Kutoa msaada ni sadaka inayoweza kukufanikisha katika mambo mengi kwenye maisha yako

Kutoa msaada ni sadaka inayoweza kukufanikisha katika mambo mengi kwenye maisha yako

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
Kutoa msaada kunaweza kukupa fursa kubwa maishani mwako soma hapa chini

Kutoa msaada kama vile pesa, mali , ushauri n.k kwa ndugu, jamaa na marafiki au mtu yoyote mwenye uhitaji ni sadaka pia,

Unapokuwa mtu wa kusaidia unajijengea baraka au fursa kuzipata bila kutegemea kutoka kwa Mungu.

Unapojenga utaratibu wa kusaidia mtu mwenye uwitaji kama wa kifedha, nguo, chakula au ushauri na kumpa tumaini basi jua kwamba kitu unachokifanya ni hazina kwa bwana ambayo atakulipa zaidi ya ulichotoa.

Ukitaka mafanikio au utosherezi wa mali na fedha kuwa mtoaji, ukiwa mtoaji Mungu atafanya maisha yako yaendelee kustawi sababu anajua akikupa hautatumia wewe pekee utasaidia na wengine hivyo Mungu ataendelea kukubariki.

penda kutoa sadaka, na sadaka sio kutoa kanisani pekee , sadaka unaweza kutoa kwa kumsaidia ndugu, jamaa, rafiki au mtu yoyote mwenye shida na una uwezo wa kusaidia basi toa sadaka Mungu atakubariki na kufanya maisha yako yaendelee kufanikiwa.
 
Ushauri umekua mwingi sana siku hizi... Ndugu wenyewe unawapa msaada wanaona ni haki yao kupewa na siku usipowapa wanakukalia vikao
 
Ushauri umekua mwingi sana siku hizi... Ndugu wenyewe unawapa msaada wanaona ni haki yao kupewa na siku usipowapa wanakukalia vikao
Kutoa msaada kwa ndugu ni wajibu wako na hakuna baraka.
Kusaidia wasio jiweza au wapo kwenye mkwamo ndipo palipo na baraka maana unatoa kwa maumivu na hautarajii kupata chochote kutoka kwake na inawezekana usionane tena na uliyempa msaada. Huko aliko yeye atakuombea kwa Mungu kila lililo la heri kutokana na ulicho msaidia ili upate zaidi ya kile.
 
Back
Top Bottom