenu kwa nini mnamtenga, ishini kwa kupendana Kama baba yenu anavyowapenda ndio maana akagawa kwa wote, au nyinyi hawapi?
 
Wewe ni mtoto wa baba yake huyo .unadhani sheria itakupa uhalali wa mali ya baba yenu wewe peke yako?
Kama unavyofikiri una haki kwenye mali nae hivyo hivyo.

Mali ni za baba yako..

Anaweza hata kumpa hawara maadam bado hajafa .unataka kurithi mali ya mtu akiwa hai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…