Kutoka Butiama: Exclusive news

Kutoka Butiama: Exclusive news

Hata Yesu katika Biblia anasema kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni. Tusubiri tujionee kwa macho yetu nin hatma yake.
 
Hata Yesu katika Biblia anasema kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni. Tusubiri tujionee kwa macho yetu nin hatma yake.

Tena for us bible believers these people have no shame whatsover. People say they won't go to Butiama!! They just came back from Israel after praying at some of the holiest places and in their eyes they are clean.
 
Mkuu Heshima mbele, mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, lakini no way kwamba I am a clown, vipi next time ukirekebisha hii lugha ambayo kwa kweli siyo ya kistaarabu, kutumiwa tena kwenye jamii kama hii, mimi nilifikiri tunaikataa hii lugha kwa waliotuvamia, sasa na wewe wa muda mrefu ukiitumia tutawaambia nini waliotuvamia?.

1. CCM ni chama kinachotawala Tanzania, kwa ridhaa ya wananchi waliokikubali kwa kuwapigia kura kutokana na kukubali sera zao, moja ya sera za CCM kwa taifa, ambazo waliziahidi kwenye kampeni za uchaguzi, ni pamoja na uchumi wetu ambao nguvu yake kubwa hutokea BOT, sasa CCM watafanya vipi mkutano mzito bila ya gavana? I mean regardless ya how our uchumi si doing, which as usual ni a debatable ishu, lakini ni haki not only kwa CCM, bali hata vyama vya upinzani kumuita vinapokuwa na mikutano yao mikubwa.

2. Mkuu ninaamini kwamba ungekuwa na hoja nzito sana, iwapo gavana wetu wa BOT, angekuwa in the past amewahi kuitwa kwenye mikutano mizito ya vyama vya upinzani, akakataa au CCM ikamkatalia aisende,

Otherwise, naona kama sio a weak argument, basi hakuna argument kabisaa, gavana ni lazima aende kule kwenye kikao kikubwa cha CCM, yaaani chama tawala, ili aweke mambo wazi exactly yalipo na pia wajumbe wa NEC, wapate nafasi ya kumuuliza maswali muhimu huku waziri wa hazina akiwepo, kuepuka kutupiana lawama, kama alivyofanya Mama Meghji, this time wote watakuwepo yaani waziri na gavana, I thought CCM ought to be louded kwa hiki kitendo kuliko kushambuliwa. To me the move sounds good, na ni matumaini yangu kuwa opposition wata-follow the idea in the future, wakikataliwa then tutamkoma nyani.

Ahsante Wakuu.

Mwanachama mkereketwa how is the family in tanzania?? Umeshatuma hela za genereta na bili zingine!!Vp been to your village lately..shule bora? Kuna Maendeleo?
Naomba kujua sababu zako za kusupport CCM?? (Mwalimu RIP and his CCM are long gone, so dont start your arguements with reference to him..i'm concerned abt todays CCM!!) Nielimishe!!
Alafu people should stop equating uzalendo wetu with Upizani /Chadema specifically..personally sijawahi hata kusikia hutoba moja ya Chadema and i dont even know their policies..but i like wot Zito did 🙂 (Upinzani dont knw anything CCM doesnt, seems CCM wanawapa SIFA upinzani bila kujua)

Enough with my speech..nielimishe on CCM..Seems mayb some of us are just jumping on the JF band wagon?? Labda mengi mazuri ya CCM hatuyajui...patiently waiting....
 
na Edward Ibabila

BAADHI ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), wanaojiandaa kwa ajili ya kikao chao kinachofanyika mwishoni mwa wiki huko Butiama, wamepata wakati mgumu mjini Musoma.

Wajumbe hao ambao jana walianza kutembelea miradi ya maendeleo na kuona utekelezaji wa Ilani ya chama chao katika Jimbo la Musoma Mjini, walikumbana na upinzani wa wazi kutoka kwa wananchi waliokuwa wakipiga kelele za kudai kurejeshwa kwa fedha za EPA zilizofujwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Adha hiyo ilianza muda mfupi tu baada ya Naibu Meya wa Mji wa Musoma, Daudi Misango, kusimama kwa ajili ya kuanza kuwatambulisha wajumbe hao wa NEC waliokuwa wakiongozwa na Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Aliposimama naibu meya huyo na kuwataka wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Mkendo kuitikia kiitikio cha ‘CCM oyee!’ wananchi takriban wote walinyamaza na kuwaacha makada wachache wa chama hicho waliokuwa wamekaa mbele kuitikia kwa uchache.

Ukimya huo uliofuatiwa na kelele za ‘tunataka pesa za EPA kwanza’, kulisababisha Misango abuni mbinu mpya ya kuwalazimisha wananchi hao kuitikia salamu ile ya CCM oyee! Kwa kuwaita wachawi wale wote ambao walikuwa hawanyoshi mikono juu kuitikia salamu za chama hicho tawala.

“Mmm hapa naona kuna wachawi, tuanze tena; CCM oyeee,” alisema Misango ambaye alipigwa na butwaa, baada ya kuona umati mzima uliokuwa umesubiri mkutano huo kwa muda mrefu ukiwa kimya, hali iliyomlazimisha ateremke jukwaani mara moja.

Hali hiyo ilisababisha Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo, ambaye pia ni mjumbe wa NEC Mkoa wa Mara, kupanda jukwaani ili aendelee na kazi ya kuwatambulisha wageni.

Mathayo wakati akitambulisha wajumbe wenzake, mmoja baada ya mwingine, alikumbana na tukio la ukimya wa wananchi hao wakati mjumbe mmoja wa NEC kutoka Zanzibar aliposimama na kusalimia kwa kusema: ‘Viatu vya mtoto mkubwa havai’.

Ukimya huo wa wananchi ulisababisha Mathayo kuwataka wajumbe hao wa NEC kutulia, kwa kusema wananchi wengi wa jimbo lake walikuwa hawajui Kiswahili cha Kizanzibari na ndiyo maana walishindwa kuitikia salamu za mjumbe aliyetumia usemi huo.

“Jamani nyie wageni wetu msishangae. Sisi huku Kiswahili hatukijui… nawaombeni wananchi kuwa makini kusikiliza, mjue kule Zanzibar wao wanasema skuli, sisi tunaita shule... wenzetu wanasema maji ya mfereji, sisi ya bomba, na huku tunasema sokoni, wao wanasema marikiti, hicho ni Kiswahili tu,” alisema Mathayo, kauli iliyofuatiwa na migumo na kuzomea kwa baadhi ya wananchi.

Alipoendelea na hotuba yake kwa kusema Ilani ya CCM katika jimbo hilo imetekelezwa kwa asilimia 80 na hivyo kufanya wananchi kuridhishwa na utendaji wa serikali na chama tawala, wananchi walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine katika mkutano huo wa hadhara wakiguna na hivyo kuwaacha wana CCM waliokuwa wamevalia sare za kijani na njano za chama hicho kubakia uwanjani hapo.

Akihutubia mkutano huo baadaye, wakati watu wakiwa wameshapungua, Dk. Bilal aliipongeza serikali ya manispaa hiyo kwa kutekeleza ilani hiyo kwa asilimia 80.

Alisema hatua ya kufanyika kwa kikao cha NEC Butiama, kunatokana na maamuzi ya kikao hicho hicho ya kutaka kuona vikao vyake vikifanyika mkoa mmoja baada ya mwingine, huku Mara ikipewa nafasi ya kwanza.
Alisema pia mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili - Jumamosi na Jumapili ya wiki hii, unalenga kuleta umoja na mshikamano ndani ya chama na taifa kwa ujmla.

Source: Tanzania Daima
 
..kwa serikali/sirikali gani waliyonayo!

..anayeweza mwita huyo ni serikali pekee [mwajiri wake]!

DAR si LAMU,

Chama chochote kipo kwasababu kinataka kutawala nchi. Sasa wataandaa vipi
programs zao kama hawawezi kukutana na gavana hata wakitaka?

Naamini CHADEMA au wengine wakiataka kukutana na gavana itawezekana.
 
Mathayo jamani aliwalisha watu nyumbu hapa Musoma .Hivi kesi yake imeishia wapi ?
 
THATS WASSSUPP!!!,

U gotta love these Musoma people, sasa hali hii iendelee sehemu zote nchini na zaidi watu wa reflect haya kwenye ballot boxes.
 
Wito kwa watanzania wenzangu,mimi nimejifunza somo kubwa sana kwa watu wa Musoma na hii ndio inatakiwa hadi pale 20010,CCM tuwalambishe mchanga kwanza ndio adabu itawasogea vinginevyo watatufanya malofa hadi siku ya mwisho.

Watu wa musoma nawapa BIG UP kubwa.
 
Jamani leo ni alhamisi,tusiandikie mate na wino upo.Kwani Jumapili mnadhani iko mbali la hasha,mambo yatakua hadharani mtu wangu,hapo tutajua sisiem ni ileile ya kisanii au ni sisiem mpya.Baada ya kikao cha Butiama naamini tutapata mwelekeo wa CCM kama ni aidha kuendelea kuwakumbatia mafisadi au wanataka kuepukana nao hapo ndio tutapata majibu.

Mimi binafsi sitegemei jipya.Naomba kuuliza hivi na Msekwa yumo ktk hiyo NEC ya CCM?
 
Mimi sitegemei jipya zaidi ya usanii wa kutufurahisha wananchi lakini ambao hautaleta mabadiliko makubwa.

Kungelikuwa na njia ya kuwagombanisha CCM huko Butiama ili baada ya hapo wagawanyike ingelikuwa nzuri zaidi. Lakini kwasababu ya ulaji, atakachosema JK ndicho hicho hicho kitapita.

Wataishia kuunguza pesa bila jambo la maana kuonekana.
 
Hivyo ndivyo itakavyokuwa maana ndivyo tulivyo!

Nimecheka sana sana .Na mimi nasema wacha nitasema mengi toka Butiama . Salaam toka Orange Tree Hotel .Hapa wapo vingunge na mimi niko Mujungu Gueste house .Yatakayo jiriri nitasema ila Musoma imekuwa kama Hollywood ila Wajita, Wakurya, Wakome, Wazanaki na wengine wamediriki kuzomea kwa uwazi Mbunge wao Mathayo na ujumbe wa wana NEC. Hili wamenikumbusha jinsi Mathayo alivyo kataliwa hadi akaja Magufuli akaja kuingilia kati lakini alishinda kwa kuua nyumbu 40 wakala akawasimamia wakapiga kura .
 
Thanks GOD Lunyungu uko online...

Nilikuwa nimeanza kuwa na wasiwasi baada ya kutokuona kwa muda!
Hiyo ya viwanja vya mkendo itabidi waandike historia, embu tupe newz ya kinachoendelea huko!
 
Hivi jamani kweli hata kama uelewa wangu ni mdogo,lakini ninavyojua mimi ni kwamba hicho kikao ni cha wanachama wa CCM ambao ni NEC.Sasa huyu Ndulu na yeye ni NEC au wanataka kumkolimba,mbona sioni logic ya Ndulu kwenda Bitiama?

Kwani NEC ni chombo ambacho kinaweza au kinamamlaka ya kumwita mtu yoyote na ikamuhoji juu ya jambo fulani,mbona naona kama wako nje ya mipaka ya utendaji wao wa kazi na pia naona kama wanaingilia kazi za kimahakama.

Jamani Makamba hivi huoni aibu kusema eti mnakwenda Butiama kumuenzi baba wa Taifa,hivi hamuoni kama mnachekesha?Hivi mzinzi anaweza leo hii akafunga safari kwenda Roma eti ankwenda kumuenzi Pope John Paul wa pili,hii sio kichekesho kweli,makamba umezidi masiala.Hivi CCM kupeleka kikao Butiama huku mkiwa mnanuka madhambi hamuoni kama mnamdhalilisha Hayati baba wa Taifa,haya litakalo watokea baada ya kufanya upuuzi wenu sisi hatumo.

Kwenu NEC,mimi nadhani kikao cha Butiama kama kingelenga toba na ikawa toba ya kweli,CCM mngejiimarisha sana lakini kwa kua mmekanusha kwa kusema hamwendi But'kutubu mmelikoroga na mtalinywa wenyewe.
 
Mathayo jamani aliwalisha watu nyumbu hapa Musoma .Hivi kesi yake imeishia wapi ?

Huyu Mathayo amefanya uovu mwingi sana huko musoma na nina hakika Lunyungu ana file lake zima.... sasa ngoja aanze kuanikwa taratibu.

Unajua mwaka 1995, mkoa wa mara ulikuwa miongoni mwa mikoa michache bara iliyowachagua wapinzani (na matokeo yakakubaliwa na tume ya uchaguzi) zaidi ya ccm!?
 
Mkuu Heshima mbele, mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, lakini no way kwamba I am a clown, vipi next time ukirekebisha hii lugha ambayo kwa kweli siyo ya kistaarabu, kutumiwa tena kwenye jamii kama hii, mimi nilifikiri tunaikataa hii lugha kwa waliotuvamia, sasa na wewe wa muda mrefu ukiitumia tutawaambia nini waliotuvamia?.

1. CCM ni chama kinachotawala Tanzania, kwa ridhaa ya wananchi waliokikubali kwa kuwapigia kura kutokana na kukubali sera zao, moja ya sera za CCM kwa taifa, ambazo waliziahidi kwenye kampeni za uchaguzi, ni pamoja na uchumi wetu ambao nguvu yake kubwa hutokea BOT, sasa CCM watafanya vipi mkutano mzito bila ya gavana? I mean regardless ya how our uchumi si doing, which as usual ni a debatable ishu, lakini ni haki not only kwa CCM, bali hata vyama vya upinzani kumuita vinapokuwa na mikutano yao mikubwa.

2. Mkuu ninaamini kwamba ungekuwa na hoja nzito sana, iwapo gavana wetu wa BOT, angekuwa in the past amewahi kuitwa kwenye mikutano mizito ya vyama vya upinzani, akakataa au CCM ikamkatalia aisende,

Otherwise, naona kama sio a weak argument, basi hakuna argument kabisaa, gavana ni lazima aende kule kwenye kikao kikubwa cha CCM, yaaani chama tawala, ili aweke mambo wazi exactly yalipo na pia wajumbe wa NEC, wapate nafasi ya kumuuliza maswali muhimu huku waziri wa hazina akiwepo, kuepuka kutupiana lawama, kama alivyofanya Mama Meghji, this time wote watakuwepo yaani waziri na gavana, I thought CCM ought to be louded kwa hiki kitendo kuliko kushambuliwa. To me the move sounds good, na ni matumaini yangu kuwa opposition wata-follow the idea in the future, wakikataliwa then tutamkoma nyani.

Ahsante Wakuu.

Heshima Mzee:

Lakini hapa unachemsha. Watumishi wa serikali ambao nafasi zao sio za kisiasa hawatakiwi kuwapo kwenye mikutano ya vyama.

Kama sera za chama chenu ni za uchumi, mnaweza kufanya hivyo kwa kumwita waziri wa fedha na manaibu zake au kumwita waziri wa miundo mbiu za mikoa kwa sababu hao wanashikiria nafasi za kisiasa na ni wanachama wa CCM.

Masuala ya ulinzi na usalama ni muhimu. Kwanini basi mkuu wa majeshi ya ulinzi au Inspector mkuu wa polisi asiende huko.

Vilevile Tanzania ina matatizo ya njaa, kwani mabwana shamba hawapo kwenye kikao hicho?

Wanasiasa ni lazima mkubali kuwa kazi zingine ni professions ambazo hazitakiwi kuingiliwa kisiasa.
 
Huyu Mathayo amefanya uovu mwingi sana huko musoma na nina hakika Lunyungu ana file lake zima.... sasa ngoja aanze kuanikwa taratibu.

Unajua mwaka 1995, mkoa wa mara ulikuwa miongoni mwa mikoa michache bara iliyowachagua wapinzani (na matokeo yakakubaliwa na tume ya uchaguzi) zaidi ya ccm!?

Musoma ina madume sawa na kule kwa Kabwe .Hawa ndiyo walilinda kura za Wangwe kule Tarime na FFU walimwagwa na Msimamizi wa Tarime wa Uchaguzi alipotoka nje alikuta hali ni ngumu akarudi akamtangaza Wangwe baada ya shinikizo la kutaka kumtangaza mgombea wa CCM.Musoma Mathayo alichinja nyumbu watu wakala lakini wakamchagua Wandwe na kupora matokeo yake .

Musoma Mathayo anahusishwa na kuua mtu na yeye kuendelea kufanya biashara haramu ya mafuta .Mathayo ni kijana mdogo aliyemaliza form 2 akafukuzwa Makokose Seminary kwa kuwa alikuwa na akili Mgando ambaye ni Bilionea mkubwa kisa mafuta haya mafuta .

Mathayo hatakiwi lakini nadhani alisahau yaliyo mpata Shein akiwa Musoma , JK na Lowasa hadi akfikia kuwadharau wana Tarime Bungeni .Musoma ina madume bwana .Kama huamini njoo leo uone watu wanapita pita na sherehe wenzao wanavua samaki na kuwaa angalia tu .
 
Back
Top Bottom