Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakuu poleni na janga la Corona , pamoja na taarifa nyingi sana kutoka kwenye vyombo vya habari ni kuhusu Corona , lakini nchini Tanzania kuna tatizo kubwa sana la mafuriko kwenye maeneo mengi , na hivyo kuleta shida kubwa sana kwa wananchi wa maeneo husika.
Kumekuwa na uharibifu wa makazi ya raia pamoja na ukosefu mkubwa wa chakula , baada ya nyumba na mazao mashambani kusombwa na mafuriko.
Wananchi hawa wanahitaji msaada wa hali na Mali , ndio maana Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ole Sosopi ameamua kujitokeza hadharani na kugawana kidogo alichonacho na masikini wenzake.
#Tuendelee kunawa mikono ili kujikinga na virusi vya Corona .