Kutojua kuongea na kuandika vizuri kiingereza itamkwe kama Ulemavu.

Kutojua kuongea na kuandika vizuri kiingereza itamkwe kama Ulemavu.

Cha ajabu shule za kata zimekuwa nyingi nchi nzima, ongeza na za english medium lakini kiingereza hakiongewi na wahitimu wake mitaani. Najiuliza hawa vijana wa bodaboda, mama lishe, machinga, wanamuziki na filamu hawakufika sekondari kujiunza kiingereza? Hata cha kubabaisha hakipo kabisa! Simu zipo zinawezesha hata kujifunza peke yako wakajifunze huko ili waondokane na aibu ya kutokujua lugha hii kubwa ya dunia nzima
 
Kama kwenye kazi zako hukutani kabisa na kiingereza basi jua bado uko shimoni... pambana utoke huko.
Tanzania biashara kubwa hatufanyi na waingereza Wala waongea kingereza tunafanya biashara kubwa mitaani na wachina bidhaa za china ndizo zimejaa nchi nzima na tunafanya na wajapani na gari zao za Toyota

Kingereza kinahitajika huko Kwa maafisa wa Serikali kukijua vizuri wajikomba Kwa wazungu wakienda kukopa mikopo world Bank,IMF na semina na warsha nk sio kwenye private sector.Private sector ya Tanzania sehemu kubwa Haina biashara na uingereza Wala nchi zinazoongea kingereza .Serikalini huko ndio Wana biashara nao malofa wakubwa wapigia yowe kikokotoo .Wanaongea kingereza weee wakiwa maofisini na nyodo zao mwisho wa siku wanapostaafu wanatungua kilio wakiongea na kulia Kwa lugha ya kiswahili kuwa kikokotoo Cha kustaafu kiangaliwe upya wao watakuwa wageni wa nani na kingereza Chao.Wanamlilia Mama Samia Kwa Kiswahili.Wakiwa ofisini kingereza kingi you know ,you know hata Raisi akiomba ushauri wanandika kingereza kuwa hii lugha ya kitaalamu sio kiswahili hopeless language.Fainali uzeeni ndio mwisho wa kingereza Cha afisa Serikali mjidai kingereza ndio Kila kitu akistaafu hiloooo linashangaa hakuna Mtu anahitaji kingereza chake kilichonyooka mtaani au kijijini
 
Haiwezekani kama nchi maskini tuendelee kubembelezana kuijua vizuri hii lugha muhimu ya kibiashara duniani. Kama tunatakiwa kufanya export zaidi ya products na services zetu hatuwezi kukwepa kukifahamu vizuri kiingereza. Hii ni lugha kuu ya biashara duniani. HAINA MJADALA.

Kuna wapuuzi wana hoja mfu kudai mbona China ina maendeleo huku wanatumia lugha yao? Hawa ni wapumbavu wanaostahili kuchapwa viboko. Wachina wamefika hapo walipofika kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya nchi yao. Nyuma ya mafanikio ya wachina kuna machozi, jasho na damu. Mao Ze Dong peke yake aliwapelekea moto wachina wenzake waache uzembe na kupiga kazi. Hata viongozi wengine waliofuatia walikuwa sio poa wakikufuma kwenye ishu za kishenzi kama ufisadi na mambo kama hayo. Hiyo imesababisha wachina wamekuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa duniani huku pia wao pekee wakiwa na soko kubwa la ndani. Sisi kujifananisha na mchina ni upuuzi. Kuna wale wanasemaga kwamba mwaka 1961 tulikuwa sawa na China kimaendeleo huwa nashangaa sana.

Kama hujui kiingereza jitahidi ujue. Kuna app ya duolingo ni rahisi kuitumia ukajua lugha. Mimi kwa sasa kiingereza nimeshamalizana nacho najifunza kifaransa. Mimi ni mtu ninayeongea kiingereza fasaha na kukiandika.
Nyerere aliambiwa ili tutawalike "KIPUMBAVU" atunyime elimu na lugha za kimataifa...akafundisha UCHAWI mashuleni "MAZINGAOMBWE" waliosoma 70s to 80s watakumbuka, akawapa leseni kina KABWERE wazunguke nchi nzima kutoa uchawi, matokeo ndo yaleee, Kipara akaloga kiti cha Spika bungeni, bado wizara ya elimu haitaki kabisa lugha ya kiingereza kuanzia darasa la kwanza, ili WAJINGA/WAPUUZI, WASHENZI, WAPUMBAVU wazidi kuongezeka.
 
How dyu dyu dyu dyu,,,,,,, Thomaaaaas mdogo mdogo,,mwendawazimu kaingiaje
 
Kama Askari wanakibonga vizuri tu wewe unashindwaje?
 

Attachments

  • Nigerian_Girl’s_Encounter_With_The_Tanzanian_Police_#shorts(360p).mp4
    5.1 MB
Back
Top Bottom