Ndugu zangu watanzania uwe wa CCm au wa Upande Mwingine, leo ningependa kueleza masikitiko yangu kwa muendelezo wa wizi wanaofanyiwa watanzania kupitia hii misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini, kwa kile mafisadi wanachodai kwamba sheria haiwaruhusu kuwafutia lodi ya mafuta.
Huo ni uongo kwani kinacho ongoza nchi ni sheria za nchi na sheria za kodi, na kama mkataba ukionekana unakwenda kinyume na sheria kuu, na basic principle za uendeshaji biashara basi mkataba huo ni batili, lakini kwa kuwa wahusika wengi wanaotengeneza hiyo miswada ya sheria iwe sheria kuu, sheria za kodi na mikataba yenyewe ni mafisadi, ndio maana leo hii kwa kupitia hiyo hiyo mikataba, leo hii wanataka kutuaminisha ya kwamba kitu hicho hakiwezekani (Kufuta hiyo Misamaha ya Kodi).
Pili kanuni za biashara zinataka watu wote waendeshe biashara katika hali sawa. Je leo hii wachimbaji wapya wakija itakuaje? Maana wao tumeambiwa hawatapewa misama wakati mwingine ana msama wa kodi, haki itakuwa wapi?
Hivyo naomba watanzania wote iwe ni mbunge, diwani, mtu wa kawaida nk tupinge wizi huu.