emmarki
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,001
- 1,430
Habari wana jamvi.
Kisiwa cha Mafia ni mojawapo ya wilaya zinazounda mkoa wa Pwani.
Kutokana na aina ya wakazi wa kisiwa hiki kuegemea sana kwenye shughuli kuu ya uvuvi na kilimo cha nazi, imesababisha mazao jamii ya matunda na mbogamboga kuagizwa kutoka dar.
Nimeona biashara ya kununua matunda kutoka masoko ya dar na kuleta mafia itakuwa ni biashara nzuri kwa sababu ya uadimu wa matunda haswa ndizi.
Kutokana na hali ya usafiri kuwa shida, ambapo bado tunategemea kivuko kimoja cha Mv Kilindoni, lakini majahazi yapo ijapokuwa siyo salama sana kiusafirishaji.
Nategemea kuanza na kuagiaza ndizi, naomba ushauri au ABC za wapi pa kupata ndizi kwa bei nzuri. Je niagize ndizi mbichi nije kuzivundika huku Mafia au ninunue ndizi mbivu (mizigo kushindiliana itaharibu ndizi nyingi)